Masikhara hayo, ni kama vile anasema mkuu wa Mkoa wa Lindi , Godfrey Zambi kuhusiana na kuendelea kutumika kwa vyoo vya muda ambavyo havikidhi kiwango. Choo hicho cha muda Shule ya Msingi Ng’au kilitengenezwa baada ya kubomoka kwa choo kilichokuwepo awali.
Baada ya kufanya ukaguzi Mkuu wa Mkoa alitoa maelekezo yafuatayo:
-          Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wahakikishe Kamati ya Shule hiyo inakutana ndani ya wiki hii ili wafanye makubaliano ya haraka  ili vyoo vimalizike kwa wakati.
-          Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ahakikishe anamsimamia fundi vizuri ili hatua ya umaliziaji wa ujenzi iwe yenye kukidhi vigezo na Thamani ya Pesa Iliyotumika.
-          Halmashauri ianze kupanga katika bajeti zake mipango ya kuboresha miundombinu ya shule zote za zamani.
-          Mkuu wa Mkoa  Lindi Godfrey  Zambi amefanya ziara ya siku moja Wilayani Ruangwa ambapo amekagua miradi  mbalimbali Ikiwemo ya  ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Mnacho pamoja na Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nandagala,Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi na  Kakutana na Walengwa wa Mradi wa Kaya Maskini chini ya ufadhili wa TASAF III katika Kijiji cha Mitope na  Baadae Kuhutubia Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani wa Ruangwa ili kujadili Hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Mkuu wa Mkoa wa Lindi akitoa maelekezo baada ya kufanya ukaguzi kwenye mradi wa Ujenzi wa vyoo Shule ya Msingi Ng’au katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi

Moja ya majengo ya zamani ya  madarasa katika Shule ya Msingi Ng’au

Jengo la Zahanati linalojengwa katika Kijiji cha Nandagala Wilayani Ruangwa. Mradi huu unajengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Huawei Tanzania unajumuisha ujenzi wa Kichomea taka, Vyoo, Mfumo wa Kuvuna maji ya mvua, na nyumba moja ya mtumishi. Una thamani ya Sh. 118,000,000/=

Mkuu wa Mkoa wa Lindi akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nandagala unaoendelea ambapo kwa sasa upo kwenye hatua ya upauaji

Moja ya maeneo ya ndani ya Zahanati ya Nandagala.

Mkuu wa Mkoa akiondoka kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nandagala baada ya kufanya ukaguzi.

Mratibu wa TASAF Bi Mwajuma akisoma  taarifa ya Walengwa wa Kaya Maskini chini ya ufadhili wa TASAF III katika Kijiji cha Mitope Ruangwa

Baadhi ya Walengwa wa Kaya Maskini chini ya ufadhili wa TASAF III katika Kijiji cha Mitope

Baadhi ya Walengwa wa Mradi wa Kaya Maskini chini ya ufadhili wa TASAF III katika Kijiji cha Mitope
Katika Mkutano Huo,Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi  amewataka  Walengwa wa Mradi huo kuhakikisha wanatumia Malipo wanayolipwa na TASAF  kujiwezesha kwa kuwa na miradi itakayowezesha kujikwamua. Pia amemwagiza Mratibu wa TASAF kuwafuatilia na kuwasimamia walengwa ili wazitumie fedha kwa malengo husika na sio kwa kunywea pombe.
Vilevile watendaji wa Kata na Vijiji wameagizwa kuhakikisha walengwa wa mradi wawe ni wale wanaotakiwa na si vinginevyo kwani kumekuwepo na malalamiko la watu wenye uwezo kuingizwa kwenye malipo Huku masikini wakiachwa
  Aidha, walengwa wameshauriwa  pia kujiunga katika vikundi ili waweze hata kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kuweza kukopeshana.
Mwisho Mkuu wa Mkoa aliwapongeza Walengwa wa Mradi kwa TASAF kwani wapo ambao wamefanikiwa kununua mabati, kujenga vyoo, na kununua mifugo kama  kuku na bata.

Ukaguzi wa Vyoo vinavyojengwa kupitia mpango wa WASH kwa kushirikiana na Halmashauri na Serikali ya Kijiji cha Ng’au uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi (hayupo pichani) pamoja na wataalam wa Sekriterieti ya Mkoa wa Lindi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO