TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                

Dar es Salaam unakuwa mji wa 475 kujiunga na mtandao unaokua wa Uber duniani ambao huwaunganisha madereva na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka na marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber hutoa njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.
Meneja wa Uber Kusini mwa Sahara, Alon Lits anasema:“Tunajivunia kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao uchumi wake unakua. Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya viwanda, hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa kuaminika.”
Akaongeza, “Tumeweka viwango vya kuunganisha watu katika usafiri wenye kiwango cha juu duniani, kusafirisha mamilioni ya watu duniani kote kila siku kupitia huduma zetu za usafiri  nafuu na za kuaminika kwa kubonyeza kitufe tu. Huduma zetu zinaenda sambamba na aina za usafiri uliopo, hivyo wote tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza foleni barabarani na kuboresha mazingira ya usafiri katika jiji.  
Kwanini Uber?
Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu kitufe-hakuna kusubiri barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa ajili kutafuta basi. Ni njia bora na karibu zaidi kupata usafiri salama, nafuu na wa kuaminika. 
Kabla ya kuingia ndani ya gari
 • Hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku.   
 • Safari hazina kificho. Mara dereva anapokubali ombia lako, unaona jina lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana na dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna mkanganyiko wowote kuhusu muda wa kukuchukua.  
Wakati wa Safari
 • Julisha mahali ulipo. Unaweza kuwajulisha ndugu na marafiki zako kwa furaha zaidi juu ya mipango ya safari yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na mahali ulipo, na muda unaotarajia kuwasili. Watapokea linki ambapo wataweza kuona muda kamili, jina na picha ya dereva, gari lake na mahali ulipo katika ramani hadi utakapowasili na wanaweza kufanya haya yote bila haja ya kupakua App ya Uber wao wenyewe.  
Baada ya Safari
 • Fanya mrejesho na toa alama kila baada ya safari.  Baada ya kila safari, wewe na dereva wako mnahitaji kupeana alama na kufanya mrejesho. Timu yetu ya usalama hupitia taarifa hizi na kufanya uchunguzi juu ya kila jambo.
 • Msaada masaa 24 kwa wiki. Endapo jambo litatokea ndani ya gari, kama ni ajali ya barabarani au kutoelewana kati yako na dereva, mfanyakazi wetu wa huduma kwa wateja yupo tayari kukusaidia kwa suala lolote masaa 24 kwa wiki.
 • Msaada wa Haraka. Tuna timu mahiri inayoshughulika na matukio kujibu suala lolote linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Tukipokea taarifa kuwa dereva au abiria amesababisha tukio la hatari au hayupo njia sahihi, tunafunga akaunti zao na kumzuia asiweze tena kuingia katika jukwaa la Uber wakati tukifanya uchunguzi.  
Nyuma ya Pazia
 • Muda wote kwenye ramani. Kukubali kuwajibika ni moja ya mambo yanayofanya wasafiri kujisikia wako salama ndani ya Uber. Tunatumia teknolojia ya mawasiliano ya GPS kuweka taarifa za mahali madereva wanakotakiwa kwenda wakati wa safari, ili kutuwezesha kuthibitisha njia zinazotumika ni bora, kitu kichanachojenga uwajibikaji na ushawishi mkubwa kwa utendaji mzuri.
 • Utendaji na mamlaka za sheria. Endapo mamlaka za kisheria zinatupa taratibu za kisheria, tunatafanya kazi kutafuta vielelezo, mfano kwa kutoa taarifa za safari. Hata hivyo uwazi na uwajibikaji upo katikati ya mafanikio ya Uber.       
 • Upimwaji wa madereva. Madereva wote lazma awapitie mchakato wa upimwaji kabla ya kuanza kutumia App ya Uber. 
Alon Lits aliongeza:
“Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria. Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”
Uber inasherehekea uzinduzi mjini Dar es Salaam kwa kutoa huduma ya bure ya usafiri. Tanzania wanaweza kujaribu huduma mpya kwa kupata huduma ya bure kwa kuingia kwenye App ya Uber. . 
MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure)
 • Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni MoveTanzania ili upokee usafiri wa bure
 • Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6 mchana mpaka Jumapili Juni 19 katikati ya usiku.
 • Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na kila safari isizidi kiasi cha shs 12,000
 • Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na kuishia maeneo ya Dar es Salaam yaliyopangwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO