Polisi wa India wamewatia mbaroni simba 18 kwa tuhuma za kuua watu watatu katika jimbo la Gujarat.
Watuhumiwa wote hao wanatarajia kutwaliwa vipimo vya wayo zao na kinyesi chao kuchunguzwa kujua ni simba gani kati ya  hao 18 ndio wauaji.
Wapelelezi pia wanajifunza tabia za wanyama hao kuwa na uhakika.
Mtaalamu wa wanyamapori Ruchi Dave  ameiambia BBC kwamba simba wanaokula binadamu kwa kawaida huwa wakorofi wanapomuona mtu.
Imeelezwa kuwa watakaobainika kuwafanya  mauaji hayo watapelekwa katika bustani ya wanyama na  waliobaki kurejeshwa msituni.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO