ZIFF inakuja, wasanii tupo tayari?

MSIMU wa   tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF)   umefika na waandaazi wake wamewakumbusha wasanii na watengeneza filamu p...



MSIMU wa  tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF)  umefika na waandaazi wake wamewakumbusha wasanii na watengeneza filamu pamoja na wawezeshaji, kwamba sasa ni muda wa kuwasilisha kazi zao kwa ajili ya kuangaliwa na zikipasi ziwekwe katika kabati la kuoneshwa.
Wiki iliyopita meneja wa tamasha hilo, Dan Nyalusi  alisema kwamba kuna siku chache zilizobaki ambazo watu wanaweza kuwasilisha kazi zao na si lazima wafike Zanzibar bali wanaweza kusafirisha kazi hizo kwa njia ya kisasa ya mtandao.
Wakati sampuli ndio zinatakiwa, wageni wao ndio wamekuwa kila mara makini zaidi kuchangamkia fursa hiyo inayotokana na tamasha hilo linalofanyika katika ardhi ya Tanzania, likileta kila aina ya watu kushiriki katika utamaduni wa mwambao, kuliko wenyeji.
Kazi zinazotakiwa kuwasilishwa ni za filamu, muziki, sanaa za uchoraji na uchongaji na kadhalika.
ZIFF moja ya matamasha makubwa kabisa ya filamu Afrika Mashariki linalofanyika nchini Zanzibar katika visiwa vya Unguja kwa siku takribani kumi  linawawezesha wasanii kukutana na kuonesha kazi zao kwa jamii na kwao wenyewe na kuwezesha mawasiliano ya kikaribu kama soko la filamu na kadhalika.
Kutoka pande zote za Afrika na dunia kuna muziki, kuna sanaa, kuna filamu na kuna fasihi inayojadiliwa, kudadavuliwa na kupewa majibu yanayopelekea wanazuoni kuona siku za mbele za binadamu kwa kuangalia historia yake.
Kuna faida kubwa ya kushiriki tamasha hili uwe msanii wa muziki au filamu  na faida kubwa ni kuangalia soko, ladha ya kazi yako na wengine na kuona namna ya kutumia changamoto mbalimbali kama fursa katika kukuza usanii ulionao.
Dan Nyalusi anasema kwamba kazi za watu zinaweza kupelekwa kwa njia ya YouTube, Vimeo, Sound Cloud, picha na kuandika wasifu wa msanii kwa  mpa@ziff.or.tz na  mwisho wa maingizo ni Machi 31 mwaka huu.
Kwa filamu  kuna ushindani mkubwa unaotarajiwa hasa kutokana na kukua kwa masimulizi ya filamu duniani na hasa masimulizi ya karibu na ukweli yenye ladha ya changamoto za binadamu katika maisha yake ya kila siku kutengeneza maisha katika serikali na maisha ya ndani kama mapenzi na matunzo.
Katika tamasha hili tuzo kubwa kabisa ni ya jahazi ya dhahabu na fedha. Na hii hutolewa kwa watengeneza filamu wanaotoka nchi za majahazi pekee. Nchi hizo ni pamoja na zile zinazopakana na bahari ya Hindi na visiwa ndani ya bahari hiyo ikiwamo Iran, Irak na Afghanistan na nchi zote za Afrika.
Tuzo nyingine ni ya  Sembene Ousmane  ambayo imewekwa kwa ajili ya ushindani kwa watengeneza sinema wa Kiafrika na wale wanaoishi Ughaibuni na maprojuza wao ambao huenda wakati mwingine ni mapatna.
Kuna kila sababu ya watanzania  kutafuta tuzo hizi ambazo mara ya mwisho ilinyakuliwa na waliotengeneza sinema ya maangamizi na baada ya hapo zimeishia mikononi mwa wageni  na wakati mwingine kutoka nje ya bara la Afrika.
Ushindani wa kupata tuzo upo katika filamu za makala na zile fupi, za kubuni, dokumentari na za vikaragosi zikiwa zimepigwa picha na waafrika na madarekta kutoka nchi za majahazi.
Kwa mujibu wa Nyalusi katika upande wa Dokumentari, seksheni  hii iko wazi katika fomati za aina zote. Seksheni za maendeleo hii iko wazi kwa watengeneza sinema wa kiafrika na pia  kwa watengenezaji waliopo ughaibuni na mapatna zao.
Pia kuna eneo la muziki ambalo limetengwa kwa ajili ya kazi njema ya ubunifu wa muziki kwa watu wa Afrika Mashariki na pia kutakaribisha filamu lukuki  kwa ajili ya starehe, yaani kuburudika lakini hazipo katika ushindani.
Tamasha hili pia lina tuzo nyingine kama ya vipaji Afrika Mashariki inayotolewa na Signis, tuzo ya filamu bora ya Kiafrika kwa mtazamo wa Mtandao wa matamasha ya Ulaya na Afrika na pia kuna tuzo ya Zuku kwa ajili ya filamu zilizotengenezwa kwa Kiswahili za Bongo.
Tamasha la Zanzibar  ukiangalia ukuaji wake na ukubwa wake na mtandao wa kuheshimika unaoendelea kutokea duniani, ni sahihi kusema kwamba ipo haja kwa Watanzania si kuingiza sinema za kuonwa bali za kushindana katika madaraja mbalimbali.
“Ni matarajio yangu kwamba ndugu zangu wa Tanzania na hata Afrika Mashariki watazingatia ushiriki wa ushindani na si tu ushiriki,” anasema Dan Nyalusi ambaye kwa sasa amekomaa na tamasha hilo.
Anasema katika mahojiano kwamba kila mwaka tamasha hilo linaonesha sinema zilizokwenda shule kutoka pande mbalimbali za Afrika hata duniani na katika hilo heshima yake kubwa pia inapatikana kutokana na baadhi ya filamu kuamua kufanya primia.
Filamu za ZIFF ni babu kubwa kwa kuwa zinaangalia sinema zilizozalishwa katika kipindi cha mwaka mmoja na hivyo utimamu wa kufuatilia utamaduni wa sinema na simulizi zake unakuwa wa kisasa zaidi.
Moja ya vitu ambacho  kinavutia katika tasnia ya sinema ni kule kuwa na mambo mengi ya kujifunza pamoja na kwamba unapeleka kazi yako. Tamasha hili limesukwa kwa namna ambavyo linaibua vipaji mbalimbali kutokana na  mfumo wake hasa wa maonesho, matamasha mbalimbali ya sanaa, makongamano na hata maonesho ya jukwaa katika kazi mbalimbali.
Tamasha hili lenye vitu mbalimbali  bado ni tamasha linaloweza kutumika kuinua wasanii Tanzania  hasa wale ambao wanataka kwenda kimataifa.
Tamasha hili linafanyika Julai lakini maandalizi ndiyo hayo yako mbioni huku waandaazi wakikumbusha watanzania ujio huo.
Wakiwa wanapatikana katika jengo la zamani ambalo ni ngome al maarufu kama Ngome Kongwe tamasha hili lina kitu cha ziada kwamba sinema huangaliwa katika  uwanja wa wazi  na kufanya  ladha yake kuwa ya aina yake . Ni wakati wasanii tuchangamkie fursa.

mwisho

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: ZIFF inakuja, wasanii tupo tayari?
ZIFF inakuja, wasanii tupo tayari?
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHRQy0APyXjMeMGpXpkF1Oaf4z2QJLD2vRA2TIn3eEuBNwqUI9xZ2qzOvkTAydD-odkfC16q8dHF5zz5k87TRQtndx3Xhxe_A7CZ4U1lGs3TiZqSjnv2cyK2zCt7fI_wpTVR6cwD_WMUk/s320/zanzibar-international-film-festival.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHRQy0APyXjMeMGpXpkF1Oaf4z2QJLD2vRA2TIn3eEuBNwqUI9xZ2qzOvkTAydD-odkfC16q8dHF5zz5k87TRQtndx3Xhxe_A7CZ4U1lGs3TiZqSjnv2cyK2zCt7fI_wpTVR6cwD_WMUk/s72-c/zanzibar-international-film-festival.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/02/ziff-inakuja-wasanii-tupo-tayari.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/02/ziff-inakuja-wasanii-tupo-tayari.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy