KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA MATUMIZI YA FEDHA MTAMBO WA RUVU CHINI.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 141 zilizotolewa na ...



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 141 zilizotolewa na Serikali kugharamia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo kwenda jijini Dar es salaam kufuatia ujenzi wake kukamilika.

Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ya mradi huo ikiwemo mtambo wa Maji wa Ruvu Chini, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanan'g Mhe. Mary Nagu amesema kuwa kamati kamati yake  imeridhishwa na ubora wa  kazi iliyofanyika chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salam ( DAWASA).

Amesema mradi huo wenye urefu wa kilometa 56  umekamilika na kueleza kuwa itakua historia kwa wananchi   wa Dar es salaam waliounganishwa na mtandao wa mabomba ya DAWASCO kukosa maji.



Amesema kama kamati wamejiridhisha kuwa kiasi cha maji kinachozalishwa kwa siku lita milioni 270 kutoka mtambo wa Ruvu Chini ni kingi  na kueleza kuwa kiwango hicho kitaongezwa kwenye uzalishaji wa awali.

"Sisi kama Kamati ya Bunge tumeridhishwa na kazi nzuri iliyofanyika, tumeshuhudia wenyewe maji yanayozalishwa ni mengi tunaipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wakazi wa jiji la Dar es salaam" Amesema Mhe.Nagu.
Amesema kazi iliyopo sasa kwa Serikali na mamlaka zinazohusika ni kuhakikisha kuwa inakabiliana na na changamoto ya usambazaji wa maji hayo ili wakazi wengi zaidi wa jiji hilo wanaunganishwe na mtandao wa mabomba ya DAWASCO.

Amewataka DAWASCO kuifanya kazi hiyo kwa kasi  pia kuangalia upya gharama za usambazaji wa maji pia kuwaangalia upya mawakala waliowekwa kusimamia usambazaji wa maji ili kuwadhibiti wale wasiowaaminifu ili wananchi waweze kupata maji kwa bei nafuu na kuepuka kutumia maji yasiyo salama ambayo yamekuwa chanzo cha milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.

Aidha,ametoa wito kwa wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji ili upatikanaji wa maji hayo uwe endelevu huku akitoa wito kwa Wizara kulifanyika kazi suala la kuwapatia maji wananchi wote wanaoishi kuzunguka miundombinu mikubwa ya maji kote nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara ya wabunge hao kwenye mtambo wa Maji wa Ruvu Chini amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutalifanya jiji la Dar es salaam kupata maji.

Amesema katika kuchukua hatua za kukabiliana na uhaba wa maji Serikali iliamua kufanya maboresho makubwa mifumo ya maji kwa kujenga mipya na kurekebisha ile ya zamani ili kuendana na kasi ongezeko la uhitaji wa maji.

Amesema kazi kubwa ambayo inaendelea sasa ni kuhakikisha usambazaji katika maeneo yenye mitandao ya mabomba na ile ambayo haikuwa na mitandao ya mabomba ili kuwapatia maji ya uhakika.

" Naishukuru kamati kwa kuja kutembelea mradi wetu wametupa changamoto ya kuhakikisha maji yanafika kwa wananchi, sisi kama serikali tuna mpango wa kuhakikisha tunaondoa mifumo yote chakavu katika jiji la Dar es salaam kwa kuweka mipya na hii tunaendelea nayo kwa kasi" Amesisitiza.

Amesema kazi ya kuweka miundombinu ya usambazaji maji  katika jiji la Dar es salaam imeshaanza akifafanua kuwa Serikali imeingia mikataba na wakandarasi kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa viwango.

Aidha, amesema kuwa baadhi ya maeneo ya jiji ikiwemo eneo la Kimara kazi inaendelea huku maeneo ya katikati ya jiji miundombinu yake ni chakavu inaendelea kubadilishwa ili iweze kuhimili wingi na nguvu ya maji inayosukumwa


Ametoa wito kwa wananchi na wenye viwanda kutumia maji hayo ili kulinda afya za walaji kwa kuwa maji hayo ni salama na yamepita kwenye vipimo vya ubora ili kuepuka kutumia maji yasiyo salama ambayo yamekuwa chanzo cha magonjwa.

" Tumeshatoa maelekezo viwanda vyote vya Dar es salaam vihakikishe kuwa vinatumia maji haya, sasa tuna maji ya kutosha, waje tuwaunganishe na maji haya japo baadhi yao wamekuwa wakijiunganishia maji kiholela na kutumia visima wanavyochimba ambavyo si salama".

Kuhusu Serikali kuhakikisha ulinzi wa mtandao wa bomba hilo lenye urefu wa Kilometa 56 amesema kuwa kazi hiyo inafanywa na DAWASCO ikiwahusisha viongozi na wananchi ambao mradi unapita katika maeneo yao.

" Ni kweli ulinzi wa bomba hili ni muhimu,DAWASA wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo linakopita bomba, pia tumeshaweka matoleo kwa ajili ya kuhakikisha tunawafikishia huduma ya maji wananchi wanaoishi kuzunguka bomba hili ili nao wawe sehemu ya walinzi wa mradi wao" Amesema.

Mhe. Lwenge ameongeza kuwa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) litaweka mfumo wa ulinzi wa kieletroniki ili kulinda bomba hilo, mfumo huo utakua unapima kiwango cha msukumo wa maji yanayotoka Ruvu Chini kisha kutoa taarifa kwenye vituo vitakavyoanzishwa endapo itatokea hitilafu ya miundombinu hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni Wabunge wakizungumzia kukamilika kwa mradi huo wamesema kuwa wameridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na serikali na kwamba itaondoa kero ya maji katika jiji la Dar es-slaam.

Mbunge wa jimbo la Itirima, Mhe. Njalu Silanga ambaye  ni mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo ameeleza kuwa ameridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kwa kuwa mradi huo umejengwa katika viwango vya hali ya juu na kuongeza kwamba wakazi wa Dar es salaam sasa watarajie kupata maji Safi na Salama.

"Naipongeza sana Serikali kwa kufanikisha mradi huu,kweli  wamefanya kazi kubwa sana, mimi na wabunge wenzangu tumeona na tumeridhishwa na utendaji wa Serikali katika kuhakikisha jiji la Dar es salaam linapata maji safi na salama"

Ameiomba Serikali kuweka msisitizo katika uimarishaji wa miundombinu ili kuwezesha maji kufika kwa urahisi katika makazi ya watu.

Naye Mhe. Dkt.Sware Semesi, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa ameridhishwa na miundombinu imara iliyojengwa na kuiomba serikali kusimamia usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

" Mimi pamoja na wabunge wenzagu tumeshuhudia mradi huu ni mkubwa,kilichobaki kwa mamlaka zinazohusika ni kujipanga na kuhakikisha kunakuwa na mgawanyo mzuri wa maji haya,kufanyika kwa Uhakiki na ukusanyanji wa ankara za wateja unaoendana na matumizi halisi ya maji hayo ili huduma hii iwe endelevu" Amesema.

Aidha, ametoa wito kwa DAWASCO kusimamia kikamilifu usambazaji wa lita milioni 270 zinazozalishwa kwa siku na mtambo wa Ruvu chini kwenda  matangi  ya maji yaliyoko Chuo Kikuu Ardhi

Source: Aron Msigwa - MAELEZO.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA MATUMIZI YA FEDHA MTAMBO WA RUVU CHINI.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA MATUMIZI YA FEDHA MTAMBO WA RUVU CHINI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgd4HJrhPUd8x5A8ySGD-2u2bl-29nTbi70qILckTQA_I_VY9qB8-Ozwm7qrKczYA4Ox9A2fw6EHKlZxOwutB3E27T0szEoHuzxhHzsWxxShk-JD-m2qGnkNrItG_fFHAPGUl-yhI-rUTA/s320/MAJI.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgd4HJrhPUd8x5A8ySGD-2u2bl-29nTbi70qILckTQA_I_VY9qB8-Ozwm7qrKczYA4Ox9A2fw6EHKlZxOwutB3E27T0szEoHuzxhHzsWxxShk-JD-m2qGnkNrItG_fFHAPGUl-yhI-rUTA/s72-c/MAJI.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/04/kamati-ya-kudumu-ya-bunge-ya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/04/kamati-ya-kudumu-ya-bunge-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy