SERIKALI imesema haijawafunga  midomo wabunge wa upinzani au mbunge yoyote labda awe amejifunga mwenyewe.
Hayo yamesemwa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumzia sintofahamu iliyojitokeza katika kipindi cha bunge ambapo wabunge wa upinzani walikuwa hawakati bungeni.
Akihutubia  kuahirisha bunge leo alisema kwamba wabunge wa upinzani  kwa makusudi wamekuwa wakijaribu kujenga taswira potofu kwa wananchi na nje ya nchi ili ionekane kwamba kuna kuminywa kwa demokrasia.
Alisema pamoja na juhudi hizo wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wamebaini kuwa upinzani bado haujakomaa kisiasa.
Alisema si jambo la kawaida kwa mbunge kuzitoa hoja za Bungeni na kuzipeleka mitaani eti zijadiliwe na wananchi kisha zitolewe uamuzi.
waziri mkuu alisema kwamba kama hilo linawezekana basi kusingekuwa na umuhimu wa kuwa na bunge na hivyo kuwataka wabunge hao kufikiria tena uamuzi wao na kurejea Bungeni.
Alisema ibara ya 100 na 101 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imetoa haki na kinga kwa wabunge ili waweze kujadili na kuhoji utendaji wa serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushtakiwa wanapotimiza wajibu wao huo wakiwa bungeni.
"Kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa wamamci yoyote yule nchini na kw amaneno mengine mbunge hajafungwa modomo labda aamue kujifunga mdomo mwenyewe" alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema kwa mantiki hiyo, kitendo cha baadhi ya wabunge kususa vikao vya bunge hakitoi picha nzuri kwa wananchi waliowachagua kuwasilisha matatizo yao katika bunge.
Aliwataka wabunge hao kurejea bungeni na kushiriki kutoa ushauri kwa serikali Bungeni ambao utalitea taifa maendeleo.
Alisisitiza kuwa Bunge linaongozwa na katiba, sheria na kanuni za kudumu za Bunge na kusema kwamba ni vyema zikafuatwa ili kuondoa manung'uniko yasiyo ya lazima.
"Endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya Bunge letu, zipo taratibu tulizojiwekea na kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo. kwa kususa kuingia Bungeni kunaweza kusiwe tija kwa tunawawakilisha na taifa letu" alisema.
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO