SIMBA YAANZIA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi nane kesho (Oktoba ...
SIMBA YAANZIA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia
raundi nane kesho
(Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo
Simba wakiialika
Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mechi hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka
Arusha wakati waamuzi
wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka
Shinyanga. Mwamuzi wa
akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku mtathimini wa waamuzi
akiwa Charles
Mchau kutoka Moshi.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa
mechi kati ya
Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo
chini ya kocha Boris
Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu
itakuwa mwenyeji wa
JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mgambo Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo
itakuwa nyumbani Uwanja
wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika
mechi itakayochezeshwa
na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam. Oljoro JKT inayonolewa na
Mbwana Makata itakuwa
nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini
Arusha dhidi ya
African Lyon.
LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 24
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza
rasmi Oktoba 24
mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa
tofauti katika ligi
hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mechi za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24
mwaka huu ni Burkina
Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small
Kids (Majimaji,
Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja wa Wambi,
Mufindi mkoani
Iringa).
Mkamba Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa
kundi hilo Oktoba
25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka
huu kwa Polisi
Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids
(Majimaji, Songea),
Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro) na Kurugenzi
Mufindi vs Mlale JKT
(Wambi, Mufindi).
Raundi ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City
vs Mlale JKT
(Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela,
Sumbawanga),
Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi Iringa vs
Kurugenzi Mufindi
(Samora, Iringa).
Kundi B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa
Nangwanda Sijaona,
Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati
Oktoba 25 mwaka huu ni
Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na Polisi Dar es
Salaam vs Ashanti
United (Chamazi, Dar es Salaam).
Raundi ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs
Green Warriors
(Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini,
Pwani) wakati Oktoba
28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini, Pwani)
na Oktoba 29 mwaka
huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam (Chamazi, Dar es
Salaam).
Novemba 1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United (Mabatini,
Pwani), Novemba 2
mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar es
Salaam), Novemba 4
mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es Salaam) na Transit
Camp vs Moro
United (Mabatini, Pwani).
Kundi C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake
Tanganyika,
Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi
Mara (Kirumba,
Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
Raundi ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi
Dodoma (Ali Hassan
Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga),
Kanembwa FC vs Morani
(Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino Rangers (Kirumba,
Mwanza).
Oktoba 31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino
Rangers (Karume,
Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi Dodoma
vs Pamba (Jamhuri,
Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake Tanganyika, Kigoma).
MBAGA AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA
Mwamuzi Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya
(Harambee Stars) na
Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani
jijini Nairobi. Mbaga
anasaidiwa na waamuzi wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye kutoka
Mbeya na Erasmo Jesse
wa Morogoro.
TFF imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa
Shirikisho la Mpira wa
Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo ni
moja ya vipimo
kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka Ufaransa.
TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA) imeongeza
muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama
hicho ambao sasa
utafanyika Novemba 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan
Mambosasa, jana
ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa wagombea
bado umekuwa mdogo
ambapo ni watano tu waliojitokeza.
Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu
ambapo mwisho itakuwa
ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri. Fomu zinapatikana
ofisi za TAFCA
ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu
Mkuu, Katibu Msaidizi,
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati
ya Utendaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
COMMENTS