CAG AANIKA UKWELI KUHUSU PSPF ASEMA HATARINI KUFILISIKA

.Kampuni za vigogo wa CCM zatajwa kuifilisi .Ni Tan Power ya Yona na TPI ya Madabida .Ni baada ya kuchukua mikopo bila riba .Wizara ya Madin...

.Kampuni za vigogo wa CCM zatajwa kuifilisi
.Ni Tan Power ya Yona na TPI ya Madabida
.Ni baada ya kuchukua mikopo bila riba
.Wizara ya Madini yashindwa kukusanya mrahaba
 

MFUKO wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF) uko hatarini kufilisika
baada ya ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kubaini kuwa uwezo wake wa kifedha unaendelea kushuka.
 
Katika ripoti ya CAG aliyoiwasilisha bungeni inaonyesha kuwa ukadiriaji thamani wa
mfuko huo ulibaini hasara halisi ya Sh trilioni 6.5 “Hivyo mfuko uko kwenye hatari
ya kutoweza kujiendesha kama juhudi hazitachukuliwa na Serikali.”
 
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh alisema pamoja na
mfuko kuwa katika hali mbaya kifedha, amebaini kuwa mfuko ulitoa mikopo kwa
mashirika yaumma na taasisi nyingine ambayo yamedhaminiwa na Serikali yenye jumla ya
Sh bilioni 67.2 bila riba.
 
Madeni hayo ambayo hayajalipwa na hayana riba ni Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) ambayo deni lake ni Sh bilioni 54.6, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) ambayo deni lake ni Sh bilioni 6.7 na Kiwanda cha madawa Tanzania (TPI) wamekopa Sh milioni 435.1 kwenye mfuko huo.
Kiwanda hicho kinamilikiwa na makada wa  CCM ambao ni Ramadhani Madabida na mkewe
Zarina Madabida ambaye ni mbunge wa viti maalum (CCM).
 
Taasisi nyingine binafsi ambazo zimekopa kwenye mfuko huo chini ya udhamini wa
Serikali na zimeshindwsa kulipa madeni yake ni kampuni ya Tan Power Resources ambayo
imekopa Sh bilioni 5.4 bila riba.
 
Kampuni hiyo ambayo inamilikiwa na viongozi wa zamani wa Serikali Daniel Yona na
Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ndio waliokuwa na mgodi wa Makaa ya Mawe
Kiwira na baadaye wakashindwa kuuendesha na kuurejesha serikalini.
 
Serikali Kuu WIZARA ya nishati na Madini imelaumiwa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za
Serikali (CAG) kwa kushindwa kukusanya Sh bilioni 19.7 ambazo ni mirahaba ya madini.
 
Malipo hayo ni kutokana na mabadiliko ya sheria ya madini iliyorekebishwa kiwango
cha mrahaba kutoka  asilimia 3 kwenda asilimia 4.
 
Pia wizara hiyo ilitajwa kupoteza Sh bilioni 1.6  ambazo ni maduhuli ambayo
hayakukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali kama vitalu vya madini na leseni za umeme.
 
Kwa upande wa wizara ya miundombinu inashutumiwa kutumia Sh bilioni 252.9 ambazo
zilitengwa kwenye bajeti ya wizara hiyo kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika mwaka
wa fedha 2011/2012 zilitumika kulipa  madeni ya wizara ya mwaka 2010/11 jambo ambalo
liliathiri utekelezaji wa miradi ya barabara.
 
CAG alisema dhamana za jumla ya Sh bilioni 578.4 zilikuwa zimeisha muda wake na
hivyo kuifanya serikali kama mdhamini kuwajibika kulipa deni hilo.
 
Mashirika ya Umma 
Kwa upande wa mashirika ya umma ambako ukaguzi ulifanyika kwa mashirika 126 kati ya
176, mapungufu yaliyojitokeza ni tatizo la ujangili ambalo linaelezwa kuwa vitendo
vya uwindaji haramu vimeongezeka na taarifa za mbuga saba jumla ya tembo 110
waliuawa katika kipindi cha mwaka 2011/12.
 
“Hii ina athari kubwa kwa taifa na serikali isipochukua hatua baada ya miaka
michache ijayo hakutakuwa na mnyama anayeitwa tembo katika hifadhi zetu,” alisema
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Utouh.
 
Utouh pia alishangazwa na mamlaka ya bandari kuzuia kontena mbili za vitabu vya
shule vilivyotolewa kama msaada kutokana tu na bodi ya huduma ya maktaba (TLSB)
kushindwa kulipa ushuru wa Sh milioni 147 tangu mwaka 2009.
 
Alisema kwa sasa deni halisi la kugombo vitambu hivyo ambavyo vilitolewa kama msaada
na Shirika la Kimataifa la kufadhili Watoto halijulikani kwani inasadikiwa kuwa
gharama  hizo zitakuwa zimeongezeka. “Vitabu hivi vinaenda kusaidai watoto wetu na
hata wafadhili wakisikia msaada walioutoa umekwama bandarini watashindwa kushiriki
wakati mwingine.”
 
CAG pia alibainisha malipo yasiyo ya faida ya Sh bilioni 2.2 yaliyolipwa kwa
mkandarasi baada ya kusitishwa kwa mkataba na mamlaka ya bandari (TPA) kama faini
kwa mkandarasi kampuni ya Oceana Advanced Industries Ltd kutokana na kushindwa
kumkabidhi mkandarasi eneo husika la kazi.
 
Kwa upande wa Shirika la Utangazaji (TBC), Utouh alisema mwaka 2010 TBC ililipa Sh
milioni 618.3 kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania (TCRA)
kwa niba ya Star Times (SMT)kwa ajili ya leseni ya biashara.
 
Alisema lakini ukaguzi ulibaini kwamba kampuni hiyo ina mkataba wa utendaji
uliosainiwa na kituo cha uwekezaji cha Tanzania (TIC) ambapo SMT imepewa msamaha wa
kulipa leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka 10.
 
CAG kwa mtazamo wake alisema kiasi hicho cha fedha kilicholipwa na TBC kingeweza
kuwa ni sehemu ya hisa za shirika kwa SMT kama kusingekuwa na msamaha wa leseni ya
biashara. “Malipo haya yaliyolipwa kimakosa na TBC hayajerejeshwa na TCRA.” 
 
Pia alisema baadhi ya wizara zinaingilia bodi za maishirika na akatoa mfano kuwa
wizara ya maliasili na utalii ilihamisha Sh milioni 771.2 kwenda bodi ya utalii kw
ashughuli ambazo sio za bodi ya utalii. Alisema fedha hizo zilichukuliwa kwa
maelekezo na maagizo kutoka wizarani.
 
Pia CAG amemtaja mkurugenzi mkuu wa Tanesco alitumia vibaya madaraka yake kwa kuipa
zabuni kampuni ya McDonald Live Line Technologh Ltd ya kutengeneza njia za umeme
hai, mikataba iliyosainiwa kwa nyakati tofauti mwaka 2008 hadi 2011.
 
 Alisema ilikuwa ni kinyume na kanuni za maadii za Tanesco na kanuni za maadili za
viongozi kwa mkurugenzi wa Tanesco kuipa mikataba ya kazi kampuni hiyo ambayo yeye
ni mdau.  Kiasi cha Sh bilioni 1.12 zililipwa kwa kampuni hiyo, malipo hayo ni
pamoja na kodi ya ongezeko la thamani ambazo ni Sh milioni 168.9 ambazo
hazikuwasilishwa TRA.
ends

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: CAG AANIKA UKWELI KUHUSU PSPF ASEMA HATARINI KUFILISIKA
CAG AANIKA UKWELI KUHUSU PSPF ASEMA HATARINI KUFILISIKA
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2013/04/cag-aanika-ukweli-kuhusu-pspf-asema.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2013/04/cag-aanika-ukweli-kuhusu-pspf-asema.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy