Unganishwa na simu za "bure na halisi  kutoka Airtel"


KAMPUNI ya simu ya Airtel imetangaza ofa  kwa watu wanaohitaji simu orijino ili kuendana na matakwa ya serikali ya wananchi wake kutumia simu zinazokubalika kiafya na zenye ufanisi mkubwa.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana, kampuni hiyo imesema kwamba kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo Juni 16, 2016, Airtel Tanzania imeanzisha ofa  ya kununua kifurushi chenye dhamani  ya sh. 22,000  ili kupata simu ya bure.
"  Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa  na Airtel ikiwemo  ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika  550  kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne." imesema taarifa hiyo. 
Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha  Intaneti Gaurav Dhingra alisema: "tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu  bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika siku ya Alhamisi, Juni 16."
Alifafanua kwamba ili kuwasaidia wateja kuweza  kununua simu zenye kiwango kinachokubalika, wameamua kutoa simu zenye uhalisi katika gharama nafuu kabisa  zenye vifurushi  vitakavyoduma kwa muda wa miezi minne.  
Aidha alisema wana pia simu za smartphone kama vile Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3  ambapo mteja atapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000.
Alisema mteja wa Airtel mwenye simu iliyo bandia anatakiwa kufika kwenye duka lolote la Airtel na simu yake ili aweze kununua simu yenye kiwango kinachokubalika.  
Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO