Kampuni ya kijerumani ya Volkswageni itakohoa dola za Marekani bilioni 14.7 kumaliza kashifa ya udanganyifu iliyofanya katika magari yake kuhusiana na utunzaji wa mazingira.
Fedha hizo ni kwa soko la Marekani.
Habari zinasema  kwamba makubaliano ni moja ya makubaliano makubwa ya aina yake yaliyofanywa na  walaji dhidi ya wadanganyifu ndani ya soko.
Fedha hizo zitaguswa pia na serikali na wanasheria wa wamiliki wa magari 475,000 ya aina ya Volkswagen.
Aidha dola za Marekani  bilioni 10.03 zitahusika na kununua magari hayo yaliyohusishwa na kashifa hiyo kwa bei kabla ya kuibuka kw akashifa na fedha nyingine zitatolewa kama fidia kwa wenye magari.
Fedha atakazopewa kila mmoja wa wamiliki wa magari hayo zinaanzia kuanzia dola za Marekai 5,100  hadi 10,000. Imeelezwa kuwa fedha za kuyanunua tena magari hayo na zile za ziada zitategemea thamani ya magari hayo kabla ya kampuni hiyo kuikiri hadharani kwamba iliendesha udanganyifu katika mfumo wa kupumua wa magari hayo.
 Septemba mwaka jana kampuni hiyo ilikiri kwamba kile kinachotakiwa kuwa kisafisha injini za dizeli kimewekwa pale makusudi ili kutoa tarifa za uwongo kwa wanaopima kiwango cha moshi kinachotolewa na magari hayo na kama  unakubaliana na viwango vlivyowekwa vya ulinzi wa mazingira.
Pamoja na  ukweli huo imeelezwa kuwa soko la Marekani ni dogo sana kulinganisha na magari milioni 11 yaliyosambaa sehemu mbalimbali duniani mbayo Volkswagen yenyewe imekiri kuweka program ya udanganyifu katika magari hayo.
ampuni ya kijerumani ya Volkswageni itakohoa dola za Marekani bilioni 14.7 kumaliza kashifa ya udanganyifu iliyofanya katika magari yake kuhusiana na utunzaji wa mazingira.

Fedha hizo ni kwa soko la Marekani.
Habari zinasema  kwamba makubaliano ni moja ya makubaliano makubwa ya aina yake yaliyofanywa na  walaji dhidi ya wadanganyifu ndani ya soko.
Fedha hizo zitaguswa pia na serikali na wanasheria wa wamiliki wa magari 475,000 ya aina ya Volkswagen.
Aidha dola za Marekani  bilioni 10.03 zitahusika na kununua magari hayo yaliyohusishwa na kashifa hiyo kwa bei kabla ya kuibuka kw akashifa na fedha nyingine zitatolewa kama fidia kwa wenye magari.
Fedha atakazopewa kila mmoja wa wamiliki wa magari hayo zinaanzia kuanzia dola za Marekai 5,100  hadi 10,000. Imeelezwa kuwa fedha za kuyanunua tena magari hayo na zile za ziada zitategemea thamani ya magari hayo kabla ya kampuni hiyo kuikiri hadharani kwamba iliendesha udanganyifu katika mfumo wa kupumua wa magari hayo.
 Septemba mwaka jana kampuni hiyo ilikiri kwamba kile kinachotakiwa kuwa kisafisha injini za dizeli kimewekwa pale makusudi ili kutoa tarifa za uwongo kwa wanaopima kiwango cha moshi kinachotolewa na magari hayo na kama  unakubaliana na viwango vlivyowekwa vya ulinzi wa mazingira.
Pamoja na  ukweli huo imeelezwa kuwa soko la Marekani ni dogo sana kulinganisha na magari milioni 11 yaliyosambaa sehemu mbalimbali duniani mbayo Volkswagen yenyewe imekiri kuweka program ya udanganyifu katika magari hayo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO