LEO Watanzania wa Bara na Visiwani wanaadhimisha miaka 49 ya Muungano Mtukufu wa pande hizo mbili ulioasisiwa na viongozi wa kwanza, Mwalimu...
LEO Watanzania wa Bara na Visiwani wanaadhimisha miaka 49 ya Muungano Mtukufu wa pande hizo mbili ulioasisiwa na viongozi wa kwanza, Mwalimu Julius Nyerere na Shehe Abeid Amaan Karume siku kama ya leo mwaka 1964.
Kuungana kwa Zanzibar na Tanganyika mwaka huo, kulikuwa na maana na umuhimu wake na hasa kwa kuzingatia historia ya pande hizo mbili, kwamba watu wao wana udugu wa asili lakini pia ukaribu baina ya nchi hizo ulizingatiwa.
Wakati pande hizi zinakubaliana kuungana, viongozi hao wahusika hawakuwa na uchu wa madaraka na hivyo kukubaliana kwamba Mwalimu Nyerere ndiye awe Rais wa Tanzania mpya huku Shehe Karume akiwa Makamu wake.
Makubaliano hayo yalionesha jinsi walivyoamini katika udugu wa damu moja na kubwa zaidi likiwa ni la kushikamana na kushirikiana kuongoza Watanzania katika kujiletea maendeleo yao kwa kuanza mapambano dhidi ya ujinga, umasikini, maradhi, chuki na hofu.
Miaka 49 ni mingi na kama ni kwa binadamu basi ni ya mtu mzima ambaye anaelekea uzeeni hivyo kuaminika kuwa na busara katika mambo yake, na ndivyo pia Watanzania tunavyopasa kuuenzi Muungano huu na kuulinda kwa gharama zote huku tukikumbuka na kuzingatia ukweli kuwa ‘Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu’.
Kwa kuwa kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Amani, Utulivu na Maendeleo ni matokeo ya Muungano wetu, Tuuenzi na Kuulinda’, hatuna budi kweli kuuenzi na kuulinda kwani ndio umesababisha amani, utulivu na maendeleo kutamalaki nchini.
Wapo watu ambao kwa sababu zao wanaamini kwamba Muungano haufai na unastahili kuvunjika, hayo ni mawazo yao, lakini pia wana sababu zao ambazo bila shaka haziungwi mkono na idadi kubwa ya Watanzania ambao wameshuhudia faida za kuwa na Muungano huo.
Wanaotaka uvunjike kila mara hukosa hoja za kuhalalisha azma yao hiyo na matokeo yake hujikuta wakitaja kero za Muungano ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi kila siku na kupungua moja baada ya nyingine na hivyo kukosa sababu nzito ya kuhalalisha wazo la kuvunjika kwa Muungano.
Kero zilizopo za Muungano ni kama vijipu vidogo mwilini ambavyo vinaweza kutumbuliwa na kupona na kisha mwili kurejea katika hali yake na kurejewa na siha ya kawaida na mwenye vijipu hivyo akaendelea kufanya kazi za uzalishaji bila tatizo.
Sisi tunawaomba wanaodhani kero za Muungano zinaweza kumalizika kwa kuuvunja, waachane na fikra hizo na badala yake wachangie katika kuuimarisha, ili kujihakikishia amani zaidi, utulivu zaidi na maendeleo zaidi.
Kuvunja Muungano ni njia ya kutaka kuwagawa Watanzania ili Bara iwe Bara na watu wake na halikadhalika Zanzibar iwe Zanzibar na watu wake, na kama hilo litafanyika, basi siku moja Unguja itakuwa Unguja na watu wake na Pemba itakuwa Pemba na watu wake na bila shaka visiwani kutadhoofika.
Kama alivyopata kusema Mwalimu Nyerere, Wazanzibari wanajiita sisi Wazanzibari kwa sababu ya kuwapo Muungano na halikadhalika wa Bara wanajiita hivyo kwa sababu ya kuwapo Muungano huo, hivyo kuna faida kubwa kwa kuwa na Muungano kuliko itakavyokuwa kama utavunjika.
Watanzania tuadhimishe miaka hiyo 49 ya Muungano tukiwa na mshikamano mkubwa ambao utawatisha maadui zetu ambao wanajaribu kuupekenyua, ili hatimaye tukidanganyika, wakae pembeni wakitucheka na kutuuliza kiko wapi! Tusikubali.
source habarileo

COMMENTS