Mkao unaosaidia mwili kuwa imara au kama unavyojulikana "Tadasana". Kutoka kushoto ni Waziri Nape, Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda.


 Umbo lapembe tatu au Trikonasana.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faida za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa, kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njiaya kupumua. Hali kadhalika unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Waziri Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya Yoga Duniani kwenye ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)

 Yoga ikiendelea, kutoka kulia kwenda kushoto, ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kalaghe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Balozi wa India nchiniTanzania Sandeep Arya, na Balozi Mbelwa Kairuki.

 Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati).


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO