TAMKO LA PROFESA LIPUMBA WA CUF KUHUSU MAUAJI YA JANUARI 26,2001

TAMKO 27 Januari 2015 MAADHIMISHO YA MAUAJI YA JANUARI 26 NA 27, 2001 YA CUF YATOKANAYO NA MAANDAMANO YA KUDAI HAKI Siku ya l...



TAMKO
27 Januari 2015
MAADHIMISHO YA MAUAJI YA JANUARI 26 NA 27, 2001 YA CUF YATOKANAYO NA MAANDAMANO YA KUDAI HAKI
Siku ya leo siyo siku ya furaha hata kidogo na wala si siku ya kujifaharisha, ni siku ya kihistoria kwa chama chetu, ni siku ya kukumbukwa sana, miaka kumi na nne iliyopita tarehe kama ya leo tarehe 27 Januari, 2001 na tarehe kama ya jana tarehe 26 Januari 2001, Wanachama wenzetu waliojitoa muhanga, leo hii hawapo wamekwenda mbele ya haki katika siku kama hii, mama zetu na dada zetu wanaikumbuka kwa huzuni kubwa siku kama hii ya leo, kwani si vyema kuwakumbusha lakini inatubidi tuyakumbuke yaliyowakuta siku kama hii ya leo, mama zetu na dada zetu walibakwa na kunajisiwa na askari wa kidhalimu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi, na wengine wakaachwa mayatima kwa waume zao kuuwawa na askari hao hao wa kidhalimu, na kutuachia mayatima na wengine hadi leo wanaishi na ulemavu.
Kwa mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha wakimbizi kwa ndugu zetu na wanachama wenzetu ilibidi wakimbilie Mombasa nchini Kenya katika kunusuru maisha yao, wapo wengine  waliyakimbia makazi yao na kuishi maporini na wengine walifia baharini wakati wakijaribu kujinusuru.
Tukizikumbuka nasaha nzuri alizozitoa Mwenyekiti wetu Prof. Ibrahim Haruna Lipumba mwezi Oktoba 2001 pale Bwawani Hotel Zanzibar wakati wa kutiliana saini mkataba wa Muafaka alisema kwamba “Ni vyema tukaendelea kuyakumbuka yaliyotokea ili ibaki kuwa kovu itakayotufanya tusiweze kuyarudia tena yale yaliyosababisha maafa kama yale kutokea”.  
Tukiikumbuka siku kama ya leo inatubidi pia kuzikumbuka siku mbili kabla ya leo, yaani Januri 25, 2001 wakati Mwenyekiti Prof. Ibrahim Haruna Lipumba alipopigwa na wenzake na kuvunjwa mkono na askari wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi na kumkamata pamoja na Viongozi wengine waandamizi na wanachama wenzetu na kuwafungulia kesi ya uchochezi.
Mwenyekiti alikuwa akitekeleza misingi ya Demokrasia kwa mujibu wa katiba ya nchi ya kukusanyika na kutoa mawazo yako hadharani, jambo ambalo aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Wiliam Benjamin Mkapa alishatoa amri kwenyae hotuba yake ya kuuaga mwaka 2000 na kuingia mwaka mpya wa 2001 kwa kukataza mikutano ya hadhara pamoja na maandamano akidai kwamba uchaguzi umemalizika na washindi wameshajulikana hivyo ni vyema tukaungana katika kuijenga nchi kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba katika hotuba yake pale Mbagala Zakiem kabla ya kukamatwa kwake, pamoja na kusisitiza nchi kuendeshwa kwa kufuata misingi ya utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria, lakini pia aliahidi kuwa kwa vile nchi yetu imepoteza sifa na dira ya kuitwa nchi yenye misingi hiyo, suluhisho pekee ni kufanya maandamano nchi nzima na yeye ndie atakae yaongoza maandamano hayo ambayo aliyatangaza kufanyika siku ya tatu yake yaani tarehe 27, Januari 2001.
Katika maandamano hayo tulikuwa na madai manne;
  1. Kutomtambua Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kutaka uchaguzi urudiwe
  2. Kudai  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
3.     Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
  1. Katiba Mpya
Pamoja na Mwenyekiti wetu kumkamata wakidhani kwamba watakuwa wamefanikiwa kutuzuia tusiandamane, halikadhalika watu wawili waliuliwa siku moja kabla, yaani tarehe 26 Januari pale Zanzibar, kwa agizo la aliekuwa Makamo wa Rais Marehemu Dk. Omari Alli Juma wakiamini watakuwa wametutisha kiasi cha kutosha, lakini wapi, tuliandamana na wenzetu wengine wakawa muhanga. MWENYEZI MUNGU ZILAZE ROHO ZA MAREHEMU WOTE WALIOJITOA MUHANGA MAHALI PEMA PEPONI – AMINY!!
Narudia tena kwa msisitizo; ni hali ya kusikitisha kila inapofika siku kama ya leo, inatukumbusha madhila tuliofanyiwa ndani ya nchi yetu kwa kudai haki, inatukumbusha damu ya ndugu zetu iliyomwagika kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha ulemavu walioupata ndugu zetu kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha dada zetu na mama zetu walioachwa vizuka kwa waume zao waliuwawa kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha binti, dada zetu na mama zetu walibakwa kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha watoto walioachwa yatima kwa sababu yakudai haki, inatukumbusha watu walisamehe Ubunge wao na Uwakilishi wao katika baraza la wawakilishi kwa sababu ya kudai haki.
Muhanga huu waliojiotoa ndugu zetu, ndio matokeo na mafanikio yaliyojitokeza sasa hivi hadi kufikia wengine kujidai na kujifaragua na kufikia hata kutoa kejeli na maneno ya kifedhuli na kebehi, wakati ndugu zetu wanapoteza maisha yao kwa kuandamana wao waliona tunaigiza.
Mafanikio katika madai yetu yale manne;
1.     Kuhusu kutomtambua aliekuwa Rais wa Zanzibar Amani Karume na kudai uchaguzi kurudiwa; kulipelekea kufikiwa kwa muafaka kati yake na Katibu Mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad, ndio uliopelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ambapo chama chetu kipo varandani Ikulu kwa Maalim Seif kuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na tunatarajia mwishoni mwaka huu Oktoba 2015 tunaichukua wenyewe Ikulu ya Zanzibar.
2.     Kuhusu madai ya Tume Huru ya Uchaguzi, kwa upande wa Zanzibar Tume hiyo iliundwa pamoja na  kugubikwa na wingi wa makada wa Chama cha Mapinduzi kutokana na mfumo mbovu wa uteuzi, lakini tunaamini huu ni mwanzo tu, kilichobakia ni kupigania maboresho ya Tume hiyo kuwa Huru Kwelikweli na si kama ilivyo sasa. Tunaiasa CCM na Serikali yake Bila Uchaguzi huru na wa Haki Oktoba 2015 Taifa linaweza likarudia historia ya mwaka 2001.
3.     Kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga kura tulifanikiwa kulipata, nalo huwa linachafuliwa na wajanja wa Chama cha Mapinduzi kwa kulitia mikono, lakini nalo tutalipigania kuhakikisha linatumika ipasavyo na kama tulivyokusudia wakati wakulidai, na kwa vile kuna maboresho ya mfumo mpya wa daftari, tunawaomba wanachama wetu tuhamasishane tujitokeze wote kwenda kujiandikisha kwa Dar es Salaam uandikishaji unaanza Februari 15 mwezi ujao.
4.   Kuhusu kupatikana kwa Katiba Mpya, ambapo ndani yake kungekuwa na Tume Huru ya Uchaguzi  na mengineyo yaliyomuhimu kwetu sisi katika kuleta haki na usawa kwa wote, CCM na Serikali yake wameuteka mchakato huo hatua za Mwisho za Bunge la Katiba na kuyatupilia mabali mambo yote muhimu yatokanayo na michango ya wananchi wenyewe yaliyokusanywa na Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba na kuingiza mambo yao yenye maslahi ya kifisadi kwa Taifa.  CUF – Chama Wananchi tunatoa AGIZO ni marufuku kwa wanachama na wapenzi wetu wote nchi nzima kujitokeza kwenda kupiga kura ya maoni, kwani kushiriki kwa aina yoyote hata kupiga kura ya hapana ni kubariki mchakato haramu uliofanywa na Mafisadi wa Chama cha Mapinduzi.
Waheshimiwa Wanachama katika kuyaenzi Maadhimisho haya tunatakiwa kuongeza nguvu, mshikamano, umoja na kupeana nafasi kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea kwa kuzingatia katiba yetu na kanuni zetu, kwa kuhakikisha kwamba chaguzi zijazo za kura za maoni ndani ya chama zinatupatia Wagombea wanaokubalika katika jamii katika nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais.   Tuepuke majungu na makundi yanayoleta faraka ya wenyewe kwa wenyewe, kama waliowengi wanakuona huwezi kuwafikisha wanakotaka, wewe kubali yaishe, ikifika wakati wa kuaminika kwako watakupa nafasi, tuache kususa na hata kuingia msituni baada ya matokeo ya  kura za maoni ndani ya chama.
Waheshimiwa wanachama wenzetu, tunawaomba na tunawasihi sana tuyatumie maadhimisho haya  katika kushauriana namna bora ya kuboresha chama chetu, na hasa katika kuongeza wanachama watakao kipatia chama chetu ushindi, na tunaendelea kusisitiza kimbilio letu kubwa liwe ni kwa vijana wetu tulionao, ni aibu kubwa sana kama utakuwa na kijana mwenye umri wa kupiga kura na asikuunge mkono wewe kama mzazi wake au mlezi wake, tukumbuke wosia wa Muasisi wetu Marehemu Shaaban Khamis Mloo, kuwa tuhamasishane kunzia katika sahani ya chakula, kitandani, ndani ya shuka, uwani, barazani, chumba kwa chumba, mlango kwa mlango, nyumba kwa nyumba, katika vijiwe vya kahawa, mabaraza ya bao, kinamama wanaposukana, vilabu vya mipira, maofisini na kila penye mkusanyiko wa watu na tujiwekee ahadi kila mwanachama mmoja imalizikapo miezi mitatu angalau awe ameingiza ndani ya chama sio chini ya wanachama wapya  watatu.
MWISHO;
Tunawaomba radhi na tunawapa pole Wanachama wenzetu wote wa CUF – Chama cha Wananchi, kwa kuwakumbusha siku hii nzito kwetu na ya majonzi makubwa TUNAJUA MMEGUSWA, lakini tujifute machozi yetu kwa kuenzi moyo wa kujitoa kwa ajili ya chama ili kuhakikisha haki inapatikana na chama chetu kinapata ushindi katika uchaguzi huu ujao, hii ndio namna bora ya kuwaenzi WAHANGA wetu, tukumbuke “WOGA NI ADUI WA HAKI”
HAKI SAWA KWA WOTE                
Prof.Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti CUF Taifa


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4811,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: TAMKO LA PROFESA LIPUMBA WA CUF KUHUSU MAUAJI YA JANUARI 26,2001
TAMKO LA PROFESA LIPUMBA WA CUF KUHUSU MAUAJI YA JANUARI 26,2001
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRFQWGUm6JGhLBPErsnsmZ_NNfJMOLbrlHki38C3pzVfcVzEkbN1HwU-Lk6WrLudnq3qujpYfB8GBcbf_947CoJ2Vl-yKNH_vK1UTeTuRnDhl-Gkx6CrZ9HJEGUY2WJM-Wbv1XTWlA-Xs/s1600/lipumba+kwenye+karandinga.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRFQWGUm6JGhLBPErsnsmZ_NNfJMOLbrlHki38C3pzVfcVzEkbN1HwU-Lk6WrLudnq3qujpYfB8GBcbf_947CoJ2Vl-yKNH_vK1UTeTuRnDhl-Gkx6CrZ9HJEGUY2WJM-Wbv1XTWlA-Xs/s72-c/lipumba+kwenye+karandinga.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2015/01/tamko-la-profesa-lipumba-wa-cuf-kuhusu.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/01/tamko-la-profesa-lipumba-wa-cuf-kuhusu.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy