Waeleze Mail group tumerudi tena !
Tunaomba radhi wateja wetu kwa kutorusha matangazo yetu kwa muda mrefu sasa.
Waeleze mail group inarudi tena kukusaidia wewe mteja kutuma tangazo lako au kupokea matangazo mbali mbali ya vitu vinavyotangazwa mkoa wa Kilimanjaro.

Dhumuni letu ni kurahisisha utafutaji, uuzaji na ununuzi wa chochote ndani ya mkoa wetu.
Muda sio mrefu tutawapa application yetu ambayo itakuwa inapatikana katika sumu za android na ios kwaajili ya kupata matangazo moja kwa moja kwenye application yako bila kuingia kwenye email.
Kwa sasa tuna email zaidi ya 1500 na matangazo yetu yanafikia watu wengi zaidi mkoa wa Kilimanjaro na nje ya hapa.

Kama una tangazo lolote tunaomba ulitume kwenda kwenye email yetu ya matangazo ambayo ni waeleze@gmail.com nasi tutalitengeneza tangazo lako bure na kulirusha kwa wateja wetu. Usisahau kuweka namba zako za simu.

kama hutopenda kupokea matangazo yetu tafadhali bonyeza kitufe cha reply kwenye email yako andika kwenye subject yako ONDOA basi nasi tutakutoa kwenye mail group yetu.
Kama unahitaji kumuongeza rafiki yako kwenye mail group yetu basi bonyeza reply na tutumie email yake nasi tutamuongeza.

Asanteni sana na karibuni tena kupokea huduma hii nzuri na ya bure.

Asanteni

Louis

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO