HUAWEI YAUNGANA NA LEICA KUTENGENEZA SIMU P9

H 3424 page 10 Na John Gagarini, Kibaha MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameitaka Halmashauri kudhibiti upotevu wa f...

H 3424 page 10 Na John Gagarini, Kibaha MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameitaka Halmashauri kudhibiti upotevu wa fedha sh bilioni 1.1 kwa mwaka kutokana makusanyo kuwa chini hivyo kushindwa kufikia malengo. Wakizungumza kwenye baraza la madiwani la halmashauri hiyo, baadhi ya madiwani walisema upo upotevu wa fedha nyingi na kwamba endapo mianya hiyo itazibwa itasaidia kudhibiti hali hiyo. Akizungumzia namna fedha hizo zinavyopotea, Diwani wa Kata ya Tumbi, Hemed Chanyika alisema madiwani walifanya utafiti kwenye vyanzo vya mapato na kugundua upungufu mkubwa katika ukusanyaji. Chanyika alisema mfano ni mapato ya ushuru wa mchanga ambako waligundua magari yanayoingia yanachukua mchanga kwa siku ni 103 . Alisema gari moja linalipia sh 3,000 kwa mwaka na mapato ni sh bilioni 1.1 ingawa makiso yaliyowekwa ni sh milioni 264.6 kwa mwaka huku kukiwa na tofauti ya sh milioni 900. Alisema kwa upande wa stendi ya Maili Moja makisio yalikuwa ni sh milioni 320 kwa mwaka ambapo magari yanayopita ni zaidi ya 500 kwa siku ambayo yanaingiza takribani sh milioni 564 kwa mwezi. Upotevu unakadiriwa kuwa sh milioni 183. Machinjio yalikadiriwa kukusanya sh milioni 25 na kufanya upotevu kuwa sh milioni 56. Kwa siku wanachinjwa ng’ombe 45 na ushuru ni sh 5,000 kwa mwaka 25. Mwenyekiti wa halmashauri, Leonard Mlowe alisema kuwa katika kuhakikisha makusanyo hayo yanafikia asilimia 100, atakuwa akikutana na watendaji wa serikali za mitaa na kata kujadili namna ya kukusanya mapato hayo. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji alisema suala hilo watalifanyia kazi kwa kulirudisha kamati ya fedha kwa ajili ya namna ya kudhibiti upotevu wa fedha hizo ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa. Na Fadhili Abdallah, Kigoma BAADHI ya wananchi wanaojishughulisha na uzalishaji wa asali kupitia mradi kuendeleza sekta ya nyuki, wameeleza kunufaika nao na kushuhudia mabadiliko ya kiuchumi waliyo nayo. Wakizungumza na gazeti hili wakati wa mkutano wa wadau uliotumika kutoa taarifa na tathmini ya utekelezaji wa mradi huo wa miaka minne, baadhi ya wananchi walisema wana mafanikio makubwa kiuchumi. Mkazi wa Nguruka kati wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Seifa Kabobo alisema baada ya kupata elimu na mbinu za uzalishaji wenye tija ameweza kuongeza uzalishaji na mauzo. Alisema amewaondoa watoto wake kwenye kazi za uzalishaji wajikite kwenye masomo kitendo ambacho kimewezesha watoto wake wawili kufaulu vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne. Kwa upande wake Sawia Damas mkazi wa kijiji cha Itumbiko wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma alisema mradi huo umemwezesha kuongeza thamani ya mazao hayo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ya kujipaka,mvinyo, sabuni za kuogea,mishumaa na dawa za ngozi. Alisema ametanua wigo wa biashara na kuifanya sekta ya nyuki kuwa na manufaa kiuchumi kwa wazalishaji. Sawia alisema amekarabati nyumba yake imekuwa bora na anaendelea kufanya shughuli nyingine za ujasiliamali kutokana na kipato kinachotokana na mazao ya nyuki . Mradi huo uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika lake la maendeleo (BTC) umefikia mwisho. Mratibu wa mradi huo kwa mkoa Kigoma, Nicodemus Mpemba alisema wanayo mafanikio makubwa katika miaka minne ya utekelezaji wa mradi huo. Mpemba alisema elimu iliyotolewa kwa wafugaji nyuki imesaidia wazalishaji wa asali kuboresha njia za uzalishaji,uchakati kuongeza thamani,mbinu za kutafuta masoko na kupanua miradi yao jambo ambalo limewezesha kusaidia kuongeza uzalishaji nyuki maradufu mkoani Kigoma. Mratibu wa mradi huo kwa wilaya za Kibondo na Kakonko, Seif Salum alisema miaka minne ya utekelezaji wa mradi huo wazalishaji wa asali wameongeza kutoka 2500 na kufikia zaidi ya 6000 ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani 100 hadi kufikia tani 400 kwa mwaka jambo ambalo pia linasaidia kuongeza kipato cha mzalishaji wa asali. Na Veronica Mheta, Arusha UCHELEWESHWAJI wa fedha za miradi pamoja na mchakato wa upitishaji wa fedha za manunuzi vimetajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye halmashauri mbalimbali nchini. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mussa Iyombe alisema hayo wakati akifungua kikao cha kujadili mapitio ya Mradi wa Uboreshaji Miji Tanzania (ULGSP) inayotekelezwa katika halmashauri zaidi ya 18 inayofadhiliwa na Benki ya Dunia . Iyombe alisema awali ucheleweshwaji huo ulikwamisha miradi mbalimbali katika halmashauri zinazofadhiliwa na benki ya dunia. Alisema awali mchakato wa manunuzi ulikuwa na hatua mbalimbali lakini kwa maboresho hayo ya serikali, itakuwa rahisi kwa halmashauri kuendesha miradi yao kwa kupitisha fedha kwa ridhaa ya madiwani zenye thamani ya kuanzia sh milioni 50 hadi sh milioni 900. "Awali wakurugenzi walipata tabu kusimamia miradi mbalimbali katika halmashauri zao sababu ya mchakato wa sheria za manunuzi lakini hivi sasa miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia itatekelezwa kwa wakati kutokana na serikali kurahisisha mchakato huu wa manunuzi, " alisema. Aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuleta maendeleo kwa wananchi pamoja na kuainisha vipaumbele vya miradi ya maendeleoi kutatua changamoto zilizokuwa zikiwasumbua wananchi kwenye halmashauri zao. Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Marx Kamaoni aliishukuru serikali kwa kuwezesha kuiboresha sheria hiyo ya manunuzi. Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Jenifa Omolo alisema ULGSP umeleta maendeleo kwa manispaa hiyo kwani umewezesha ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa inayotarajia kuzinduliwa mwezi huu. Mhandisi wa mradi huo wa ULGSP, Gilbert Mfinanga alisema ulianza mwaka 2013 na unatarajia kuisha 2018 na utqgharimu dola za kimarekani milioni 255. Washiriki wa mkutano huo ni wakurugenzi, wahandisi, wachumi, maofisa mazingira, maofisa maendeleo ya jamii na watunza hazina wa halmashauri 18. Pia unahudhuriwa na ujumbe kutoka Uganda ukiongozwa na Waziri wa Nchi, Maendeleo ya Miji, Rosemary Najemba. Na Mwandishi Wetu BENKI ya FNB imepanua wigo kitaifa kwa kufungua tawi jipya jijini Mwanza. Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa tawi hilo katika eneo la Rock City Mall, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois Botha alisema uzinduzi umelenga kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo. “Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.” Botha alisema tawi la Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mtandao wa matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini. “ First National Bank (FNB) daima tunafikiri njia mbalimbali za ambazo tunaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Mwanza litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani yenye biashara inayokua kwa kasi,” alisema Botha. Aliongeza kusema; “Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi.” Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema mkoa wake una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza inakua kwa kasi. "Tunakaribisha uwepo wa FNB na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na mikoa mengine," alisema Mongela. Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri mkubwa wa rasilimali. Tawi hilo lililofunguliwa kwenye jengo jipya la Rock City Mall litatoa huduma za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo. Ends

Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.
                                                      
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
29 Aprili 2016
Dar es Salaam
Mkakati wa Huawei katika kubadili namna uonavyo dunia iliyokuzunguka

Mwezi Aprili, Huawei wamezindua simu iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu katika mlolongo wao wa simu zao za P Series; Huawei P9. Uzinduzi wa Huawei P9 umezingatia kipaumbele cha teknolojia ya hali ya juu. Toleo hili la tisa la P Series limewezeshwa na Kampuni ya Huawei pamoja na kampuni mashuhuri kwa utengenezaji wa camera duniani Leica. Simu hii ina kamera ya kipekee yenye lenzi mbili, ambayo imeweka rekodi katika teknolojia ya kamera za simu za kisasa, ikiwa na mwanga Zaidi na ubora Zaidi, kupata picha zenye rangi nzuri Zaidi katika staili ya Leica ya kipekee.

Watanzania wanategemea kupata simu hii yenye teknolojia ya hali ya juu na ya kipekee katika kamera hivi karibuni. Hii inafuatia uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika mji wa Dubai wiki hii. Uzinduzi huo wa kipekee ambao ulihudhuriwa na viongozi wa Huawei Tanzania na Waandishi wa Habari umeashiria upatikanaji wa simu hii katika soko la Tanzania hivi karibuni.
Tokea uzinduzi wake mji wa London, simu hiyo imepata mapokezi makubwa kama simu “inayobadili namna uonavyo dunia”. Simu mpya ya kipekee Huawei P9 ina malengo kubadili ubora wa picha unaopatikana katika timu za kisasa maarufu kama “smartphone”. Teknolojia katika simu hiyo inabadili namna tunavyopiga na kufurahia picha, hii imetokana na shauku ya Huawei kuendelea kuvuka mipaka ya uvumbuzi, ikilinganishwa na uzoefu na kipaji katika utengenezaji wa kamera na lenzi wa Leica pamoja na ushirikiano mzuri katika kutengeneza P9.
Waliokuwepo katika uzinduzi huo ni pamoja na viongozi wakuu wa Huawei Tanzania akiwemo Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania, Lydia Wangari Meneja Masoko kampuni ya Huawei Tanzania, waandishi wa Habari na wadau mbalimbali kutoka Tanzania.
Akionglea ujio wa simu hiyo katika soko la Tanzania Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania alisema ”Tunategemea kuleta simu mpya ya Huawei P9 kwa wateja wetu wa Tanzania hivi karibuni; Tunaamini teknolojia hii ya hali ya juu na ya kipekee iliyotokana na utafiti wa hali ya juu na shauku ya kubadili namna watumiaji wetu waonavyo dunia inayo wazunguka, P9 ikifanya kazi na Leica, tumeweza kufanya maajabu katika teknolojia ya lenzi ya kamera”.
Akiongea katika uzinduzi huo, Lydia Wangari Meneja Masoko Huawei Tanzania alisema, ”Tunaendelea kuzindua simu mpya , tukitilia mkazo katika teknolojia ya kipekee. Kwa kushirikiana na wadau wengine, tumeweza kujumuisha utamaduni, mtindo ya maisha ya wateja wetu na teknolojia ili kuwapatia wateja watu simu bora zaidi”.
Kuongezeka kwa aina mbalimbali za simu za mkononi za smartphone nchini Tanzania inaashiria ukuaji na umuhimu wa Tanzania katika soko duniani huku wa Tanzania Zaidi wakigundua umuhimu wa teknolojia maishani mwao. Mahitaji katika maendeleo na simu za  kiteknolojia yanaongezeka kila kukicha nchini Tanzania na kampuni ya Huawei imeendelea kutatua hitaji hilo nchini Tanzania.
Kufuatia mafanikio ya simu aina ya P zijulikanalo kama “P Series”, kwa ujumla mapokezi ya simu ya Huawei P9 ni mazuri duniani kote. Huawei Tanzania wana matarajio makubwa juu ya ufanyaji kazi wake katika soko la Tanzania. Wakiahidi watumiaji simu yenye nguvu na ubora wa kipekee usio linganishwa, simu mpya ya P9 itapatikana katika rangi nne: Dhahabu, kijivu, Dhahabu iliyoiva Zaidi na Siliva huku P9 Deluxe Version ikipatikana katika rangi ya dhahabu na Nyeupe.
Familia ya simu za Huawei P9  imetumia njia za kipekee na ubora wa hali ya juu kubadili namna tunavyoona dunia iliyotuzunguka. Inaendeleza heshima ya Huawei ya simu zenye ubora wa juu ambazo zimeacha alama katika soko kwa ubora na ufanisi.
Huawei itaendelea kukamata fursa mbalimbali ili kubadili soko na kuinuka duniani katika biashara za watumiaji wa simu za mkononi. Huku simu za kampuni hiyo zikizidi kua na teknolojia ya hali ya juu, Huawei itaendelea kutengeneza vifaa vinavyoweza tumika na mteja wakati wowote na mahali popote. Na Wataendelea kuungana na wadau wengine katika soko la vifaa, programu. Kupitia uvumbuzi wa teknolojia pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali, kampuni ya Huawei ina ahidi kuleta vifaa Zaidi kwa wateja wake wote duniani.

Kuhusu Huawei
Huawei ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500. Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.
Kampuni ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.
Huawei imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Kupata habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com



COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4811,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: HUAWEI YAUNGANA NA LEICA KUTENGENEZA SIMU P9
HUAWEI YAUNGANA NA LEICA KUTENGENEZA SIMU P9
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCI4nCV4uf-JU4mi3y8Hulb4bqhyoHb5jpM4x0JFxlte4cEjJ9AtojXKfvAb1a7lUDJWxUl8pJ4QoNYsLNG3GhkQcgA9TX7ePgLehu9QjGaOv3ZoFjrPzKOfGrTSR2iwSnH0FQkkzkrOQ/s640/P9+-+All.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCI4nCV4uf-JU4mi3y8Hulb4bqhyoHb5jpM4x0JFxlte4cEjJ9AtojXKfvAb1a7lUDJWxUl8pJ4QoNYsLNG3GhkQcgA9TX7ePgLehu9QjGaOv3ZoFjrPzKOfGrTSR2iwSnH0FQkkzkrOQ/s72-c/P9+-+All.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/05/huawei-yaungana-na-leica-kutengeneza.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/05/huawei-yaungana-na-leica-kutengeneza.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy