Ubabe wa polisi unakuaje hasa...wakodishwa kumtia mtu adabu wamvunja mikono.. Dar wavuta pikipiki na kuwatumbukiza mtaroni abiria

Mkazi wa Loksale, Samweli Shani (47), akiwa amefungwa POP baada ya kuvunjwa mikono yake na polisi, kushoto ni ndugu yake Gabriel Shani akio...

IMAG2765

Mkazi wa Loksale, Samweli Shani (47), akiwa amefungwa POP baada ya kuvunjwa mikono yake na polisi, kushoto ni ndugu yake Gabriel Shani akionyesha picha za X-ray alizopigwa zikionyesha jinsi mikono ilivyovunika.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, amekiri kupokea malalamiko ya mkazi mmoja wa Loksale wilaya ya Monduli, Samwel Petro Shani (47) ya kuvunjwa mikono yake miwili kutokana na kipigo cha askari Polisi wa kituo cha Leskale.

Hata hivyo amesema kwamba kwa sasa yupo likizo ila aliwasiliana na mkuu wa kituo cha polisi Monduli (OCD) ili kupata undani wa tukio hilo.

Imedaiwa kuwa kipigo hicho kimesababishwa na mfanyabiashara mmoja ambaye alikodisha askari ili kumfunza adabu kwa kushindwa kulipa fedha zake anazomdai zipatazo 250,000.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la ,Shamimu alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi alikana kukodisha askari wa kumpiga na kumvunja mkono mlalamikaji .

Alisema yeye kama mwananchi alienda kulalamika kituo cha polisi kuhusu deni lake kwamba kilichotokea huko baada ya yeye kuondoka hafahamu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mlalamikaji Samweli askari hao hawakutaka kumkamata bali kuitoa roho yake kwani walikuwa wakitumia chuma kinene kumpiga na kumvunja mikono yake miwili huku mwingine alikuwa akimshambulia kwa rungu na mateke.

Alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Februali 6,mwaka huu majira ya saa 3 usiku na kwamba aliwatambua askari wawili waliomtesa kwa kipigo kuwa ni Steven na Justini wote ni askari wa kituo hicho cha Loksale.

''Mnamo tarehe 6 mwezi huu majira ya saa 3 usiku,walikuja askari wawili wakiwa wamevaa nguo za kiraia ,walinikuta nimekaa kwenye ukuta nikiwa na kijana mmoja,walinikamata na kunifunga pingu wakiwa wamenikandamizia chini ,walinipiga sana na kunivunja mikono yangu miwili''alisema Samweli

Akisimulia chanzo cha tukio hilo alisema, mfanyabishara Bi. Shamimu alienda katika kituo hicho cha polisi na kuwaeleza askari hao kuwa alikuwa akimdai shilingi 250,000 na kwamba sikuwa nimemlipa deni hilo.

''Ni kweli Shamimu alikuwa akinidai shilingi 250,000 ila nilishamlipa shilingi laki moja na kubaki sh,150,000 ,hizo hela kuna msichana nilimdhamini alikuwa mfanyakazi wa duka lake aliyedai alimwibia,ndipo mimi kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na msichana huyo nilikubali kulilipa deni hilo''alisema Samweli

Alisema askari hao walimvamia na kumkaba kabari kisha askari mmoja alimfunga pingu na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na rungu na chuma na walipoona wamepoteza fahamu baada ya kumvunja mikono walimkokota hadi kituo cha polisi na kuendelea kumpiga sehemu zingine za mwili ikiwemo miguuni.

''Baadae usiku wakiwa wamenifungia lokapu alikuja mkuu wa kituo na kuniangalia ,alikuta hali yangu ni mbaya na kuondoka bila kusema lolote''alisema.

Hata hivyo askari hao waliingiwa na woga kutokana na hali yake na kuamua kumchukua usiku huo wa manane na kumpeleka katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

Alieleza kuwa kesho yake askari hao walimchukua na kumpeleka kituo cha polisi wilaya ya Monduli na kumweka lokapu.

Aliongeza kuwa mkuu wa upelelezi wa wilaya OC CID,aliyemtaja kwa jina moja la Bw. Abichi alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila alitakiwa akubaliane na masharti ya dhamana .

''OC CID aliniambia kuwa nataka nikupatie dhamana ila kwenye maelezo yako unatakiwa ueleze kuwa ulikuwa unatoroka ulinzi halali wa polisi ukiwa na pingu ,na wakati ukikimbia ulianguka na pingu zikakuvunja mikono yako ''alisema bw Shani.

Aliongeza kuwa hakukubaliana na kauli hiyo ndipo OC CID alipoamua kumrudisha lokapu ,ambapo alikaa kwa muda wa siku nne wakimbembeleza akubaliane na maelezo ya polisi .

Alisema kuwa aliamua kuwa na msimamo huo,hadi tarehe 12 walipoamua kumfikisha mahakama ya wilaya ambapo alisomewa shitaka , la kuvunja na kuiba na kujaribu kutoroka polisi akiwa na pingu, suala ambalo ni uongo uliolenga kupoteza haki yake ya kulalamikia jeshi hilo.

Imeandaliwa na Woinde Shiza wa libeneke la kaskazini blog
post hii ya Arusha imenikumbusha zari la leo asubuhi kiasi cha saa tatu kasoro au mbili na nusu hivi katika taa za kuongozea magari tazara, eneo la sub station ya Tanesco hapa dar es salaam.Askari doria (si trafiki) alimvuta mwenyepikipiki akiwa amepakia abiria na matokeo yake pikipiki ikajikita katika msingi wa kwenye mtaro na jamaa wakaumia wote wawili na pikipiki ikaharibika. Lakini cha kushangaza abiria akilalamika kwanini wamevutwa na kuletewa shida, alipigwa pingu na askari aliyeivuta pikipiki ile kwa nyuma (mzaha wa kijinga kabisa huu). Askari huyu alikuwa amebeba bunduki ya G5 kwa wale tuliopitia hii kitu au tuseme Nato 5 (enzi zetu ndivyo tulivyoziita zile bunduki za Nato) hizi bunduki zina tofauti na SMG tulizozoea kitaani kutoka China) ambayo bati yake (kitako) ilikuwa na namba mbili. Askari huyu unaweza kumtambua kwa bunduki hiyo yenye namba 2 lakini amejivalia miwani meusi hakuwa na adabu kabisa anamesababisha ajali mbaya ya pikipiki kisha anajiona anasheria. Pikipiki ya watu imeharibika, abiria na dereva wake mtaharuki na kisha anamtia pingu raia anayelalamika, watu wanamwambia mvue pingu jamaa, yeye anaonekana kutaka kujihami na silaha yake hawa askari vipi hawa? Anakuja trafiki pale naye anashangaa, haelewi, anakuja afisa wa kawaida naye anashangaa lakini jamaa wanamtyia pingu na mwingine anakokota pikipiki ile ambayo steringi imevunjia upande wa kushoto. Madigani imetoka ya mbele na saiti mirror imepasuka. Sijui kama Kapinga anajua hili au kamanda kova na ninaamini jamaa atabambikiwa kesi kama si ya kutoroka chini ya ulinzi wa polisi basi ni wizi. Hii ni tabia ya kishenzi kabisa utamtiaje mtu pingu kumtisha ?Shen**** kabisa. nimekasirika sana kwa uonevu wa askari yule.nilitaka kushuka katika basi konda akanizuia manake angezushiwa seleka nilitaka tu kwenda kusoma namna ya unifiomu yakekimya kimya nijue kufuatilia hili.nimeishia kukariri bati ya bunduki tukwamba ina namba 2 nyeupe kama wanaweza kudhuru watu hawa waliobarabarani hawa kweli si ndio usiku wanakuwa majambazi hawa! . Askari Polisi aliyefundwa hawezi kufanya mambo ya kishenzi hapa, kundi kubwa la wenye pikipiki walisimama, kama wakichukua sheria mkononi kw akuona kilichompata mwenzao inakuaje? Huyu askari aliyekuwa hapo doria anastahili kuchukuiliwa adhabu ili wengine wakome.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Ubabe wa polisi unakuaje hasa...wakodishwa kumtia mtu adabu wamvunja mikono.. Dar wavuta pikipiki na kuwatumbukiza mtaroni abiria
Ubabe wa polisi unakuaje hasa...wakodishwa kumtia mtu adabu wamvunja mikono.. Dar wavuta pikipiki na kuwatumbukiza mtaroni abiria
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/IMAG2765.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2015/02/ubabe-wa-polisi-unakuaje-hasawakodishwa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/02/ubabe-wa-polisi-unakuaje-hasawakodishwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy