HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA,

Akihutubia kwenye uzinduzi 1 HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI W...

Akihutubia kwenye uzinduzi

1
HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI
JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE
VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE,
DAR ES SALAAM.
 Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano,
 Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
 Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,
 Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,
 Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
 Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar,
 Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,
 Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
 Viongozi wa Vyama vya Siasa,
 Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
 Ndugu Wananchi,
 Wageni Waalikuwa
 Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.
1.0. UTANGULIZI
Ndugu Wananchi,
Page 2
2
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya
leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa
hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa
mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa
Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa
miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo
ilikuwa Mei 2, 2012.
Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo
Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano
kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga.
Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao
1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa
mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya
wananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano
ya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume,
Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala
mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.
Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika
jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini,
wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika. Makundi zaidi ya
160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya viongozi wa juu
wa Serikali walioko madarakani na waliostaafu. Kwa jumla viongozi 43walitoa
maoni.
Page 3
3
Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni ya
wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni tuliyopata
yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, tulitambua
umuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchi
yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana. Aidha,
baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji. Tulifanya
uchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo tumeikamilisha na rasimu
imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya kuizindua, ambapo Wananchi
watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya Tume, napenda kutaja maeneo
machache tu ambayo tunayapendekeza.
2.0. IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA
Ndugu Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina ibara 152. Tume ilifanya jitihada kubwa sana kuandaa
rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu ya
Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.
3.0. MISINGI MIKUU YA TAIFA
Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni
Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na
inastahili kubaki kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza
misingi mingine mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tume
imependekeza Katiba iwe na Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki,
Udugu, Usawa, Umoja, Amani na Mshikamano.
4.0. TUNU ZA TAIFA
Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values).
Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume
imependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu,
Page 4
4
Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya
Kiswahili.
5.0. MALENGO YA TAIFA
Tume ilipozunguka nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu malengo ya
taifa. Walitaka Katiba ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto yao ya
Tanzania ya kesho na kesho kutwa. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna sura
nzima inayohusu Malengo mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli za
Kiserikali na Sera za Kitaifa. Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa Malengo ya Kitaifa
yaliyoainishwa ndani ya Rasimu yatakuwa ni Mwongozo kwa Serikali,
Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa, Taasisi na Mamlaka nyingine, na kwa
kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri Masharti ya Katiba au Sheria
nyingine za Nchi.
Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa
mpangilio wa kuonesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni,
kimazingira na sera ya mambo ya nje. Malengo hayo yameingizwa kwenye
Rasimu ya Katiba.
6.0. VYOMBO VYA KIKATIBA
Wananchi walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba na
kuingizwa kwenye Katiba ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wa
majukumu yao. Tume imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vya
Kikatiba; Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, Kamati
Maalum ya Makatibu Wakuu na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na
Usalama la Taifa, Tume Huru ya Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume
ya Utumishi wa Umma, Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora
Page 5
5
7.0. MAADILI YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI
Wananchi wengi pia walizungumzia kwa upana sana kuhusu maadili na miiko ya
Viongozi, kwa kuzingatia maoni ya wananchi Tume inapendekeza maadili ya
viongozi wa umma, pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba.
Tume pia imependekeza kuwa Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume
yenye mamlaka makubwa ya kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja
miiko ya uongozi.
8.0. HAKI ZA BINADAMU
Kuhusu haki za binadamu wananchi walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe na
vikwazo visivyo vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko katika baadhi ya haki za
binadamu kwa madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni kuhusu
uhuru wa mwananchi kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwamba
vikwazo vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine
Tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja
na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za
Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na
Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari na
kadhalika.
9.0. URAIA
Wananchi wengi walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba.
Tume imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya Muungano na haki zake.
10.0. MIKOPO NA DENI LA TAIFA
Ndugu Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa
utaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa kuzingatia
Page 6
6
maoni ya Wananchi, Tume imependekeza kuwa, Serikali itawajibika kutoa taarifa
Bungeni kuhusu Mikopo kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba yake na matumizi
ya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.
11.0. MFUMO WA UTAWALA
Kuhusu utawala, Tume inapendekeza Tanzania iendelee na mfumo wa Jamhuri kwa
maana ya nchi inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi wa
Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
12.0. UCHAGUZI WA RAIS
12.1. Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombea
Urais. Baadhi walipendekeza mtu akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia na
sifa ya kugombea Urais. Umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura ni miaka 18.
Wengine walipendekeza umri uliopo kwenye Katiba wa mtu kugombea Urais,
yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea, uendelee kubaki kama ulivyo.
Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea Urais uwe miaka 35 au
miaka 50 na kuendelea.
Tume imeyachambua maoni yote hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za
Nchi zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Marais
katika Nchi mbalimbali Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea wa nafasi
ya Urais kuwa na umri chini ya miaka 40.
Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na umri wa miaka
40 au zaidi.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza Rais
aendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeomba
urais asiwe chini ya miaka 40.
Page 7
7
Uchaguzi wa Rais itakuwa kama ilivyo sasa, yaani mgombea Urais atakuwa na
mgombea mwenza kwa utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tume
imependekeza Mgombea Urais anaweza kupendekezwa na Chama cha
Siasa au kuwa Mgombea Huru.
Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa
amepata kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa
Mahakamani, lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaoweza
kufungua kesi ni wagombea Urais. Aidha, ni Mahakama ya Juu pekee ndiyo
itakuwa na Mamlaka na uwezo wa kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya
uchaguzi wa Rais na shauri lazima liamuliwe ndani ya mwezi mmoja, yaani siku
therathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwa
mshindi au kuthibitishwa na Mahakama.
13.0. MADARAKA YA RAIS
Ndugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa
ngazi za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo
vingine katika uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya
watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo
Bunge litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe
chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya
Page 8
8
majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais
kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.
14.0. KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama
ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
15.0. IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na
tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge
isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.
16.0. BUNGE
Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa
kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu
wenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na
mwingine mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa
Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata
hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa
kipindi chake.
Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi
inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza
Page 9
9
nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa
basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe
Viongozi wa vyama vya Siasa.
17.0. TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume
inapendekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza
sifa za wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa
Tume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa
zilizoainishwa ndani ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na
Kamati ya Uteuzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine
sita ambao ni Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano, Maspika wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu.
Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi
wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa
tume ya uchaguzi.
Inapendekezwa Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi,
kura ya maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.
18.0. MAHAKAMA
Kuhusu Mahakama inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme
Court) Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais
baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
19.0. MUUNDO WA MUUNGANO
Page 10
10
Ndugu Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote.
Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwamba
hadidu za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya
wananchi walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni
hayo. Licha ya kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana,
Tume ilichambua sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.
Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza
Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na muungano wa
mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na uzito, kwa hiyo
Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zao
zilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni changamoto
kubwa kuwa na Muungano wa Serikali Moja
Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchi
wa Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana
wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa lakini
hakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume iliona
kuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitiza
muungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali mbili
walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi hili
walipendekeza mabadiliko mengi na makubwa.
Tathmini ya Tume ilionyesha
kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.
Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi
yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito.
Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huu
zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbali
Page 11
11
za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa
Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
20.0. ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
Ndugu Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano
yawe 7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3. Uraia na Uhamiaji
4. Sarafu na Benki Kuu
5. Mambo ya Nje
6. Usajili wa Vyama vya Siasa
7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo
ya Muungano.
21.0. BENKI KUU
Kwa kuwa Tume imependekeza Muungano wa Shirikisho kutokana na uzito wa maoni
ya wananchi. Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itakayokuwa na wajibu wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigeni
na Benki za Washirika wa Muungano.
Page 12
12
22.0. BENKI ZA SERIKALI ZA WASHIRIKA
Kutokana na pendekezo la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu,
inapendekezwa kuwepo kwa Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya
fedha za Serikali za kila Mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biashara
katika mamlaka zao.
23.0. BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA
23.1. Serikali ya Majimbo
Ndugu Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katika
rasimu hii. Moja ya mambo hayo ni Serikali za Majimbo. Tume ilichambua
maoni na sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tume
ilibaini changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.
Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa
Serikali Tatu, ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeleta
gharama kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo,
Mabaraza ya Mawaziri na Mabunge na gharama yake ingekuwa kubwa.
Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya
Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo na
ukabila. Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha
nchi kwenye utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini
na ukanda na kuzigawa rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuleta
tofauti kubwa ya kimaendeleo katika nchi.
23.2. Mahakama ya Kadhi
Ndugu wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya kadhi. Tume ilipokea maoni mengi kuhusu suala
hili. Baadhi ya wananchi walitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba na
Page 13
13
wengine walipinga. Baada ya kuamua kuwa Muundo wa Muungano uwe wa
Serikali Tatu, Tume iliona kuwa Mahakama ya Kadhi siyo suala la
Muungano na imeliacha ili lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala siyo kuwapo au kutokuwapo kwa
mahakama ya kadhi. Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwa
katika Katiba. Zanzibar kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenye
Katiba ya Zanzibar. Kwa kutumia uzoefu huo hata Tanzania Bara inaweza
kupata ufumbuzi wa suala hili.
23.3. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
Jambo la Tatu ni Kuwepo au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa na
Wilaya. Baadhi ya Wananchi walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo,
wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kuwepo lakini
wachaguliwe na wananchi na waengine wakasema wawepo na waendelee
kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu suala hili na kuamua
kwamba siyo suala la Muungano na kwa kuwa Muundo wa Muungano
imependekezwa uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona suala la uwepo au
kutokuwepo na namna ya upatikanaji wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya
lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
23.4. Serikali za Mitaa
Kuhusu Serikali za Mitaa, Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu
kuziimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili wa
kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hili
na kuamua kwamba siyo jambo la Muungano na hivyo, litashughulikiwa
kwenye Katiba za Washirika wa Muungano.
23.5. Uraia wa Nchi mbili
Ndugu Wananchi,
Page 14
14
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi
mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada
ya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi
yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria
inayohusu jambo husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi
mbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye
Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo
linaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza
kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
24.0. MWISHO
Naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwa
kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoa
maoni na kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili na
kuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya ambayo
itaakisi ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:
1. Kwa kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima
2. Kwa kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,
3. Kwa kutokuingilia Uhuru wa Tume wakati wa Utekelezaji wa Majukumu
yake na
4. Kutoa Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini na Waadilifu ambao
wameunda Sekretarieti ya Tume.
Ndugu Wananchi,
Page 15
15
Shukrani za pekee ziwaendee:
1. Wakuu wa Mikoa,
2. Wakuu wa Wilaya,
3. Wakurugenzi / Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4. Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya,
5. Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.
Kwa kuisaidia Tume kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru
Asasi za Kiraia, Taasisi, Jumuiya za Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbali
kwa namna walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni.
Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa Wananchi na
katika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Nachukua nafasi hii kuwaomba Wananchi kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,
Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanyofanana
kushiriki vyema, kwa umakini, utulivu na kwa amani katika hatua hii ya kuipitia,
kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.
Tume imekuwa ikithamini na itandelea kuthamini mawazo na maoni kutoka kwa
Watanzania wote.
Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
www.katiba.go.tz
SASA NAKUOMBA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS UIZINDUE RASMI
RASIMU YA KATIBA
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
TOA MAONI TUPATE KATIBA MPYA

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA,
HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA,
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgv4wuNNn0XC4PBzdBej4rtDBlTxwzPQZ8H3zNiW4w4bOzyBmVG_qG05cCB0F9MHyMnLoMQO2zKJDkxXJdJZq2vZSo1LQDWtGPCn9GUC2pAiwfOBys-kvdyiWWKTu2bXjZSSQd_eZhSUdg/s320/FSA_5532.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgv4wuNNn0XC4PBzdBej4rtDBlTxwzPQZ8H3zNiW4w4bOzyBmVG_qG05cCB0F9MHyMnLoMQO2zKJDkxXJdJZq2vZSo1LQDWtGPCn9GUC2pAiwfOBys-kvdyiWWKTu2bXjZSSQd_eZhSUdg/s72-c/FSA_5532.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2013/06/hotuba-ya-mwenyekiti-wa-tume-ya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2013/06/hotuba-ya-mwenyekiti-wa-tume-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy