hotuba ya jk kwenye warsha ya mfumo mpya wa ufuatiliaji wa vipaumbele

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA WARSHA YA WAZI (OPEN DAY) KUH...




HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA WARSHA YA WAZI (OPEN DAY) KUHUSU MFUMO MPYA WA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KITAIFA YA KIPAUMBELE, VIWANJA VYA MAKUMBUSHO YA TAIFA, DAR ES SALAAM, MEI 24, 2013

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Seif Shariff Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri;
Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi;
Makatibu Wakuu;
Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango;
Washirika na Wadau wa Maendeleo;
Viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma;
Viongozi wa Kidini na Sekta Binafsi;
Wataalamu Elekezi kutoka PEMANDU na Mckinsey;
Washiriki wa Maabara;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana:
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote katika Warsha ya Wazi kuhusu mfumo mpya unaoanzishwa na Serikali wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kitaifa ya kipaumbele.  Warsha hii inatoa nafasi ya pekee kwa wananchi kushiriki na kutoa mawazo yao jinsi ya kuboresha mfumo huo unaopendekezwa.  Ni Warsha ya kuelimishana, kubadilishana mawazo na kufahamishana mipango na mambo ambayo Serikali inatarajia kuyafanya katika siku za karibuni. 
Namshukuru Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, viongozi na watumishi wote wa Tume ya Mipango kwa kuandaa Warsha hii mahsusi.  Kwa namna ya pekee nawashukuru pia wataalamu wa PEMANDU na McKinsey kwa kushirikiana vizuri na wataalam wetu katika kila hatua ya safari hii ambayo Serikali yetu imeianza.
Ndugu Wananchi;
        Kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo sio jambo geni hapa nchini.  Ni jambo ambalo tumelifanya tangu tupate Uhuru na tunaendelea nalo.  Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilianza na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo mwaka 1961 – 1964.  Mpango huo uliainisha maadui watatu wa maendeleo ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.  Mikakati mbalimbali na mipango madhubuti ya maendeleo ilibuniwa ili kupambana na maadui hao.  Baada ya hapo ukaja Mpango wa Maendeleo wa Miaka 15 wa mwaka 1964 – 1980, uliokuwa umegawanywa katika vipindi vitatu vya utekelezaji vya miaka mitano mitano.
Baadhi yenu mtakumbuka kuwa utekelezaji wa vipindi viwili vya mwanzo ulikuwa wa kuridhisha.  Hata hivyo, utekelezaji wa kipindi cha mwisho cha Mpango ule, yaani kati ya mwaka 1975 – 1980, ulikuwa duni mno.  Utekelezaji wake ulivurugwa sana na changamoto za wakati ule kama vile kupanda sana bei ya mafuta, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (1977) na Vita ya Kagera.  Mambo haya yalisababisha fedha zetu nyingi kutumika kuagiza mafuta, kujenga taasisi zetu wenyewe na kutetea mipaka ya nchi yetu.  Rasilimali kidogo tuliyonayo ikaenda huko badala ya kugharamia miradi ya maendeleo.    
Ndugu Wananchi;
            Pamoja na changamoto zilizojitokeza, Serikali iliamua kuanzisha mpango mwingine wa maendeleo wa muda mrefu wa mwaka 1981 – 2000.  Kwa bahati mbaya mpango huo nao haukutekelezwa kufuatia kuendelea kudorora kwa uchumi.  Kati ya mwaka 1981 na miaka ya 90 mwanzoni, Serikali ilianza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi.  Tukawa na National Economic Survival Programme (NESP) mwaka 1981 – 82 na Structural Adjustment Programme (SAP) mwaka 1982 – 1985.  Mipango hiyo haikutekelezwa vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa rasilimali za kutosha.  Kati ya mwaka 1986 – 89, Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ikaanza kutekeleza programu ya kwanza ya kufufua uchumi (ERP – I).  Ya pili ikafuatia kati ya mwaka 1989 – 1992.
            Mwaka 1994 Serikali ikaanza kuandaa mpango wa maendeleo wa muda mrefu utaowezesha kuzikabili changamoto mpya kufuatia mageuzi ya kiuchumi na kijamii yaliyokuwa yanaendelea nchini na duniani kwa ujumla.  Kazi hiyo ilikamilika mwaka 1999 na kuzinduliwa kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.  Malengo ya Dira hiyo ni kuleta maendeleo ya haraka nchini na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.  Maana yake ni kwamba wananchi wawe na chakula cha kutosha, huduma ya elimu na afya iliyo bora iwafikie watu wengi zaidi, vifo vya watoto na akina mama vipungue, wastani wa kuishi uongezeke, maji safi na salama yapatikane kwa wote, uhalifu upungue na umaskini uliokithiri usiwepo kabisa na pato la wastani la Watanzania liwe zaidi ya dola za Kimarekani 3,000.  Vile vile pawe na maendeleo ya viwanda, matumizi ya teknolojia na sayansi yaongezeke, miundombinu ipanuke na uchumi ukue kwa asilimia 8 au zaidi. 


Ndugu Wananchi;
Juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali za awamu zote ikiwemo na hii ninayoiongoza mimi zimeleta mafanikio ya kutia moyo.  Kwa mfano, uchumi wa nchi umekua kwa wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi iliyopita, mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 10, mapato ya ndani yameongezeka, mauzo ya nje yameongezeka na hifadhi ya fedha za kigeni imeongezeka pia.  Hata hivyo, idadi ya Watanzania walio maskini bado ni kubwa hususan umaskini wa kipato.  Vile vile bado hatujafanikiwa kufikia malengo katika maeneo mengi tuliyojiwekea.  Hata tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2025 tuliyofanya mwaka 2000 imethibitisha hivyo.  Hatuendi kwa kasi inayotakiwa na utekelezaji wake siyo wa kuridhisha.  Matokeo yake tupo nyuma ya hatua tuliyotakiwa kuwa.  Kwa mfano, kwa upande wa safari ya kuelekea pato la wastani la watu kuwa dola 3,000 mwaka 2025, tulitakuwa tuwe tumefikia dola 995 mwaka 2010.   Lakini ilikuwa tumefikia dola 545 tu.  Kwa ukuaji wa uchumi, tulitakiwa tuwe asilimia 8, lakini tulikuwa asilimia 7. 
Zipo changamoto nyingi za ndani na nje, zilizofanya tusifikie malengo hayo:  Kubwa ni misukosuko ya uchumi wa dunia, uhaba wa rasilimali fedha na ufuatiliaji mdogo katika utekelezaji wa miradi iliyoainishwa kuleta maendeleo. Aidha, mipango na mikakati ya maendeleo ilikuwa na vipaumbele vingi kwa wakati mmoja wakati rasilimali za utekelezaji wake ni kidogo.  Hali hii haikutuwezesha kujielekeza ipasavyo kwenye maeneo yenye kuleta matokeo makubwa na kwa haraka.
Ndugu Wananchi;
Baada ya kutafakari yote haya, tukafikiria namna ya kuweza kufikia malengo yetu ya Dira ndani ya muda uliobakia. Hivyo, tukaamua kuja na Mpango ya Maendeleo wa Muda Mrefu wa Miaka 15 ambao utatekelezwa katika awamu tatu za miaka mitano mitano. Katika Mpango wa Kwanza Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16), maeneo yaliyopewa kipaumbele ni Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Huduma za jamii na Uendelezaji Rasilimali Watu na Utalii, Biashara na Huduma za Fedha.  Changamoto kubwa ikabaki kuimarisha mfumo wetu wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ili kuleta matokeo ya haraka.  Kuendelea kufanya vilevile tulivyokuwa tukifanya  kusingeweza kuleta mabadiliko tuliyokuwa tunayataka katika utekelezaji wa mipango yetu.  Ilibidi tubadilike, ikiwezekana tukimbie pale ambapo wengine wanatembea. 
Ndugu Wananchi;
            Tukiwa katika hali hiyo ya kutafakari cha kufanya, mwezi Mei, 2011 ikawa bahati mimi kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa “Langkawi  International Dialogue” uliofanyika mjini Kuala Lumpur, Malaysia.  Katika mkutano huo, Serikali ya Malaysia iliwasilisha mada jinsi inavyoendesha na kusimamia utendaji wake ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma kwa jamii.  Mimi na viongozi wenzangu tuliohudhuria mkutano huo tulivutiwa sana na mfumo wa utendaji wa Malaysia na tukadhamiria kujifunza zaidi kutoka kwao.  Tukaomba watusaidie.  Bahati nzuri Serikali ya Malaysia ikakubali ombi letu na kuandaa warsha maalum mwezi Novemba, 2011.  Ujumbe wa Tanzania kwenye warsha hiyo ya aina yake uliongozwa na Dkt. Philip Mpango.  Waliporudi, tukaamua kuwa na sisi tuanze kutumia utaratibu wa Malaysia wa “Matokeo Makubwa Sasa” ama kwa Kiingereza “Big Results Now”.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mfumo wa “Big Results Now” hapa nchini ulianza kwa kuainisha maeneo sita yenye uwezo wa kutupatia matokeo makubwa kwa haraka. Maeneo hayo ni nishati, elimu, maji, miundombinu, kilimo na utafutaji fedha.  Kazi ya kuchagua maeneo sita ya kwanza nayo haikuwa rahisi.  Tulibishana sana katika kuchagua vipaumbele vichache lakini vyenye kuleta matokeo makubwa.  Hatimaye tukafanikiwa.  Vipaumbele hivi vinabeba msingi wa kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa Tanzania kwa ujumla na kuchochea ustawi wa maisha bora kwa wananchi. 
Hatua ya pili ikawa ni kufanya uchambuzi wa kina kupitia awamu ya kwanza ya maabara (lab) kama alivyoeleza Katibu Mkuu Kiongozi. Kazi hiyo ilitekelezwa kwa wiki sita mfululizo na wataalam wetu zaidi ya 300 kutoka nyanja na sekta mbalimbali na kukamilika tarehe 05 Aprili, 2013. Nawapongeza sana kwa kazi hiyo kubwa na moyo wao wa kujitolea. Tumeandaa ratiba ya utekelezaji kwa kila mradi na programu ikionyesha kazi zilizopangwa kufanywa, mtekelezaji-husika na muda na kukamilisha kazi.   
Katika mfumo huu, Mawaziri na Watendaji katika Wizara na Idara watapimwa kwa vigezo vilivyo wazi na ninyi wananchi mtapata fursa ya kuvijua vigezo hivi pamoja na matokeo ya upimaji.  Hapatakuwa na siri. Hii itarahisisha usimamizi wa utendaji kwa maana Waziri au Katibu Mkuu atajifunga yeye mwenyewe kimaandishi na ataweka saini yake kwenye vigezo ambavyo atapimwa navyo na wananchi mtashuhudia matokeo ya upimaji huo.
Ndugu Wananchi;
Ili kuweza kuratibu vyema shughuli za ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mfumo huu mpya, nimeunda chombo maalum kitakachokuwa chini ya Ofisi yangu ambacho kitajulikana kama President’s Delivery Bureau (PDB). Kazi zake za msingi zitakuwa ni pamoja na: kupanga na kuendesha shughuli za uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs); kuandaa mikataba ya kupima utendaji kazi wa Mawaziri kwenye miradi na programu za maendeleo katika wizara zao; kwa kushirikiana na Tume ya Mipango kuishauri Serikali kuhusu maeneo machache ya kipaumbele yenye kuleta matokeo ya haraka (National Key Results Areas); kusaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye maeneo hayo; na kufanya tathmini huru ya utendaji kwa viongozi wote hususan Mawaziri katika utekelezaji wa maeneo muhimu ya kitaifa.
Ndugu Wananchi;
Tumefanya kazi kubwa sana ya kuandaa na kuainisha maeneo ya kimkakati na kuyaandalia programu za kina kwa ajili ya utekelezaji. Lakini tumeona ni vyema kuwashirikisha wadau na wananchi katika jambo hili kubwa.  Ndio maana tupo hapa kuhakikisha kuwa wananchi kwa ujumla wenu mnapata fursa ya kuchangia katika miradi na programu hizo kwa maendeleo ya taifa letu na watu wake.
Ndugu Zangu;
Sitapenda kuongea sana hivyo basi nataka niwape nafasi wananchi na wadau wengine mliofika hapa kupita katika eneo la kila maabara na kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam.  Muwe huru kuuliza maswali, kujenga hoja, kutoa maoni na kukosoa na kuboresha katika kila maabara. Baada ya kupata maoni yenu ndipo tutaboresha na kwenda kuyafanyia kazi maoni na ushauri wenu.  
Ndugu Wananchi;
Baada ya kusema hayo, napenda kutamka kuwa Warsha ya Wazi imefunguliwa rasmi.  Ninawatakia majadiliano mazuri na uchangiaji mzuri.
Asanteni kwa kunisikiliza



COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7050,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,738,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: hotuba ya jk kwenye warsha ya mfumo mpya wa ufuatiliaji wa vipaumbele
hotuba ya jk kwenye warsha ya mfumo mpya wa ufuatiliaji wa vipaumbele
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpbxXW67cqakovOzzdckp15JLvtHcKxa8E9WNsh681FS4-Ek1iZoI-LMMwFGgrsmkvUunjU52ko8HbGJPEt5Xo-rCYVwb2Kbrr-30G5DqvkLJc_BnwfQbodM3MfG9bEIwIu3Lyo2QUYhL9/s320/JK+9.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpbxXW67cqakovOzzdckp15JLvtHcKxa8E9WNsh681FS4-Ek1iZoI-LMMwFGgrsmkvUunjU52ko8HbGJPEt5Xo-rCYVwb2Kbrr-30G5DqvkLJc_BnwfQbodM3MfG9bEIwIu3Lyo2QUYhL9/s72-c/JK+9.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2013/05/hotuba-ya-jk-kwenye-warsha-ya-mfumo.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2013/05/hotuba-ya-jk-kwenye-warsha-ya-mfumo.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy