Saa 37 za Dar hadi Mpanda

. Mama moyo wangu! yaani mashaka na hofu  barabarani,msituni .Dereva macho pima, abiria mapenzi, kinywaji,kuchimba dawa .Kondakta gari...


.Mama moyo wangu! yaani mashaka na hofu  barabarani,msituni
.Dereva macho pima, abiria mapenzi, kinywaji,kuchimba dawa
.Kondakta gari halijai si ndoo ya maji,sogea kule,ukiwa mzee balaa


NIMETUMIA takribani saa 37 kutoka Dar es salaam na kufika katika makao makuu ya mkoa wa Katavi, mji unaonekana kubadilika kwa kasi wa Mpanda.Na ninachoandika hapa si hadithi ya kubuni ni ukweli nikichukua muda hadi muda.

Majira ni saa kumi na nusu alfajiri,naamshwa na watoto, nisije nikachelewa kwani basi linaondoka saa moja kasoro robo na kwa utata wa usafiri wa huku kwetu nikaapo, ni lazima ujihimu kidogo.Saa kumi na moja na dakika 15 naondoka nyumbani na dakika 25 baadaye nafika stendi ya kunipeleka Kimara, hakuna basi , muda unaenda naamua kuchukua pikipiki.

Saa kumi na mbili na nusu ninafika Kimara, nasubiri basi litakalonichukua hadi Mpanda kwa kupitia Mbeya na Sumbawanga, sikujua kwamba nitalazimika kulala Mbeya; wenyewe waliniambia kwamba niwape 67,000 na nitafikishwa Mpanda hawakunipa hadhari kwamba ni lazima nijitegemee kulala Mbeya na tena nikifika Sumbawanga ni lazima niingie katika gari nyingine na hivyo kuhamisha mizigo yangu.

Moja kasoro nikawapigia simu kwamba abiria wenu wa Kimara nawasubiri,wakaniuliza gari la saa ngapi,nikawaambia la moja kasoro wakasema linakuja wakanitajia gari namba 616 kwamba ndilo litakalonichukua kuelekea Mpanda, mkoa mpya wa Katavi.

Wakati nashangaa kunataka kutokea nini pale kituoni , daladala akabanana na basi ninalosafiria,akalambwa kioo nikasema ohoo ishakuwa nuksi tena, manake hapa hamjatoka Dar, dereva kaonesha kutojua upana wa gari lake.Nikalifuata pale nikaingia, wakamalizana tukaanza safari kuelekea Mpanda.

Mbezi tukachukua abiria mbele kidogo tukaanza mwendo. Basi lilitakiwa kuwa lakshari, lakini haa, ndani utadhani halikaguliwi na Sumatra manake viti hovyo, mikanda haipo na stuff carrier ilionekana kama inataka kuachia japo ilitengenezwa kama yale ya kwenye ndege.

Mhh sikuwa pekee yangu aliyeshangaa, mtu aliyepanda Mbezi naye alishangaa, wale waliokuwapo wakasema what kind of a car, ilikuwa kiinglish lakini matamshi yake yalifanana na watu wanaotoka Zambia, Wanyanja wakijiuliza ni aina gani ya gari wamo,kwani wanatazama mle ndani silo walilooneshwa jana yake wakati wakikata tiketi linapiga madebe kwelikweli kwa ndani.

"Halafu konda hii bei ni ya lakshari kinywaji kipo? manake basi lenyewe halielewekieleweki" alijibiwa kiinywaji kipo lakini  he Dar hadi Mbeya tulipewa kwa lazima Cocacola ya kwenye plastiki hawakuwa na kinywaji kingine na wala maji hawakutoa.Walitupa kinywaji hiki kabla ya kuingia Doma, mara tu baada ya kumaliza kuchimba dawa.

Mbali baada ya kuanza kupata mwendo tukaingia foleni ya Kibaha na mbele ya Kibaha akapanda mama analalamika kwelikweli kaachwa na basi la kampuni hiyo,kumbe asubuhi kampuni ile iliamua kukodisha basi bila taarifa kwa watu wakajiendea tu.

Njiani jamaa anaovateki magari matatu manne na unajua barabara ya Dar-Chalinze ilivyo, ikiwa na mibinuko ya ajabu, jamaa anazipangua anaziweka, hapo roho inaanza kuwa mkononi, unashangaa umpigie Mpinga au nani barabarani na namba walizosema wanaweka kwenye mabasi mle haipo, unakula uchungu , mama moyo wangu! breki vuu, ghafla mnaingia kushoto. Mashaka barabara ya lami.

Haya  bora salama, Mungu anasaidia mnaacha miti ikirejea nyuma na nyie mkisonga mbele mnaingia Morogoro, stendi ya Msamvu unapumua,mnapakia abiria wengine, wanatoa chati kwa Sumatra na Polisi wanaikagua wanaruhusu mnaingia barabarani tena mnaanza kuitafuta Mikumi, Mbele kidogo kabla ya kufika Doma  Kondakta anaelezea suala la kuchimba dawa. Wazungu kama tisa hivi waliokuwa mle ndani hawakuelewa nini kinatokea.

" kuchimba dawa,”  anashangaa .. "kuchimba ni to dig, dawa medicine maana yake nini hasa" akajiuliza mtu aliyeonekana anajua kiswahili zaidi ya wenzake walitaka maelezo.Watu (watumishi wa basi) hawakuzungumza Kiinglish lakini walipoona, watu wanateremka waliteremka na wakabaini kwamba ni suala la kujisaidia.

Unakumbuka maneno  ya kuwepo na vyoo kwa ajili ya abiria njiani , choo kile kinauwezo wa watu watatno, abiria sitini, wengine na wazungu kadhaa waliingia msituni huku  karibu na barabara kuna gulio la nyama.

Mnamaliza kuchimba dawa mnaingia , mnapita mbuga ya Mikumi na spidi 110 wakati wenyewe wameweka matuta na kusema spidi inayofaa ni nusu yake, unashangaa mkikutana na tembo itakuaje , ama tembo ama nyie.

Njiani sasa simulizi zinaanza zimeanzia katika suala la kuchimba dawa. Masimulizi yanahama kushutumu serikali na matamko yake,wakaingia hapo kuzungumzia urais na nia za akina fulani wakiwataja kwa majina kwamba wanawania Urais huku wakiwa wagonjwa na wala hawawezi kabisa kuongoza taifa.

Siasa za kuanzia Morogoro hadi Comfort zilikuwa za wastani, wakichamba elimu na kusifia namna watoto wanaojifunza Uganda walivyokuwa na akili kuliko Tanzania kwa kuwa wanajua kupepeta Kiingereza.

"ahh kwa wale wa Uganda labda kiingereza lakini uchambuzi na uelewa bure kabisa" niligeuka kutazama wanaozungumza nikagundua ni vijana. Hawa walibishana kwelikweli manake walisema kwamba mfumo wa elimu tanzania bado ni bomba  mwingine akisema kwamba si kweli elimu ya Tanzania imeoza watu wanajiumajiuma katika kujieleza.

Comfort, pale Kitonga tuliingia mapema,pamoja na ukweli kuwa eneo limechakaa, hata akili za watu zimechakaa sana kwani wanauza bidhaa kama wapo Mogadishu, aina moja bei ghali urafiki haupo,  bure kabisa!

Mnamaliza  mnaondoka, mtu na mkewe (vijana hao!) gari limepiga mijihoni hawakusikia wala kuona na  asali zikiwamiminika (si bure wameona juzi hawa) tuko juu kelele mtindo mzima, bahati yao tulikuwa bado kuingia barabara kuu na mzee moja akashtuka kiti kimoja hakina abiria.

"Mmeacha mtu na mkewe" anasema  huku mtu mmoja njiani mbele anapunga kwa nguvu kuashiria watu wanaokimbilia gari.Walipanda hawana hata sura ya hasira wakaendelea na asali zao, hawa niliwapenda.

Kitonga ilipandishwa kama tambarare, siasa zikaelekea kwenye shimo kubwa zaidi nani anafaa kuwa rais, wote wakawa wanajadiliana wagombea wa CCM badala ya kuangalia na vyama vingine unasema kaazi kwelikweli.Ukimtazama dereva, haongei na mtu anabadilisha gia,anakanyaga mafuta huku mguu upo kwenye breki kama anaibia vile, staili ngumu zaidi. Kwa mwendo ule lazima awe macho pima.

Saa tatu mnaingia Mbeya, unadhani mnaendelea:"wale abiria wa Mpanda na Sumbawanga tukiingia mjini mfike ofisini kwa maelezo, mshuke na mizigo yenu"

Kweli tulifika maelezo ni kuwa uripoti saa kumi na moja na nusu na basi linaondoka saa 12 kamili kuelekea Mpanda nba wale wa Sumbawanga wakaambiwa saa mbili asubuhi. Wapi pa kulala, mzee sio ndege uko tranziti, wewe tafuta gesti zipo nyingi la maana kesho uawahi.

Naam linakushuka,usiku wewe mgeni, unampa mtu buku anakutoa kidogo stendi anakufikisha gesti inaitwa sinahela. Unalala, umechoka hata hujui itakuwaje saa kumi na moja hiyo unaomba msaada wa kuamshwa na mlinzi. Unagusa maji ya baridi, unauliza maji vipi unaletewa maji ya moto unaoga na fasta unalala.

Wala huhitaji kuamshwa, kwani usingizi wenyewe unao?Anafika kukugongea anakukuta wewe unatoka kuoga angalau uchangamke. Unasubiri kupambazuke unauliza je salama anakuambia salama. unaondoka na kufika stendi.

Unauliza ofisini basi la kwenda Mpanda wanakuambia mngoje mhusika. Mhusika haji unatoka nje unaenda katika magari unauliza la Mpanda wanakuonesha unasema duhh hii kali unaingia kukaa katika kiti cha pembeni aliyekaa kala kiti kimoja na nusu halafu unajiangalia mwenyewe.
pembeni mwako wapo watu na asubuhi ile wanazungumzia siasa, masuala ya sensa na jinsi wengine walivyogomea sensa.

Siasa za kuanzia Mbeya kuelekea Mpanda zilikuwa ni ukali wa Chadema,na kutokuwa wavumilivu. He mwenzio kama jamaa yangu na khanga yake ya CCM kafua kaianika wanakuja watu wenye nyumba wanaanza nani kaweka balaa hili atowe mara moja, khanga ile si ilikuwa na maji wakamlaimisha aiondoe pale.

"Jamani chadema sijui vipi yaani washari shari".

Tukaondoka kondakta akisema wazi hataki mtu wa kusimamisha huku dereva akilalamikia upangaji mbaya wa mizigonutamletea taabu kwenye mizani. Tuliondoka njiani kote hakuna kupandisha wala kuongeza tukapita mizani, tukaingia Tunduma tulipoachana na Polisi wa Tunduma na kutokomea zaidi katika barabara ya vumbi inayojengwa, basi lilikuwa halijai labda ndoo ya maji.

Akaingia mtu mzima akaona haina maana akaweka begi lake chini, akalikalia konda akasema weee!!! wala bibi hakujibu, mdada mmoja akasema mhh wazee hawa wana lao, jamaa anasema wala hamjibu anayetaka kupita aende nyuma yake na apite tu, anagemesha bega lake pembeni umruke. Inayojaa ndoo ya maji si basi.

Njiani wanapanda wawili, mvulana na msichana inaonekana wanajuana. wanakimwaga cha nyumbani lakini mvulana akamuona demu mmoja rangi ya chungwa amesimama, akamwambia binti aliyeingia naye aanzishwe swaga za mapenzi, jamaa alisahau kwamba kibantu tunasikilizana kwa asilimia 50 nikafuatilia maagizo.

Mapenzi yalinoga sana katika gari hili la Mbeya kwenda Mpanda. Jamaa alikuwa tayari kumshusha Laela binti wa watu na kumpandisha gari kesho yake, mtoto akamsikiliza akamtolea nje.Akasema anajeuri ya fedha alikuwa anafika laela kununua spea ya pikipiki yake, kisha simu hiyo inayothibitisha kwamba ni dereva wa pikipiki jamaa anatafuta usafiri akamwambia yupon garini anaenda laela kutwaa spea ya waya wa eksereta umekatika.

Anamaliza anaendelea kumpelekea rapu za mapenzi msichana yule hadi anafika Laela akitaka kumpa fedha za kushika:Nikasema watu wanahatari humjui mtu katoka wapi unataka kushuka naye.

Masikio yangu yalikuwa na utamu mkubwa, huku mapenzi, huku uongozi ujao na katiba huku mama mmoja akisema kwamba haoni sababu ya kupiga kura,wengine wakisema ni wajibu wake kuchagua viongozi.. wewe wanakusaidia nini au tuseme wameshakusaidia nini.

Masikio yangu yalinogeshwa na siasa,mapenzi yanaendelea na kisha inakuja suala la barabara. Vumbi linatimka watu wamefunga vioo  kondakta akagundua wageni wengi ndani ya basi. Jamani msifunge vioo tutakufa  wacheni vumbi liingie na kutoka. Basi limejaa ndindindi. lahela sick love boy akashuka na mbele kidogo tukanasa katika maji madogo kwenye barabara inayotengenezwa.

He tunashtukia tunaelekea katika majumba ya watu basi limeacha njia, vile vimaji kidogo katika barabara viliharibu kabisa eneo tunalopita. maji yale yalimwagwa katika barabara inayojengwa. Mhh ilituchukua dakika 15 kutoka hapo, watu wengine waliamua kutumia muda huo kuchimba dawa.

"Hawa wajanja wanataka kumaliza barabara hii muda mfupi nkabla ya uchaguzi kujipa maileji" anasema mtu mmoja.Ahh tunajenga na madafu yetu tunachelewa kodi hatulipi.. hapana bwana fedha hizi mbona ni za MCC. " Nakuambia kumbe watu wanajua na uwezo wa kubishana upo, wanasema kuhusu uchelewefu halafu wanauliza rais kwanini alimuondoa Magufuli.

Baada ya kukamata mwendo sasa ukafika muda rasmi wa kuchimba dawa, watu waliposhushwa kulikuwa na mti wa matunda pori, wenyeji wanajua wakaanza usijisaidie hapo( kwa lile neno halisi) kuna matunda , watu wakaenda mbali kujisaidia wakirejea wanachukua matunda hata dereva naye alifanya hivyo hivyo,ilituchukua muda kuondoka hapo.

Kutoka hapo ikawa pandisha shusha,ingia kushoto ingia kulia mpaka tukafika Sumbawanga saa 9 na nusu, nimechakaa kwa vumbi na kutokuwa na mahali pa kuegemea. Nabanwa na mwanamama aliyejaaliwa na katikati kuna mtu wa kufa mtu wamesimama.mambo hayo nikatulia watu wakawa wanashuka. Mara mzee kama unaendelea Mpanda ni basi hilo la pili hili hapa ndio mwisho wa safari.

Maskini mie nabadilisha basi mara ya tatu kwa tiketi moja ya Dar-Mpanda. Nikachukua  vitu vyangu nikaingia basi la pili, hapana mzee kwanza ofisini ukabadilishe tiketi.Vitu vyangu? Hapa Sumbawanga atakayekuibia lazima awe taahira.,

Unaweka begi kubwa unaondoka na beki lako dogo lenye vifaa vyako vya kazi.

Unabadilisha tiketi. Unaingia msalani kumeandikwa bei 200 unatoa hela unaambiwa bei 300 zi ile iliyoandikwa.

Basi linaondoka saa  kumi hapa Polisi wanafanya kazi yao wanasema zipo namba kama dereva anajaza au kukimbia tupigieni safarini salama. kweli basi lile lilikuwa na namba za RPC wa Rukwa, Mbeya, katavi na Dodoma.  Mnaanza safari,mazungumzo hapa yanabadilika, watu wote wamechoka wanatazama saa, simu zinaanza kuingia.

Kila anayejibu analalamika kuchelewa kwa gari, kumbe tulitakiwa kuwa Sumbawanga saa saba ili saa moja tuwe Mpanda.

Jirani yangu akanisimulia jinsi ilivyo hatari kusafiri usiku na kwamba basi lile lilishawahi kufanyiwa kitu mbaya na dereva yule yule. Watu walikusanywa simu na fedha huku mkusanyaji akiwa ni dereva wa Fuso lililotekwa kabla yake.

Paniki zinaanza kuingia, huwa natembea na chuo kidogo cha sala, pamoja na kumuomba Raphael, malaika mkuu kuwa nami safarini pamoja na abiria wengine na kumchunga dereva asifanye maamuzi ya kipuuzi nilianza safari ya mateso ya Kristo, kuomba ulinzi kamili kwangu , basi na abiria wengine kwa maana kulikuwa na wanawake wengi katika basi na watoto na kila mmoja kwa namna fulani alionekana kugwaya.

Dereva alichapa mwendo na wakati kiza kinaingia tulikuwa njia panda ya kwenda bandari ya Debwe, dakika 15 za ukweli za kuchimba dawa, hakuna hata choo cha kulipia watu wakajitoma katika vichaka vichafu unachagua tu pa kuweka uchafu wako pia.

Dakika 15 ziliisha na kisha tukaanza mwendo tukaingia katika Mbuga kila mtu alikuwa kimya mbele kidogo kwenye kiteremko kibaya gari likasimama, akashuka Kondakta, mara dereva akasema Hassan mbele yako kuna simba, watu wote wakataharuki, mama mmoja akafungua simu akaanza kusoma duwaa,kiza kilikuwa kimetanda. Hapa ni Lyamba la Mfipa.

Yule mtu akaingia tukaanza taratibu kushuka,mama mmoja jirani yangu akasema pale si pazuri hata kidogo wakiweka mtego hatuwezi kupona, lakini jambazi anayekaa msitu wa simba naye lazima awe kanuia kufa. Lakini ni katika hifadhi watu wanatekwa. Paniki, nikasema damu azizi ya Kristo iliyomwagika msalabani tuondolee kiwewe. hata ile ya Getsmane sikuikumbuka. Kila mmtu alionekana kivyake sana.

Saa mbili usiku bado tupo katikati ya msitu, unaowaka moto na baadaye tukaupita tukakutana na magari kadhaa na saa tatu kasoro tukaona umeme, dalili ya kumalizika kwa msitu,lakini kumbe watekaji nyara ndio maeneo yao, kijiji cha kwanza tu kutoka mbugani.

"Naomba nishuke ..."sikusikia alisema kama kwa kilugha lakini aliyeshuka usiku ule eneo lile lisilokuwa na umeme alikuwa na watoto sita akiwemo mchanga mgongoni, watu wakasema jamani usiku na watoto,ulikuwa usiku lakini kile kilikuwa kijiji, mbele watu walikuwa wakitembea.

Tulipiga mwendo, mbele zaidi kiboko akawa ametulia katikati ya barabara.Jamaa akafunga breki akazima taa akawasha. akazima tena. Alipowasha kiboko yule akajiondoa pale barabarani tukapita.

Saa nne tunaingia Mpanda hoi bin taaban, kasheshe za kutafuta mahali pa kulala.Muungwana mmoja alifika akanipokea akanifikisha nyumba ya wageni,tukala saa tano na sita kamili nilijitupa kitandani sikujua kinaendelea nini.
mwisho
https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Saa 37 za Dar hadi Mpanda
Saa 37 za Dar hadi Mpanda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFwGdXhEgIpcIz0MWwP1kPNq6d-aO0tNU7OOv3qUBDg4uLQRAqEGCB91qJ8GYiMruhf5JTQJ6fiJlqREZ0eRMNYbifY8TcRfmVLrSvLnghfZINJf_h9Lh8Ausjd169fBJRPDJMvuJNnXI8/s320/ndnai+ya+basi.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFwGdXhEgIpcIz0MWwP1kPNq6d-aO0tNU7OOv3qUBDg4uLQRAqEGCB91qJ8GYiMruhf5JTQJ6fiJlqREZ0eRMNYbifY8TcRfmVLrSvLnghfZINJf_h9Lh8Ausjd169fBJRPDJMvuJNnXI8/s72-c/ndnai+ya+basi.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/10/saa-37-za-dar-hadi-mpanda.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/10/saa-37-za-dar-hadi-mpanda.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy