Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika mafunzo hayo.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano  ya elimu ya kukabiliana na majanga hasa yanayosababishwa na tsunami.

Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo washiriki watajenga uelewa mkubwa kuhusu Tsunami na namna ya kupunguza athari zake kwa jamii .

Aidha alisema washiriki hao watakuwa mabalozi wazuri wa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.

"Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami ya Japan iliua zaidi ya watu 20,000 kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami inakuwa na madhara hata kama imetokea mbali na hapa tulipo," alisema Bi. Rodrigues.


 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito Kodijat akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo ambayo watapatiwa.

Mkuu wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini (TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.

Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu washiriki ya kuhusu Tsunami.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja. ( Habari na Picha na Rabi Hume, MO Blog)

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami ya mwaka 2004 ambayo ilitokea mbali ndani ya  bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano.

"Mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali," alisema Dk. Chamuriho.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO