SERIKALI ya Zambia imewataka wenye vyombo vya moto wote ambao wamebadili namba za vyombo vyao na kuweka majina ya wagombea katika uchaguzi ujao waondoe majina hayo na kurejesha namba zao za awali.
Agizo hilo linatakiwa kutekelezwa mara moja.
Zipo habari kwamba kuna zaidi ya gari  20 katika jimbo la  Copperbelt pekee zenye namba moja ya, ECL 2016. 
 Waziri wa mambo ya ndani ya Zambia Panji Kaunda  amesema kuweka majina ya wagombea hao ni kosa la jinai.
Kumezuka mtindo hapa nchini watu kuweka namba za wagombea wanaowapenda, wakitumia majina yao.
Kanali Kaunda ameonya kwamba yoyote atakayebambwa na namba hizo atachukuliwa hatua kali na chombo chake kukamatwa.
Kanali Panji  amesema kwamba kiusalama ni mbaya kuweka namba hizo za majina ya wagombea.
Alifafanua kwamba itakuwa ngumu sana kwa vyombo vya usalama kutambua kama chombo hicho ni cha chama husika au ni cha mhalifu.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO