Wakati  mapambano ya kupinga ukatili kwa watoto yanapamba moto, babu  mmoja mwenye umri wa miaka 65  ambaye amekamatwa  kwa tuhuma za kungonoana na binti wa miaka 11 na kumfanya mtumwa wake wa ngono, amesema kwamba binti huyo ndiye aliyekwenda eneo lake la kazi na kumshawishi kufanya vitendo hivyo.
Mzee huyu anayetambuliwa kwa jina la  Akinlolu Ogunlade, pichani, alisema, binti huyo mdogo sawa na mjukuu wake alimshinikiza kufanya ngono naye hata alipomnwambia kwamba yeye hajui  na wala hawezi.
“ Mimi nina miaka 65 ni fundi bomba binti huyo mdogo alifika eneo langu la kazi na kunilazimisha kufanya naye mapenzi. Nilimwambia kwamba yeye ni mdogo. Akasema ananimudu. Nikamwambia tena hawezi kufanya mambo hayo na mimi akasisitiza kwamba anaweza. Baadae nikamkubalia nikafanya mapenzi naye mara mbili na  nikakaa naye kwa siku 4 tu” alisema Ogunlade wakati akihojiwa na Vanguard.
Babu huyo ambaye mkewe amefariki dunia na ana mtoto mmoja alisema hayo wakati alipofikishwa kituo cha polisi chajimbo la Oyo Juni 10 mwaka huu.
Akizungumza kuhusu kukamatwa kwake kwa babu huyo kamishina wa polisi Leye Oyebade alisema kwamba walifanikiwa kumkamata mzee huyo kutokana na taarifa  walizokuwa wamepata.
Alisema kwamba binti huyo Bisi ( jina la pili limefichwa) mwenye umri wa miaka 11 aliondoka nyumbani kwao Mei 27 saa mbili usiku kwenda kanisani kwa maombi  huko Abidi=Odan, Akobo, Ibadan lakini hakurejea nyumbani siku ya Jumamosi na juhudi zote za kumtafuta zilishindikana.
Hata hivyo Mei 30 wapelelezi wa polisi kwa kuzingatia taarifa walizokuwa nazo waliweza kumfuatilia binti huyo na kumkuta nyumbani kwa babu huyo.
Source:Vanguard

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO