Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Brazil, Dunga ametimuliwa kazi.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya timu ya nchi hiyo kuchapwa moja bila na Peru katika mechi ya Jumapili iliyopita na kuondolewa katika michuano ya Copa America.
Dunga, ambaye alikuwa nahodha katika timu ya taifa iliyofanya vyema katika michuano ya dunia 1994 alitajwa kwa mara ya pili kuwa kocha wa timu ya taifa mwaka 2014.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa kikosi cha Brazil kutolewa mapema katika michuano hiyo toka mwaka 1987.
Dunga, 52, alitwaa mara ya kwanza nafasi ya ukocha  kuanzia mwaka 2006 hadi 2010 na kufanikiw akutwaa kombe la Copa America 2007.
Kocha wa Corinthians, Tite  anaonekana ndiye atakayerithi mikoba ya Dunga.
Kocha huyo mwenye miaka 55 aliiwezesha klabu yake kutwaa ubingwa wa Serie A mwaka  2011 na 2015,  kombe la Copa Libertadores  na Kombe la dunia kwa fasi ya vilabu mwaka 2012.
Yeyote atakeyapata nafasi ya Dunga atakuwa na kibarua cha kusuka timu ya under-23, akiwamo  mshambuliaji wa Barcelona, Neymar katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika Agosti mjini Rio de Janeiro.
Kocha mpoya pia atakuwa na kibarua kigumu cha kuisuka timu ya taifa ambayo imeanza kw akusuasua katika kuwania kukwolifai kombe la dunia 2018 nchini Russia, kwa kuwa na nafasi ya sita katika nchi za Amerika ya Kusini.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO