JESHI la Polisi mkoani Tanga limewahakikishia wananchi kwamba eneo la Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto yanayodaiwa kutumiwa na wahalifu ambao walisababisha mauaji hasa ya wakazi nane wa Kibatini lipo salama baada ya kuwakamata watuhumiwa  watatu pamoja na silaha mbalimbali.

Silaha zilizokamatwa ni Bunduki 2 aina ya SMG,  Bastola moja, Risasi 30, Mapanga, Majambia ambavyo vimepatikana kupitia msako maalum ulioshirikisha Kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama ambacho kimehusisha baadhi ya askari kutoka majeshi yote.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paulo amebainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake jana kwamba kiongozi mkubwa wa kundi la wahalifu hao aitwae Abuu Seif ambaye pia ni miongoni mwa majambazi walihusika kuwachinja baadhi ya wakazi hao wa Kibatini amekamatwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO