Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’,

VIJANA zaidi ya 300 kutoka mkoa wa Dar es salaam wamepatiwa ujuzi muhimu katika kibiashara ili waweza kujiajiri na kuendesha maisha yao ya kila siku.
Mafunzo hayo yaliyowezeshwa na kampuni  ya simu ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa yalifanywa  kwenye ukumbi wa Urafiki Social Hall, Shekilango jijini Dar es Salaam.
Katika warsha hiyo, kijana Stephano Gimase ambaye alikuwa ni miongoni mwa vijana aliyeshiriki na kuelezea biashara yake alibahatika kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya biashara yake.
Vijana wengine waliohudhuria walionyesha shukrani kwa kampuni ya simu ya Airtel na kuahidi kutumia ujuzi waliopata katika warsha hiyo kwa manufaa yao wenyewe.
"Airtel imetambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na kutusaidia sisi vijana,” alizungumza Yvonne Obeth mmoja wa vijana waliohudhuria.
"Leo hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja zaidi. Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha yangu. "aliongeza Obeth
Meneja kwa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema program hiyo ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuunda fursa na kutengeza ajira kwa vijana.
“Kijana akiwa na ujuzi wa mambo mbali mbali ni faida kwake na ananafasi kubwa ya kutengeneza ajira yake na Jamii inayomzunguka. Tunahitaji kuwawezesha vijana na kubadili mawazo yao kutoka kutaka kuajiriwa  na kujiajiri wao wenyewe.” Alisema Bayumi.

Kwa upande wake  Stephano Gimase  ambaye ni miongoni mwa vijana watatu walioweza kuwezeshwa na Airtel Fursa katika warsha hiyo na kupatiwa vitendea kazi, aliwashukuru Airtel kwa kuboresha biashara yake.
Hadi sasa Airtel Fursa imeweza kufikia vijana zaidi  ya 3,600  hapa nchini kupitia mafunzo haya ya elimu ya ujasiriamali.
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO