Labda nianze na hili la jumla hivi kuna sheria Zanzibar inayotokana na sera ya matumizi ya fukwe ? kama ipo inasemaje? Inampa haki na...
Labda nianze na hili la jumla hivi kuna sheria Zanzibar inayotokana na sera ya matumizi ya
fukwe ? kama ipo inasemaje? Inampa haki nani? yaani naulizia Land
Tenure Act. Sasa endelea
Nina
imani kubwa watu weusi waliokuwa katika Bara la Afrika walipopigania UHURU
hawakuwa na ndoto za kuzimu. Walipigania kwa nia ya kumkomboa Mu-Afrika ili
kuwa na uhuru wa kujitawala na kuongoza katika mipaka yao.
Mnamo
mwaka 2011, wananchi wa maeneo ya Mji Mkongwe, Shangani walipeleka malalamiko
yao Serikalini (Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, na Afisi ya Makamo wa Pili
wa Rais) kuhusu kujengwa kwa hoteli hiyo na athari ya wazawa wa maeneo hayo
ambapo sasa imejengwa jengo la hoteli ya kifahari la Park Hayatt.
Kujengwa
kwa hoteli hiyo imeleta mtafaruku kwa wananchi wa Zanzibar na hata katika haiba
nzima ya kisiwa katika mlingo wa kumbukumbu za kale za Umoja wa Mataifa
(UNESCO) na kuisababisha Zanzibar kuyumba kutolewa katika Miji mashuhuri
duniani kwa uhifadhi wa Mji Mkongwe.
Licha
ya kuwa Zanzibar ni maarufu ulimwenguni kwa biashara yake ya usafirishaji wa
Karafuu kwa karne kadhaa, Utalii ni dhana nyingine ambayo imechangia kwa kuipa
Zanzibar hadhi hiyo chini ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa UNESCO.
Wananchi
wa maeneo hayo hivi sasa wakiwemo watoto wamekuwa hawana maeneo ya kuchezea
ambayo yako wazi ikiwa ni haki ya msingi.
Pia
kuondolewa kwa eneo hilo la wazi, kumekuwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira ya
mji ikiwa hakuna eneo lililoainishwa la
kutupa taka za majumbani ambapo hapo awali eneo hilo lilikuwa ni jaa, ambapo
hivi sasa taka za majumbani zimekuwa zikitupwa ovyo vichochoroni, wajenzi
pamoja na walinzi wa eneo hilo wamekuwa wakijisaidia haja ndogo na kubwa kwenye
chochoro za nyumba za karibu na kusababisha harufu mbaya na uchafu kwa nyumba
za jirani.
Pia
wavuvi wa nyumba za karibu kushindwa kuendesha shughuli zao kama hapo awali kwa
kikwazo cha hoteli hiyo kutokana shughuli zao nyingi walikuwa wakiziratibu
hapo.
Hivi
sasa wananchi wa karibu wanapata huduma ya kutumia fukwe ya bahari lakini kuna
uwezekano mkubwa baada ya kukamilika ujenzi na kuanza kazi kwa hoteli hiyo,
wananchi watakosa access ya kutumia fukwe ya hapo karibu. Hili si jambo la
ajabu kwa wananchi wa Zanzibar kunyimwa fursa ya huduma ya kutumia fukwe ya
bahari zilizo kando na mahoteli na wenye Mahoteli hayo. Kanda ya Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Kiwengwa kumekuwa malalamiko na unyanyasaji na udhalilishaji
kwa wananchi wa maeneo hayo kutotumia fukwe hizo.
Muekezaji
huyo wa Park Hayatt hivi sasa amefanikiwa kununua nyumba kadhaa za maeneo hayo ya
Mji Mkongwe ili kuongeza idadi ya matumizi yake.
Kwa
nyakati nyingine, migahawa ambayo inaendeshwa pia na wageni nao pia wamekuwa na
kiburi dhidi ya wenyeji wanaofika eneo hilo kwa huduma. Maegesho ya gari ni
eneo la wote isipokuwa wale wamelipia na kupewa idhini ama kibali na Manispaa
ya Mji kuwa eneo hili ni la mtu Fulani kinyume na hapo maegesho ni haki ya kila
mmoja.
Mgahawa
uliopo pembeni na Korti Kuu ya Zanzibar mtaa wa Vuga, ambao unamilikiwa na
kutoa huduma za jamii ya Ethiopia ukijulikana kwa jina la Abysinian ulimtaka
mwenyeji kuondoa gari lake hapo pembeni ili mwenye mgahawa aweze kuengesha yeye
gari lake. Dada huyo ambaye anaendesha mkahawa huo alidai kuwa eneo hilo ni la
kwake ili hali hakuna alama ya kuonyesha kuwa anamiliki hapo.
Wakati
hali ikiendelea kwa wawekezaji kuwa na kiburi, pia jengo la hoteli lililopo
mkabala na hoteli ya Grand Palace mtaa wa Malindi pembeni na Wizara ya
Biashara, Viwanda na Masoko nalo limekuwa likipora nafasi ya ardhi nje ya
mipaka yake na pia kuendesha shughuli zake wakati wa mchana za kupakua mizigo
na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo ambayo ina waruhusu
watumiaji wengine kufika maeneo yao ya kazi. Hali hiyo imejitokeza hivi
karibuni ambapo Afisa mmoja alishindwa kufika afisini kwake baada ya gari la
kupakua mizigo likiwa limezinga njia. Afisa huyo alipojaribu kuomba kupishwa na
kutoa shauri gari hilo likae pembeni na kuendelea shughuli zake, wasimamizi
walionyesha kupuuza shauri hilo na kuendelea shughuli za upakuzi.
Je unadhani hali hii si tete kisiwani ? Au tuseme tunafikiria nini miaka 20 ijayo? Hususan katika maeneo ya Mji Mkongwe ambapo hivi
sasa kumekuwa na ushamiri wa ujenzi wa mahoteli hasa kwenye fukwe zake? Je fukwe zitabaki mikononi mwa wananchi?Je utalii wa kihistoria utaendelea kuwepo ?Je hadhi ya Mji Mkongwe itaendelea kuwapo?Safari nyingine tutaitazama Ngome Kongwe.
COMMENTS