MHASIBU wa Kampuni ya Serikali (TSN) inayochapia magazeti ya Dailynews, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo Shafi Mpenda (36...
MHASIBU wa Kampuni ya Serikali (TSN) inayochapia
magazeti ya Dailynews, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo Shafi
Mpenda (36) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge
katika Jimbo la Mlele mkoani Katavi kupitia CCM katika
uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2015.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye anashikilia
Jimbo hilo la Mlele ameshatangaza rasmi kuwa hatagombea
tena .
“Nikiwa mzawa wa jimbo hili, nilitafakari kwa makini sana, na kujiuliza maswali mengi sana……….
Hatimaye nimepata majibu kwamba baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye taasisi yaSserikali, wakati umefika wa kurudi nyumbani na kuwa karibu zaidi na wananchi wenzangu wa jimbo hili ili niweze kuwatumikia na kutoa mchango wangu katika maendeleo ya jimbo letu na mkoa wa Katavi kwa ujumla wake.
Nawaomba wananchi wenzangu waniamini kwamba Kazi hii naiweza, naimudu, nimejipima na nimeona natosha katika kuwa sauti kwa wale wasio na sauti ……….. Baada ya kuangalia changamoto tulizonazo, najua wapi tunataka kwenda ikizingatiwa kwamba Katavi bado tupo nyuma sana kimaendeleo” alieleza .
Akifafanua anaongeza kuwa Mbunge wa Jimbo hilo Pinda ambae pia ni Waziri Mkuu amefanya mambo makubwa sana ya kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Katavi na wilaya mpya ya Mlele.
“ Kwa maana nyingine ni kwamba, serikali sasa imesogea karibu na wananchi kwa ajili ya kuwahudumia vizuri zaidi……..
Aidha, mzee Pinda ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya elimu, na sekta hii ni miongoni mwa mambo ambayo nakusudia kuyapa kipaumbele iwapo wana CCM wenzangu watanichagua kwenye kura ya maoni na kunipa ridhaa ili niweze kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba, 2015” alibainisha
Alitaja meneo mengine ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kilimo ambacho kinajumuisha bei ya mazao ya biashara kwa mfano tumbaku,
“ Kero zinazowakabili watu wa katavi ni nyingi na zinahitaji mtu imara kama Mzee pinda mwenye uwezo mkubwa wa kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya katavi. Miongoni mwa kero kubwa ni pamoja na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Mawasiliano ya simu, barabara na Reli, maji, afya pamoja na elimu” alieleza
Aliongeza kuwa nachokiona yeye (Mpenda) ni fursa nyingi za kuleta mabadiliko katika mkoa wa Katavi ambazo zinahitaji mtu makini, mbunifu, mwenye uwezo mkubwa wa kushughulikia mabadiliko kwa kasi na kwa vitendo, aliye tayari kutumwa na akatumika, msikivu na mwenye hofu ya mungu, mwenye upendo na aliyekulia katika kupenda maendeleo.
Wengine ambao wamejitokeza kutaka kurithi mikoba ya Waziri Mkuu Pinda ni pamoja Kamwele Isack Kilinda ambaye ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Katavi, Lephy Gembe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Emmanuel Nzumba ambaye ni Mfanyakazi wa Tanapa-Simiyu.

Kadhalika wengine ni pamoja na , Maganga Kampala ambaye ni
mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM, Richard Mbogo ambaye ni Kamanda wa
Vijana CCM wilaya ya Mlele, Oscar Albano ambaye ni Mtaalamu wa kilimo,
Pudenciana Kikwembe ambaye ni Mbunge wa viti maalumu jimbo la katavi.
COMMENTS