ELECTIONS COMMITTEE TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MAAMUZI KUHUSU RUFAA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI ZA UCHAGUZI VYAMA VYA MPIRA WA ...
ELECTIONS COMMITTEE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAMUZI KUHUSU RUFAA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI ZA UCHAGUZI
VYAMA VYA MPIRA WA
MIGUU MKOA WA MBEYA (MREFA), MKOA WA SHINYANGA (SHIREFA) NA MKOA
WA DAR ES SALAAA
(DRFA).
19 OKTOBA 2012
1.
Kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Kanuni za Uchaguzi
za wanachama wa TFF, Ibara ya 10(6), 12(1)na 26(2) na
(3), Kamati ya Uchaguzi ya
TFFkatika vikao vyake vilivyofanyika tarehe 12 na 18 Oktoba 2012
ilijadili michakato
ya chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ya Mbeya (MREFA),
Shinyanga
(SHIREFA) na Dar es Salaam (DRFA) na kutoa maamuzi
kama ifuatavyo:
(a)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA)
(i)
Rufaa ya Ndg. Charles Makwaza:Kamati ilijadili rufaa
iliyowasilishwa na Ndg. Charles Makwazadhidi ya Kamati ya Uchaguzi
ya MREFA,
iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kubatilisha uamuzi wa Kamati
ya Uchaguzi ya
MREFA kumpitisha Ndg. John Mwamwaja kugombea nafasi ya Mwenyekiti
wa MREFA, kwamba
hakutekeleza wajibu wa kikatiba wa kuitisha Mkutano Mkuu wa MREFA
kwa muda wa miaka
3.
Baada ya kupitia maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF
ilijiridhisha kuwa vielelezo na maelezo yaNdg. Charles Makwaza
yaliyowasilishwa
mbele ya Kamati kwa kiwango kikubwa hayakuwa ya kweli. Kamati ya
Uchaguzi ya
TFFimeitupa rufaa hiyo.
(ii)
Rufaa ya Ndg. Lusekelo E. Mwanjala:Kamati ilijadili rufaa
iliyowasilishwa na Ndg. Lusekelo E. Mwanjala ikipinga
maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi
ya MREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Mwenyekiti
wa MREFA, kwa kigezo cha
kutokuwa na uzoefu wa uongozi wa mpira wa Miguu.
Kamati ilipitia vielelezo kuhusu rufaa na kujadili maelezo ya
Mrufani na Mrufaniwa
na ilijiridhisha kuwa Ndg. Mwanjala anakidhi kigezo cha uzoefu.
Kamati inakubaliana
na rufaa ya mrufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya MREFA
na hivyo
imemrejeshaNdg. Mwanjala kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa
MREFA.
(iii)
Rufaa ya Ndg. Thadeo T. Kalua:Kamati ilijadili rufaa
iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Kalua ikipinga
maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya
MREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa TFF, kwa
kigezo cha kutokuwa Mkazi wa Mkoa wa Mbeya. Kamati ilipitia
vielelezo kuhusu rufaa
hii na kubaini kuwa Katiba ya MREFA iliyosajiliwa haina sharti
hilo kwa waombaji
uongozi. Kamati inakubaliana na maombi ya
(iv)
mrufaa na inamrejeshaNdg. Thadeo Kalua kugombea nafasi ya Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa TFF.
(v)
Uchaguzi wa MREFAutafanyika Jumamosi, tarehe 27 Oktoba 2012 kama
ulivyopangwa.
(b)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA).
(i)
Rufaa ya Ndg. Ibrahim Magoma:Kamati ilijadili rufaa
iliyowasilishwa na Ndg. Magoma ikipinga maamuzi yaKamati ya
Uchaguzi ya SHIREFA
kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Katibu wa SHIREFA, kwa
kigezo cha kuingilia
Mchakato wa Uchaguzi kunyume na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa
TFF na pia
kutozingatia matakwa ya Kanuni hizo katika kujaza fomu za maombi
ya uongozi wa
SHIREFA.
Kamati ilipitia vielelezo kuhusu rufaa ya Ndg. Magoma na kujadili
maelezo ya Mrufani
na Mrufaniwa na ilijiridhisha kuwa Ndg. Magoma aliingilia
mchakato wa uchaguzi wa
SHIREFA kunyume na Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF akiwa
Katibu Mkuu wa
SHIREFA kwa kushiriki kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA
iliyokuwa ikendelea na
mchakato wa uchaguzi wa SHIREFA. Kamati inakubaliana na
uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya SHIREFA wa kumwondoa Ndg. Magoma kugombea nafasi ya
Katibu wa SHIREFA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFFimeitupa rufaa hiyo.
(ii)
Uchaguzi wa SHIREFAumesogezwa Mbele kwa siku nne. Uchaguzi huo
utafanyika Alhamisi, tarehe 25 Oktoba 2012, mjini Shinyanga.
(c)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijadili Mchakato wa Uchaguzi wa DRFA
na rufaa dhidi ya
maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na kuamua kama
ifuatavyo:
(i)
Marekebisho na usajili wa Katiba ya DRFA:Hoja ya rufaa
iliwasilishwa na Ndg. Michael R. Wambura ilikihoji uhalali wa
marekebisho na usajili
wa Katiba ya DRFA, kwamba usajili wa Katiba ya DRFA si halali.
Kamati ilibaini kuwa
marekebisho ya Katiba hiyo yalifanyika kwa kufuata maagizo ya TFF
na kwamba DRFA
ilizingatia maagizo hayo. Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliridhika
kuwa Katiba ya DRFA
imesajiliwa na Msajili wa vyama na vilabu vya michezo baada ya
kuridhiwa na TFF, na
hivyo, Kamati iliitupa hoja hiyo ya Mrufani kuhusu uhalali na
usajili wa Katiba ya
DRFA.
(ii)
Kuundwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF :Hoja ya rufaa ya Ndg.
Michael R. Wambura iliomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa tamko
kuwa Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA imeundwa bila kufuata Kanuni za Uchaguzi Ibara ya
3(2). Kamati
iliridhika kuwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA iliteuliwa kabla ya
marekebisho ya Kanuni
za Uchaguzi za wanachama wa TFF hususan, Ibara ya 3(2),
hivyo uteuzi wa wajumbe wa
Kamati hiyo haukukiuka Kanuni za Uchaguzi. Kamati iliitupa rufaa
hiyo.
(iii)
Wapiga kura wa Mkutano Mkuu wa DRFA:Hoja za rufaa za Ndg.
Michael R. Wambura na Ndg. Juma Jabir ziliomba kuyaondoa majina ya
Ndg. Abeid Mziba,
Ndg. Salehe Ndonga, Peter Muhinzi na Ndg. Daudi Kanuti katika
orodha ya wapiga kura
wa Mkutano Mkuu wa DRFA na uongozi wa wanachama wa DRFA, kwamba
hawana sifa kwa
mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba za wanachama wa DRFA.
Kamati ya Uchaguzi ya
TFF haikupata vielelezo kuhusu hoja iliyowasisilishwa mbele ya
Kamati na hivyo
kuitupa hoja hiyo ya mrufani.
(iv)
Rufaa dhidi ya Ndg. Mohamed Salim (Bakhressa) kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa DRFA. Rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA wa
kumpitisha Ndg. Amin Mohamed Salim (Bakhressa) kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa DRFA
iliyowasilishwa na Ndg. Michael R. Wambura na Ndg. Juma
Jabiriliomba jina la Ndg.
Amin Mohamed Salim (Bakhressa) liondolewe katika orodha ya
wagombea uongozi wa DRFA
kwa nafasi ya Mwenyekiti, kwa kuwa hana elimu ya kiwango cha
kidato cha nne na hivyo
kutokidhi matakwa ya Katiba ya DRFA Ibara ya 29(2) inayotamka
kwamba ‘Mtu yeyote
anayegombea nafasi yoyote ya DRFA hana budi awe na kiwango cha
elimu kisichopungua
kidato cha nne (Academic Certificate of Ordinary Secondary
Education).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia vielelezo kuhusu rufaa dhidi ya
maamuzi ya Kamati
ya Uchaguzi ya DRFA na kujadili maelezo ya Warufani, Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA na
Ndg. Amin Mohamed Salim na ilijiridhisha kuwa Ndg. Amin Mohamed
Salim (Bakhressa)
hana elimu ya kiwango cha kidato cha nne na hivyo hakidhi matakwa
ya Katiba ya DRFA
Ibara 29(2). Kwa kutokidhi matakwa hayo ya katiba ya DRFA, Ndg.
Amin Mohamed Salim
(Bakhressa) hastahili kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa DRFA.
Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inakubaliana na maombi ya Warufaa.
(v)
Rufaa kupinga kuenguliwa kugombea Uongozi DRFA: Ndg. Evans
Elieza na Ndg. Juma Jabir waliwasilisha rufaa wakiomba
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kutengua uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA wa kuwaengua
kugombea uongozi kwa
madai ya kugushi sahihi ya Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya
ya Kinondoni
(KIFA). Katika vielelezo mbalimbali vilivyoletwa mbele ya Kamati
na baada ya
kuwahoji warufani, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA,
Katibu wa KIFA, Ndg.
Seif Ally Mailo aliyeshuhudiamaelezo ya fomu za waombaji uongozi
DRFA na baadhi ya
waombaji uongozi ambao kupitishwa kwao na Kamati ya Uchaguzi ya
DRFA kulilalamikiwa,
Kamati ilibaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na
taratibu za uchaguzi
zilizofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na pia ama KIFA au
wagombea wenyewe.
Kutokana na mkanganyiko, maelezo yenye utata kutoka kwa warufani
na warufaniwa na
maamuzi ya utata ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA
yameufanya mchakato wa
uchaguzi wa DRFA kupoteza hadhi ya uchaguzi unaozingatia
Kanuni za Uchaguzi na misingi ya demokrasia na uwazi kama
ilivyoainishwa kwenye
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijiridhisha
kwamba:
· Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA iliwapitisha wagombea Ndg. Gungurugwa Tambaza,
Ndg. Mohammed Bhinda, Ndg. Benny Kisaka na Ndg. Hamisi Ayoub Mpapai
bila kuwa na
vielelezo vinavyothibitisha kuwa wana kiwango cha elimu
kisichopungua kidato cha nne
(Academic Certificate of Ordinary Secondary Education).
· Hoja ya kughushi
saini ya Katibu wa KIFA katika kushuhudia maelezo ya
baadhi ya wombaji uongozi, ambayo ilitumiwa na Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA kuwaondoa
kugombea uongozi waombaji uongozi watano (5) Ndg. Hamis
Ambar, Ndg. Hamisi Kisiwa,
Ndg. Andrew Tupa, Ndg. Evans Elieza na Ndg. Juma Jabir
haikutumika kuwaondoa baadhi
wagombea ingawa fomu za waombaji uongozi saba zilisainiwa na
Ndg. Ndg. Seif Ally
Mailo.
· Ndg. Seif Ally
Mailo ambaye si mwajiriwa na si kiongozi wa KIFA hakuwa na
mamlaka ya kushuhudia maelezo ya wagombea kwa mujibu wa Kanuni za
Uchaguzi.
· Kulikuwa na hali
ya kumficha Ndg. Seif Ally Mailo aliyesaini fomu za
wagombea walioenguliwa kwa kigezo cha kughushi saini asifike
kwenye kamati ya
Uchaguzi ya TFF kutoa maelezo kuhusu ushiriki wake katika mchakato
wa uchaguzi wa
DRFA.
· Fomu za wagombea
Ndg. Said H.Tully na Ndg. Shaffih Dauda zilizojadiliwa na
Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na hivyo kupitishwa na Kamati hiyo
zilichezewa
(tempered-with) kwa kunyofolewa baadhi ya kurasa na kuwekwa kurasa
zenye maelezo na
saini ambazo si za Ndg. Said H.Tully na Ndg. Shaffih Dauda.
Wagombea hao ambao
walikuwa wamepetishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kwa maelezo
kwamba fomu zao
zilikuwa zimeshudiwa kwa sahihi halali ya Ndg. Ndg. Seif Ally
Mailo
walikana kwa maandishi na kutoa vielelezo vilivyothibitisha kwamba
fomu zao
zilichezewa na maelezo yaliyo kwenye kurasa zilizobadilishwa siyo
wao walioyandika
na kusaini.
· Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA iliwaondoa baadhi ya waombaji uongozi kwa
maelezo kwamba maelezo kwenye fomu za wagombea hao hayakushuhudiwa
na viongozi vyama
wanachama wa DRFA wenye mamlaka ya kushuhudia maelezo ya waombaji
uongozi lakini
bila kuzingatia matakwa hayo ya kikanuni ikawapitisha kugombea
Ndg. Muhsin S.
Balhabou na Ndg. Benny Kisaka ambao maelezo ya kwenye fomu zao
hayakushuhudiwa na
kiongozi wa chama mwanachama yeyote wa DRFA.
· Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA inahusika kwa kiwango kikubwa katika ukiukwaji
wa Kanuni na taratibu za uchaguzi na kutozingatia matakwa ya
Katiba ya DRFA katika
mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa DRFA.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Katiba ya TFF Ibara ya
49(1), Kanuni za
Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10(6), 12(1)na
26(2) na (3):
(i)
Imeifuta Kamati ya Uchaguzi ya DRFA. DRFA inaagizwa kuteuwa
Kamati mpya ya Uchaguzi itakayoandaa na kutekeleza majukumu yake
ikizingatia Kanuni
za Uchaguzi za wanachama wa TFF na Katiba ya DRFA. Uteuzi wa
Kamati mpya ya Uchaguzi
ya DRFA ufanyike kabla ya tarehe 25 Oktoba 2012
(ii)
Imefuta mchakato wa Uchaguzi wa DRFA. Mchakato wa uchaguzi
utaanza upya tarehe 29 Oktoba 2012 na uchaguzi utafanyika tarehe
08 Desemba
2012.Wagombea wote waliokuwa wamelipia Fomu za maombi ya uongozi
(Fomu Na. 1)
wanaokidhi sifa za kugombea uongozi kwa mujibu wa Katiba ya DRFA
na Kanuni za
Uchaguzi za wanachama wa TFF wajaze upya Fomu Na.1 bila kutozwa
ada kwa nafasi
zinazoendana na zile walizokuwa wameomba kugombea.
Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
COMMENTS