Wananchi mkoani Kagera na watanzania wote kwa ujumla pamoja na wananchi wote katika nchi za Umoja Afrika Mashariki za Tanzania, Rwanda, ...
Wananchi mkoani Kagera na watanzania wote kwa ujumla pamoja na
wananchi wote katika nchi za Umoja Afrika Mashariki za Tanzania, Rwanda,
Uganda, Kenya, Burundi na Sudan kusini, wamehimizwa kutumia daraja la Rusumo
lililozinduliwa, ili kuudumisha amani, upendo, undugu kwa kutembeleana na
kubadilishana biashara.
Wito huo umetolewa na Mhe. John Pombe Magufuli tarehe 6.4.2016 wakati wa sherehe za kihistoria za uzinduzi wa daraja hilo jipya katika mto wa Kagera eneo la Rusumo.
Pamoja na uzinduzi wa daraja hilo la Kimataifa la Mto Rusumo katika Mpaka wa Tanzania na Rwanda.
, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame wamefungua Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post).
Mradi huu wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha utoaji wa Huduma za Mpakani cha Rusumo, umehusisha ujenzi wa majengo ya mamlaka ya Mapato katika pande zote mbili na daraja lenye urefu wa mita 80 na upana wa mita 9.5, na umegharimu shilingi Bilioni 61.4 zilizotolewa kwa ufadhili wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.
Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi wa mradi huo Rais Magufuli ameishukuru Japan kwa kutoa fedha za kuwezesha utekelezaji wa mradi huo na ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Rwanda kupitisha mizigo yao Tanzania kupitia mpaka huo, pamoja na kuitumia bandari ya Dar es salaam.
Dkt. Magufuli amewasihi wananchi wa Rwanda na wanajumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla, kushirikiana kibiashara kwa kutumia fursa zilizopo huku akibainisha kuwa Tanzania imeanza juhudi za kuimarisha miundombinu yake ya barabara na kujenga reli ya kati, ambayo tayari washirika 13 wameonesha nia ya kufanikisha ujenzi huo.
Rais Magufuli amewaonya maafisa forodha na vituo vya ukaguzi kuacha mara moja tabia ya ucheleweshaji wa upitishaji wa mizigo, na amesema serikali imeshaamua kuwa barabara ya Rusumo hadi Dar es salaam itakuwa na vituo vitatu ambavyo ni Rusahunga, Singida na Vigwaza ili magari yatumie muda wa siku 3 badala ya kutumia siku zaidi ya 10.
Kwa upande wake Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye ameongozana na mkewe Mama Janeth Kagame, pamoja na kuishukuru Japan kwa kufadhili mradi huo amesema Tanzania na Rwanda zina kila sababu ya kushirikiana kiuchumi na ameongeza kuwa ni matumaini yake kujengwa kituo hicho kutaongeza biashara na idadi ya watu wanaovuka daraja kutoka 2,000 wa sasa hadi watu zaidi ya 15,000 kwa siku.

Source: Joseph Sekiku
FADECO COMMUNITY RADIO
KARAGWE
FADECO COMMUNITY RADIO
KARAGWE
COMMENTS