TUZO za muziki wa Kilimanjaro zinatarajiwa kufanyika Juni 8, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Milimani City Dar es Salaam, huku wasanii Ommy Dimp...
TUZO za muziki wa Kilimanjaro zinatarajiwa kufanyika Juni 8, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Milimani City Dar es Salaam, huku wasanii Ommy Dimpoz na Mwasiti, wakiteuliwa kuwania tuzo nyingi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Meneja wa Bia ya Kilimanjaro inayotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), George Kavishe, mashabiki wa muziki nchini wataanza kupiga kura kuchagua wasanii wanaotaka washinde kwenye vipengele mbalimbali kuanzia Mei 2, mwaka huu.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa jana, na waandaaji wa tuzo hizo, bia ya Kilimanjaro kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), mwaka huu vipengele vinavyoshindaniwa vimeongezeka kutoka 22 mpaka 35, na pia kutakuwa na tuzo mbili za heshima.
Katika orodha hiyo, msanii Ommy Dimpoz anaongoza kwa kuchaguliwa kuwania tuzo nyingi, anawania tuzo nane.
Dimpoz anawania tuzo kwenye vipengele vya Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka, ambako wimbo wake wa Me & U, utashindania tuzo hiyo pamoja na Dear God wa Kala Jeremiah, Lekadutigite wa Kigoma All Star, Mapito wa Mwasiti aliyeshirikiana na Ally Nipishe na Pete wa Ben Pol.
Msanii huyo pia anawania Tuzo ya Msanii Bora wa Bongo Flava kwa wanaume, akishindanishwa na Ally Kiba, Ben Pol, Diamond, na Linex.
Yupo pia kwenye kuwania Tuzo ya Video Bora ya Wimbo wa Mwaka ambapo wimbo wake wa Baadae unawania tuzo hiyo pamoja na wimbo wa Kamili gado wa Profesa J alioshirikiana na Marco Chali, Marry me wa Rich Mavoko, Nichum wa Bob Junior, na Party Zone wa AY alioshirikiana na Marco Chali.
Dimpoz pia yupo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mashairi, akipambana na Ally Kiba, Barnaba, Ben Pol na Linex. Nyimbo zake za Baadae na Me & U pia zinawania Tuzo ya Wimbo Bora wa Bongo Pop.
Katika tuzo hiyo, pia zipo nyimbo za Aifola wa Linex alioshirikiana na Fundi Samweli, Chuki ni Bure wa marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ alioshirikiana na Dully Sykes na Marry me wa Rich Mavoko.
Me & U pia upo kwenye kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana, ikishindania tuzo hiyo pamoja na Chuki ni Bure, Mapito wa Mwasiti alioshirikiana na Nipishe, Sihitaji marafiki wa Fid Q na Vyonne, na Single boy wa Kiba aliomshirikisha Lady Jaydee.
Msanii mwingine kwa kizazi kipya kwa upande wa wanaume anayemfuatia Dimpoz kwa kuwania tuzo nyingi ni Ben Pol ambaye mwaka jana alipata Tuzo ya Mwanamuziki Bora na Wimbo Bora wa R&B. Mwaka huu, ameteuliwa kuwania tuzo tano.
Kwa wanawake kwenye Bongo Flava, Mwasiti anawania tuzo tano, ambazo ni Mwanamuziki Bora wa Kike anayewania na Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee na Recho.
Pia yumo kwenye kuwania Tuzo ya Wimbo Bora wa mwaka, ambapo wimbo wake wa Mapito umechomoza. Aidha, anawania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Bongo Flava, Wimbo Bora wa Kushirikiana na Wimbo Bora wa Zouk Rhumba.
Wasanii wengine wa kike kwenye tuzo hizo ni Linah, ambaye mwaka jana alitamba na wimbo wake wa Angalau, Recho aliyetamba na Nashukuru umerudi na Upepo, Shaa aliyetamba na Siri ya Penzi.
Kwa upande wa msanii anayechipukia, tuzo hiyo inawaniwa na Nipishe ambaye aliibuka katika wimbo wa Mapito alioshirikishwa na Mwasit. Kwa sasa, Nipishe anatamba na wimbo wake wa My.
Msanii mwingine anayewania tuzo hiyo ni Angel, Bonge la Nyau, Mirror na Vanessa Mdee ambaye naye alianza kusikika kwenye wimbo wa Me & U alioshirikishwa na Dimpoz. Kwa sasa, anatamba na Closer.
Kwa upande wa taarab, kutakuwa na Tuzo ya Msanii Bora wa Kike ambayo inawaniwa na Mashauzi, Khadija Kopa, Khadija Yusuph na Leila Rashid. Kwa upande wa wasanii wa kiume, tuzo hiyo inawaniwa na Ahmed Mgeni, Hashim Said na Mzee Yusuph.
Tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab inawaniwa na Kopa kupitia wimbo wake wa Mjini Chuo Kikuu, Jahazi (Mzee Yusuph) na wimbo wake wa Mpenzi Chocolate, Leila na wimbo wake wa Sina Muda huo, Mashauzi na wimbo wake wa Si Bure una mapungufu na Siwasujudii viwavijeshi.
Tuzo ya Bendi Bora ya Mwaka inashindaniwa na African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mapacha Watatu, Mashujaa, Mlimani Park na Msondo Ngoma. Kwa Wimbo Bora wa Afrika Mashariki, zipo nyimbo za Fresh All Day wa Camp Mulla, Make you dance (Keko akimshirikisha Madtrax), Maswali ya polisi (DNA), Still a Liar (Wahu), Valu Valu (Jose Chameleone).
source Habarileo

COMMENTS