THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-ma...
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amesisitiza kuwa pamoja na kweli kuwa gesi asilia imegundulika
mkani Mtwara lakini gesi hiyo siyo mali ya wana-Mtwara bali ni
raslimali ya Watanzania wote ambao wataitumia kwa manufaa ya nchi
nzima.

Hata
hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Mtwara wanayo haki ya kunufaika na
gesi hiyo asilia kama walivyo Watanzania wengine
katika sehemu zote za nchi.
katika sehemu zote za nchi.
Rais Kikwete
ameyasema hayo usiku wa Jumapili, Juni 2, 2013,
wakati alipokutana na kuzungumza na Jumuia ya Watanzania wanaoishi
katika Japan kwenye Hoteli ya Royal Park Yokohama mjini Yokohama.

Rais
Kikwete alikuwa katika ziara ya wiki moja nchini Japan ambako
alihudhuria Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya
Afrika – TICAD V (Tokyo International Conference on African
Development).

Akizungumza
na Watanzania hao, Rais Kikwete amesisitiza kuwa raslimali yoyote
inayogundulika katika sehemu yoyote ya Tanzania ni mali ya
Watanzania wote na lazima itumike kuwanufaisha wote na siyo wale
ambako raslimali hiyo imepatikana.

Katika
risala yao, Watanzania walikuwa wameeleza kutofurahishwa kwao
na ghasia na fujo ambazo zimekuwa zinafanywa Mtwara na baadhi ya watu
wanaojiita wakazi wa Mkoa huo wakidai kuwa gesi asilia hiyo ni lazima
itumike kuwanufaisha wananchi na Mtwara badala ya kuisafirisha kwenda
Dar Es Salaam kuzalisha umeme kwa ajili ya nchi nzima.

amesisitiza kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa raslimali ya nchi
inaweza kuzuiliwa isitoke katika eneo ambako inapatikana kwa vile
hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu jambo la namna hiyo.

“Hiyo
nchi haipo duniani na wala sera za namna hiyo haziwezi kuanzia
Mtwara. Sijui hii dhana wamepata wapi. Nadhani wanavurugwa na
wanasiasa ambao wanajitafutia umaarufu. Mafuta ya Texas pale Marekani
ni ya Wamarekani wote siyo ya watu wa Texas. Mafuta ya North Sea pale
Uingereza ni ya Uingereza yote,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Pato
letu la taifa linachangiwa na kila raslimali yetu – migebuka ya
Kigoma inachangia, sato wa Mwanza wanachangia, almasi ya Mwadui,
dhahabu, pamba na kahawa vyote kwa pamoja vinachangia pato letu la
taifa ambalo tunaligawana kwa maendeleo ya kila mmoja wetu. Kule Mtwara
kuna mengi yamefanyika kwa nini mbona wana-Mtwara hawajiulizi pesa ya
kuyafanya hayo ilitoka wapi? Mbona hawadai kuwa hata korosho isitoke
Mtwara?”

amekumbusha kuwa siyo mafuta yote yatakayosafirishwa nje ya Mtwara. “Kama
nilivyosema ni asilimia 14 tu ya mafuta ambayo
itasafirishwa nje ya Mtwara. Asilimia kubwa itabakia Mtwara. Kuna
viwanda vingi kiasi cha 47 vitajengwa Mtwara vingi kuliko vilivyo
katika eneo lolote la nchi yetu. Linalosubiriwa ni kukamilika kwa
upimaji mkubwa wa Mji wa Mtwara na maeneo ya jirani.”

Amesema
kuwa ni jambo la kushangaza kuwa wana-Mtwara wanadai kuwa gesi asilia isitoke
Mtwara. “Sasa gesi isipokwenda sokoni wana-Mtwara
watanufaika vipi? Gesi asilia hii ni lazima iuzwe ili fedha ziweze
kupatikana na kuwanufaisha wana-Mtwara na Watanzania wengine.”

Kikwete amesema ni jambo la kushangaza vile vile kuwa watu
wanaandamana leo kuhusiana na mapato ya gesi. “Mapato ya gesi hii
hayataanza kuonekana kati ya miaka sita hadi 10 kuanzia sasa, sasa
tunatoana macho ya nini wakati uwekezaji ndio kwanza umeanza?”

Kikwete ambaye aliandamana na mawaziri kwenye mkutano huo na
Watanzania aliwataka mawaziri hao mmoja mmoja kuelezea maswali na
maoni ya Watanzania hao kuhusu maeneo yao.

Mawaziri
hao ni Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Harrison Mwakyembe, Waziri wa Nishati na
Madini Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Kazi na Ajira
Mheshimiwa Gaudensia Kabaka.
Rais
Kikwete ameondoka Japan asubuhi ya Jana kwenda Singapore ambako atafanya ziara
rasmi ya siku mbili ya Kiserikali kwa mwaliko wa
Serikali ya nchi hiyo.
Serikali ya nchi hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES
SALAAM.
5 Juni, 2013
COMMENTS