BABU Durga Kami amekuwa ni mwanafunzi mzee kuhudhuria darasa la msingi akiwa na umri wa miaka 68 nchini Nepal.
Babu huyo ameamua kukamilisha elimu yake ambayo hakuipata akiwa mtoto kutokana na umaskini.
Mzee Kami amepania kumaliza shule yake ili awe Mwalimu kama alivyokusudia alipokuwa kijana.
Mzee huyu hutembea kiasi cha  saa moja kila siku kwenda shule akisaidiwa na mkongojo wake.
Kwa sasa akiwa gredi 10 kwa mfumo wa elimu wa Nepal anasoma na vijana wa miaka 14 na 15.
Mmoja wa walimu anasema kwamba hii ni mara yake ya kwanza kumfunz amtu mwenye umri mkubwa sawa na baba yake.
Kami ni baba wa watoto sita na babu kwa wajukuu wanane.
Wanafunzi wenzake huwa hawamwiti kwa jina lake na bada la yake wanamuita Baa yaani baba kwa Kinepali.
Akizungumza mzee Kami anasema kwamba ili asahau huzuni zake huenda shule na ametaka kuepuka maisha ya upweke baada ya mke wake kufa.
Amesema kwamba nyakati za usiku  husoma kwa kutumia tochi.
Aidha akiwa shuleni pamoja na umri wake mkubwa hushiriki matukio yote ya shule pamoja na kucheza mpira wa wavu.
Anasema anataka kusoma mpaka kifo kimchukue na  anaamini itasaidia wengine kuona kwamba umri si kitu katika kutafuta elimu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO