Abiria 775 wa treni waliokwama Kilosa baada ya stesheni ya Gulwe kukumbwa na mafuriko wamefanyiwa utaratibu na Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuendelea na safari yao kwa treni ya deluxe wakianzia Dodoma leo saa 2 usiku.Wakati taarifa hii inatolewa na Uongozi wa TRL treni iliokwama Kilosa iko njiani kurejea Morogoro ambapo mabasi yapatayo 12 yatawasafirisha hadi Dodoma ambapo watasafiri na deluxe kuelekea Tabora, Kigoma na Mwanza.


Hadi jana asubuhi treni 2 za abiria zilikuwa zimekwama katika stesheni za Dodoma ( treni ya Deluxe iliokuwa inateremka kuja Dar) na Kidete mkoani Morogro ( ilikuwa inapandisha kwenda bara).Abiria 219 wa treni ya Dodoma walipatiwa usafiri mbadala wa mabasi kuja Dar es Salaam lakini hawa wa Kidete ilitarajiwa mafuriko Gulwe yangepungua na kuiwezesha treni kupita salama.

Taarifa za kiufndi Alafjiri ya leo zilithibitisha kuwa mafuriko bado yanaongekeza na hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa aliyekuwepo katika tukio alirejea Kilosa asubuhi leo kutoka Gulwe na kujiunga na abiria wa treni hadi Morogoro . Basi la kwanza linatarajiwa kuwasili Dodoma saa 10 jioni.

Katika taarifa hiyo ya Uongozi umeomba radhi kuwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria na jamaa zao waliokuwa wakiwasubiri kuwapokea katika vituo mbali mbali vya treni nchini.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Aprili 07, 2016
DAR ES SALAAM

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO