Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza Wananchi walio wengi (70%) wanaripoti kuwa sauti zao hazisikiki katika maamuzi ya Serikali. Pamoja n...
Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza |
Kimsingi, haya yanaonesha
hisia zilizofanana – kwamba mbali na uchaguzi unaofanywa wakati wa kupiga kura
– wananchi wengi hawana ushawishi kwenye maamuzi ya Serikali au shughuli zake.
Wananchi pia wanaonekana
kuwa na imani ndogo na taasisi rasmi au maafisa wa Serikali za mitaa katika
kushughulikia masuala yao:
wananchi tisa kati ya
kumi wakiwa wameripoti kuwa hawajawahi kuzungumza au
kuwasiliana na mbunge wao
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita. Pia, wananchi (47%)
waliripoti kutowahi kuzungumza na mwenyekiti wao wa mtaa/kijiji ili kujadili
masuala yanayowahusu. Ni mwananchi mmoja tu kati ya saba (16%) aliye mwanachama
wa chama cha siasa.
Matokeo haya yametolewa
na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Wananchi wana uchu wa mabadiliko: Je, wananchi
wanashiriki na wanaweza kuiwajibisha serikali?
Muhtasari umetokana na
takwimu ya Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa
kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi kote Tanzania Bara.
Licha ya mwingiliano
mdogo ulio wazi kati ya wananchi na mifumo rasmi ya serikali, wananchi 6 kati
ya 10 (58%) wanaripoti kuwa wamewahi kushuhudia wananchi wakipeleka malalamiko
kwa viongozi ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Malalamiko haya kwa
kawaida huandaliwa ili kudai maboresho kwenye huduma za umma katika ngazi za
mitaa. Masuala yaliyoonekana kulalamikiwa sana yalikuwa ni pamoja na utoro wa
walimu na upatikanaji haba wa maji safi na salama.
Linapokuja suala la
kuibua na kuzungumzia masuala yanayoihusu jamii, Sauti za Wananchi ilibaini
kuwa watu walijitahidi kuzungumzia matatizo yaliyowakabili.
Wananchi nane kati ya
kumi (84%) walizungumzia masuala yao walipokutana katika makundi. Wananchi
wengine watatu kati ya kumi walipiga simu kwenye vipindi vya redio 32% na 31%
walilalamika kwa marafiki zao.
Katika kuchukua hatua za
kuungana pamoja na kusimamia jambo, wananchi walionekana kuwa wenye uwezo mdogo
wa kususia mijadala. Ni 9% tu walioripoti kuwa wameshawahi kususia mijadala
ndani ya kipindi cha mwaka uliopita, 8% walishiriki maandamano, 6% waliokataa
kulipa kodi na waliotumia nguvu kufanikisha suala la kisiasa walikuwa (1%).
Kwa kawaida, vikundi vya
kijamii hufanya kazi kubwa kusaidia maisha ya watu. Watanzania saba kati ya
kumi waliripoti kuwa wamejiunga na moja ya
makundi la kijamii.
Makundi ya kidini pia yalionekana kuwa maarufu sana: mwananchi mmoja kati ya
watatu (36%) alionekana kuwa amejiunga na kundi la kidini na wananchi wa tatu
kati ya kumi (30%) walishiriki katika karibu nusu ya mikutano yote
iliyoandaliwa na kundi lake. Mbali na makundi ya
kidini, vyama vya kuweka
na kukopa vilishika nafasi ya pili, ikiwa wananchi wawili kati ya kumi (22%)
walikuwa ni wanachama wa vyama/vikundi hivyo.
Wengi wao (20% ya
wananchi) walihudhuria angalau nusu ya mikutano ya vikundi.
Mshikamano miongoni mwa
jamii ulionekana kuwa mkubwa: karibu wananchi wote (98%) waliamini kuwa kama
lingetokea tukio lisilotarajiwa, kwa mfano nyumba kuungua moto, jamii yao bila
shaka ingekusanyika kusaidia. Kwa upande mwingine, wananchi walipoulizwa kama
waliwaamini watu kwa ujumla, tisa kati ya kumi (87%) walionekana kuwa makini
sana walipokuwa wakishirikiana na
watu wengine.
Wananchi saba kati ya
kumi (68%) wameripoti kuchangia moja kwa moja katika
ujenzi au ukarabati wa
vituo/majengo ya umma. Kati ya hawa, wananchi walio
wengi (88%) walichangia
fedha na (12%) waliobaki walichangia muda wao. Hii
haikulingana na viwango
vya ukusanyaji wa kodi, lakini ilionesha kuwa
wananchi kwa njia moja au
nyingine huchangia uendeshaji wa serikali. Hata
hivyo, makusanyo
hayaratibiwa vizuri kisheria, michango haikusanywi kwa
haki wala kutumika kwa
tija chanzo kikiwa uwazi mdogo na mfumo dhaifu wa
kudhibitiana. Wananchi
wanne kati ya kumi (39%) waliochangia vituo vya umma
walisema walilazimishwa
kufanya hivyo, na hii iliondoa imani ya wananchi.
Walipoulizwa, wananchi
walihisi kuwa na uwezo wa kuzitegemea jitihada zao
wenyewe ili kufanikisha
mambo yao. Watanzania saba kati ya kumi (70%)
waliitetea kauli hii na
kusema kuwa wanao uwezo wa kujisimamia mambo yao
wenyewe na kukabiliana na
changamoto zinazowakabili. Pia wanaweza kutafuta
ufumbuzi wa matatizo yao
na kutimiza malengo yao wenyewe.
Rakesh Rajani, Mkuu wa
Twaweza, alitoa maoni juu ya matokeo haya akisema:"Watanzania ni wanajamii
hupeleka malalamiko yao kwa viongozi. Pia Watanzania wanaamini wana uwezo wa
kukabiliana na vikwazo maishani mwao, lakini hawaamini wana uwezo wa
kuishawishi Serikali.
Wananchi wengi wanakwepa
kujihusisha na vitendo vya kufanya jambo kwa hisia hasi au kali kama vile
kukataa kulipa kodi, maandamano au matembezi ya kupinga jambo fulani. Lakini
changamoto
muhimu za utoaji huduma
bado zipo kwenye sekta zote kuu. Kama serikali
haitakuwa sikivu zaidi
kwa hatua hizi, tunaweza kushudia wananchi wakiwa
wakali zaidi katik siku
zijazo."*
mwisho
Muhtasari huu na takwimu
zilizomo zinapatikana hapa www.twaweza.org, au
www.twaweza.org/sauti
COMMENTS