Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu  na mwenyekiti mpya wa  Bodi ya
 Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Juni, 2016

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge Mstaafu  na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Spika wa Bunge Mstaafu  na mwenyekiti mpya wa  Bodi ya
 Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO