KATIKA filamu nyingi za Kiswahili za waswahili suala la uchawi ni kitu cha kawaida. Tazama sinema zinazotoka visiwa vya karibeani tazama zinazotoka Afrika magharibi na sasa Afrika Mashariki.
Lakini uchawi unaposimuliwa na wazungu  unakuwa na mashaka kwamba wanzungumzia mazingaombwe lakini katika sinema ya The Witch, mheshimiwa mmoja anayejulikjana kwa jina la Robert Eggers  amedhihirisha kwamba anataka watu waogope wasisimke kutokana  simulizi  lake hili la kichawi ambalo ama hakika limesheheni ukatili .
Filamu hii kutoka kwa dairekta ambaye ni kijana tena kutoka Marekani, ni filamu ya kutosha lakini si katika vile ulivyozoea.
Filamu hii ambayo inajulikana kwa jina lingine la "A New England Folktale"  hakika linaangalia katika rekodi za karne ya 17 zilizopo mahakamani, na ni hizi rekodia mbazo dairekta huyu amekuwa na ule ujasiri wa kutishia akili za wengine kwa kutengeneza sinema inayofanana kabisa na mambo ya maiti katika mochwari au kaburini.
Hata lugha wanayotumia kama utatazama trela yake utajua ni kile kiinglish cha kizamani sana cha  lahaja ya "thou" na "thee"  na mara kadha wanazungumzia dhambi ya asili, kama wewe unajua masuala haya ya dhambi ya asili.
Ndani ya filamu hii  sinematografia Jarin Blaschke ameifanya sinema hii kutokuwa na rangi sawia  kiasi ya kwamba unaweza ukafikiri kwamba dunia yote ile unayoiona katika skrini kwa wakati ule ni muonekano wa maiti ilivyo.
Fikiria unaona mtu anachimba kaburi, huku  nyumba ikitoa moshi na nyuma kuna vilima veynye kiza au msichana anakamatwa na  mwanga.
Filamu hii inafuatilia familia moja  ya ambayo ilikuwa na makazi yao kandoni mwa msitu. Wakati mtoto mmoja alipozaliwa na kupotea ndipo mtafaruku katika familia hii ulipoanza uliohusisha mabalaa hayo na  nguvu nje ya uwezo zao zuilizonakishwia vyema na mchawi Bathsheba Garnett anayeishi katika miti ambaye pia alikuwa na malengo ya kuwatwaa watoto wengine wa familia hiyo hasa mkubwa wao Thomasin (Anya Taylor-Joy).
Wasimuliaji wa kisasa wangehusisha zaidi hofu ya wanaukme ya wanawake wanaojitegemea ambao badaae wanatambulika kama wachawi enzi hizo za ujima katika bara la Ulaya lanini kwa sinema hii haikuwa hivyo.
Baba wa familia katika The Witch , William (Ralph Ineson),  ni mtu ambaye hana makosa na ana viwango vyake lakini katika hili la uchawi jamaa alikuwa vingine kabisa.Ni moja ya mambo ambayo unastahili kuyaona na kuyaangalia kwa makini.
Inaweza ikaonekana kwamba mbabe wetu ana matatizo lakini kiukweli, dairekta anatupeleka si kutafuyta mkanganyiko bali kuonesha ukatili unaombatana na uchawi na madhara utaamua wewe mwenyewe.
Wanasema baadhi ya wahakiki kwamba sinema hii ya The Witch  ina namna yake ya kuifurahia lakini ni lazima uangalie mpaka slaidi ya mwisho kwani imetengenezwa kwa namna ambayo inakube akwa maudhi na kumalizia kwa kishindo kikubwa.
Kimsingi mtengenezaji wa sinema hii amechanganya mambo emngi kuhusu uchawi nap engine naweza kusema ameuabudu mno kw alengo la kutiisha watuw anaotazama. Na muda muafaka uliopangwa wa mwaka 1630 ndio miaka mabayo kulikuwa na kelele kubwa za uchawi nchini Uingereza.

Ilikuwa ni familia ya watoto watano baba na mama na adha waliyoipata baada ya kuingia katika eneo jipya ilitikisa familia huku mmoja wa wanafamuilia akituhumiw auchawi.

Pamoja na imani na msimamo wa baba familia hii ilipita katika maizngira magumu sana hasa kutokana na kupotea kwa mtoto wao na mazoa wanayolima kunyauka huku watoto waliobaki wakionekana kupandwa na mizuka.

Muziki ndani ya filamu hii lazima kijasho chembamba kikutoke.kama wazungu wanaweza kuangalia mambo mabaya yaliyowatokea na kuleta jicho la tatu kutengeneza hofu, vipi masimulizi ya majini yakawa mepesi nchini mwetu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO