Usahihishaji mpya sekondari waanza

*Ukadiriaji wanafunzi wakifeli wazikwa rasmi *Mfumo upangaji madaraja nao wabadilishwa   *Utaanza na mtihani wa ‘moko’  kida...



*Ukadiriaji wanafunzi wakifeli wazikwa rasmi
*Mfumo upangaji madaraja nao wabadilishwa  
*Utaanza na mtihani wa ‘moko’  kidato cha nne

USAHIHISHAJI mpya wa mitihani ya Taifa kwa kidato cha nne na sita, unaoendana na utaratibu mpya wa upangaji wa ufaulu na madaraja, unatarajiwa kuanza kutumika katika mtihani wa majaribio wa kidato cha nne mwaka huu nchini kote, na kufuatiwa na mitihani yote ya kidato cha nne na sita.
Akitangaza mabadiliko hayo muhimu jana Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde, alisema tayari maelekezo kuhusu mabadiliko hayo, yameshatolewa kwa wakuu wa shule za sekondari nchini.
Baadhi ya faida ya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Dk Msonde, ni pamoja na kuondoa ukadiriaji wa alama za ufaulu, uliokuwa ukitumiwa awali, kuweka uwazi katika usahihishaji na kumwezesha mwanafunzi kukokotoa ufaulu wake hata kabla ya matokeo na hata mwalimu kukotoa ufaulu wa wanafunzi wake kabla hata ya matokeo.

Kwa mujibu wa Dk Msonde, mwalimu na mwanafunzi wataweza kukokotoa alama za ufaulu, kwa kuwa majibu yanayotumika kusahisha mitihani kila mwaka na namna wanafunzi walivyojibu, yatarejeshwa shuleni, ili mwalimu afahamu hali ya wanafunzi na ufundishaji.

Pili kwa mujibu wa Dk Msonde mabadiliko ya sasa, yatamwezesha mwalimu kufahamu shida ya wanafunzi wake kulingana na taarifa ya ufaulu wa waliopita na kufahamu wapi patumike mbinu gani kuinua ufaulu.


  *Ukadiriaji 
Kwa mujibu wa Dk Msonde, mabadiliko hayo yanaanza katika mfumo wa viwango vya ufaulu, kutoka katika Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Vinavyobadilika, kwenda katika Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Visivyobadilika.
Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Vinavyobadilika, Dk Msonde alisema ulianza kutumia tangu mwaka 1973, wakati Necta ilipoanzishwa mpaka 2011.
Akifafanua kuhusu mfumo huo ulioachwa mwaka 2011 na kuzikwa rasmi kuanzia mwaka huu, Dk Msonde alisema wanafunzi wakifeli sana, Necta ililazimika kukadiria viwango vya ufaulu kuwa vya chini kabla ya kutoa matokeo.
Alisema walikuwa wakiangalia wastani wa ufaulu na kulinganisha na mwaka uliopita, kama ni wa chini  waliangalia waliofaulu sana na waliofeli sana, kisha waliangalia tofauti ya alama ya ufaulu kati ya waliofaulu na baada ya hapo walikuwa wakibadilisha viwango vya ufaulu kuwa vya chini kabla ya kutoa matokeo.
Alitoa mfano, kama mwaka uliopita wastani viwango vya ufaulu wa somo kama Historia ulikuwa 60 na mwaka huo wastani huo ukashuka kuwa 40, ilikuwa ishara ya kwanza kuwa somo husika mwaka huo wamefeli sana.
Kutokana na hali hiyo, alisema kama alama A ilianzia 80 mpaka 100, Necta iliweza kushusha ianzie 70 mpaka 100, ili hata waliopaswa kuwa na alama B, wapande kidogo na hivyo hivyo katika alama zinazofuata.
“Hivyo katika mfumo huu, viwango vya ufaulu hupangwa kwa kutegemea watahiniwa walivyofaulu somo husika, hivyo viwango hivyo vya ufaulu hutofautiana baina ya somo na somo na kati ya mwaka mmoja na mwingine,” alisema Dk Msonde.
Matokeo yake, Dk Msonde alisema viwango vya ufaulu vilikuwa siri na Baraza halikuwahi kueleza popote kuhusu usiri huo na wadau walikuwa na habari za kupotosha kuwa A ilikuwa inaanzia 81 na D ikianzia 21, wakati katika hali halisi kuna wakati viwango hivyo vilishuka.
*Kuzika ukadiriaji
Kuanzia mwaka huu Mfumo wa Viwango vya Ufaulu Visivyobadilika, unaanza kutumika na viwango hivyo ni vipya baada ya kupangwa kwa kuangalia mwenendo wa ufaulu wa miaka 12, kuanzia 1999 hadi 2011.
Dk Msonde alisema katika miaka hiyo 12 ya kuangalia, A ya juu ilikuwa mwaka  1999 na 2011, ambapo ilianzia 70 mpaka 90. Alisema hakuna mwaka A ilishuka chini ya 70. Alama D katika miaka hiyo 12, ilianzia 30 mpaka 45.
Baada ya kupata alama hizo, Dk Msonde alisema walitafuta wastani wa A katika miaka hiyo 12 ambao ulikuwa ni 76.2 na wengi waliopata A ya chini katika muda huo ilikuwa 75.
Katika kutafuta wastani wa D katika miaka hiyo 12, ulikuwa 33.3 na D iliyotumika sana katika miaka hiyo ilikuwa 30 ndipo wakaamua kuweka viwango vipya vya ufaulu.

*Viwango vipya
Baada ya wastani huo, Dk Msonde alisema walianza kupanga viwango vipya vya ufaulu ambavyo vitatumika katika usahihishaji wa mtihani wa taifa wa kidato cha nne na mtihani wa taifa wa kidato cha sita, ambao hautakuwa na tofauti katika ya mitihani hiyo.
Kabla ya viwango hivyo, kidato cha sita kilikuwa na alama saba za ufaulu, yaani A, B, C, D, E, S na F wakati kidato cha nne kilikuwa na alama sita za ufaulu, yaani A, B, C, D na F.
Katika viwango vipya kutakuwa na alama saba za ufaulu kwa mitihani yote ya kidato cha nne na kidato cha sita, ambayo ni A ambayo itaanzia (75-100), tafsiria yake ni Bora sana.
Kutakuwa na B+ (60-74, vizuri sana); B (50-59, vizuri); C (40-49, wastani); D (30-39, inaridhisha); E (20-29; hairidhishi) na F (0-19, amefeli).
* Madaraja zamani
Mbali na mabadiliko katika viwango vya ufaulu, mabadiliko mengine yaliyofanyika ni katika ukokotoaji wa madaraja ya ufaulu, kutoka Mfumo wa Ukokotoaji wa Jumla wa Pointi (TPGS), ambao umekuwa ukitumiwa tangu 1973 mpaka  2014 kwenda Mfumo wa Wastani wa Ukokotoaji wa Pointi (GPA) utakaotumika katika matokeo ya kidato cha nne ya mwakani.
Katika mfumo wa TPGS, alama A ilikuwa na pointi 1; alama B+, pointi 2; B, pointi 3; C pointi 4; D pointi 5; E pointi 6 na F pointi 7.
Kwa kuwa upangaji wa madaraja, uliangalia masomo saba ambayo mwanafunzi alifaulu zaidi, mwanafunzi aliyefaulu sana katika mfumo huo, kwa maana ya kupata alama A masomo yote saba, alipata Daraja la Kwanza lenye pointi  saba, kwa maana na kila somo  pointi moja.
*Madaraja mapya
Katika mfumo wa GPA, Dk Msonde alisema alama A inakuwa na pointi 5; B+, pointi 4, B pointi 3; C pointi 2; D pointi 1; E pointi 0.5 na F pointi 0. Katika hilo, mtahiniwa ataanza kuhesabika amefaulu somo endapo atapata alama D, ambayo ni sawa na pointi 1.
Akielezea namna alama hizo zitakavyotumika kupanga madaraja, Dk Msonde alisema mfumo utakuwa kujumlisha alama za ufaulu za mwanzo katika masomo saba na kugawanya kwa saba, hivyo mwanafunzi atakayefaulu sana na kupata alama A katika masomo saba, atapata jumla ya alama 35, ambayo ikigawanywa kwa masomo hayo saba, atapata pointi 5, ambayo ndiyo utaulu wa juu utakaoitwa ‘Distinction’.

Hivyo madaraja mapya kwa kidato cha nne yatakuwa daraja la kwanza ‘Distinction’  pointi (3.6-5.0);  pili ‘Merit’ (2.6-3.5); tatu ‘credit’ (1.6-2.5); nne pass (0.3-1.5) na aliyefeli ‘fail’ (0.0-0.2).

Kwa kidato cha sita, atakayefaulu sana kupata A katika masomo matatu ya ‘combination’, atakuwa amepata jumla ya pointi 15 na ukigawanya kwa tatu, yaani masomo matatu ya ‘combination’, naye atapata 5.

Hivyo madaraja mapya kwa kidato cha sita yatakuwa daraja la kwanza ‘Distinction’ pointi (3.7-5.0); pili ‘Merit’ (3.0-3.6); tatu ‘Credit’ (1.7-2.9); nne ‘pass’ (0.7-1.6) na aliyefeli ‘fail’ (0.0-0.6).
 source:Habarileo

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Usahihishaji mpya sekondari waanza
Usahihishaji mpya sekondari waanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZAPj0H5hanXTiKQ3gdShbc1o18kfLtL5SFpiT53vnS3JZyFrqsmBxxjJLZWC5jThD6bfgVG-0XaCsFLWOa_w4RRTCcqHLs3SPXbNN4NTy_-Ec5bKCb-3ryngsOcpvEqoPnzVfpFsqK2E/s1600/shukuru+kawambwa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZAPj0H5hanXTiKQ3gdShbc1o18kfLtL5SFpiT53vnS3JZyFrqsmBxxjJLZWC5jThD6bfgVG-0XaCsFLWOa_w4RRTCcqHLs3SPXbNN4NTy_-Ec5bKCb-3ryngsOcpvEqoPnzVfpFsqK2E/s72-c/shukuru+kawambwa.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2014/08/usahihishaji-mpya-sekondari-waanza.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2014/08/usahihishaji-mpya-sekondari-waanza.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy