mtaalamu wa  ikolojia ya bakteria kutoka chuo kikuu cha Brighton  Profesa Huw Taylor
WATU bilioni 3.9 duniani watakuwa na tatizo kubwa la maji ifikapo mwaka 2050 na hivyo kusababisha uwezekano wa kusambaa kwa magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya majitaka.
Hayo yalielezwa na mtaalamu wa  ikolojia ya bakteria kutoka chuo kikuu cha Brighton  Profesa Huw Taylor wakati akizungumzia mradi wa Unesco wa kuweka mfumo mpya wa udhibiti  na menejimenti ya majitaka (GWPP).
Alisema kutokana na ukweli huo kwa sasa UNESCO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Michigan kinatafuta na kueleza kwa wadau wake suala la maji  na namna ya kuhakikisha kwamba kila mtu anakuwa na mji ya kutosha na salama.
Profesa Huw alisema kwamba mpango wa dunia wa maendeleo endelevu hauwezi kufanikiwa kama tishio la majitaka litaendelea kuwapo na lazima binadamu  aendelee kujipanga kuhakikisha kwamba anatawala mazingira ya maji na ana mfumo bora wa udhibiti wa majitaka na madhara yake.
Umoja wa Mataifa kupitia shirika lale la Sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) mwishoni mwa wiki (juzi) jijini dare s salaam liliendesha kongamano kubwa la aina yake lililoshirikisha wataalamu takribani 100 kutoka Nyanja mbalimbali kuzungumzia mradi wake huo wa GWPP.
Kongamano hilo ambalo lilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na umwagiliaji  Mbogo Futakamba ambaye hotuba yake ilisomwa kwa niaba na Mkurugenzi msaidizi katika wizara hiyo Dk George Lugomelo limelenga kujadili kwa kina matatizo ya bakteria wanaosababisha magonjwa katika maji  na madhara yake.
Akihutubia katibu mkuu huyo aliwataka wataalamu kuhakikisha kwamba wanaelewa dhana nzima ya GWPP, kuisaidia na kuhakikisha kwamba inapata majibu sahihi ili kuiwezesha kuwa na mfumo unaoeleweka wa udhibiti wa maji machafu na menejimenti yake.
Mradi huo wa Unesco ambao unajulikana  kama Global Water pathogen Project (GWPP).utamalizika mwaka wa kesho kw akutengenezwa kitabu ambacho kitakuwa kimefanya marekebisho makubwa ya kutabu kilichotungwa miaka 40 iliyoipita ambayo yaliweka alama teule ya mwisho ya usalama wa maji na mejimenti ya maji taka
 
Mkurugenzi msaidizi wizara ya Maji na Umwagiliaji Dk George Lugomelo


Mtaalamu wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis,

Wataalamu mbalimbali wakisikiliza mada kwa umakini

GWPP, ni zao la Umoja wa Mataifa lenye lengo la kuandaa kisima cha maarifa kuhusu majitaka, maji salama na usafi binafsi.
Kongamano hilo ambalo lilijadili namna bora ya kudhibiti majitaka na kinyesi barani Afrika lilijadili changamoto zilizopo katika sekta ya majitaka na namna ambavyo watu wanaweza kupata mauii salama kwa matumizi yao.
Katika hotuba yake Futakamba aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanadadavua masuala yote magumu na kuyaelekeza katika kutafuta sulkuhu ya changamoto zilizopo ili sekta ya maji iwe salama na huivyo kusaidia kuendeleza mbele mapambano ya kiuchumi.
Alisema ingawa Tanzania asilimia 93 wanavyoo ni asilimia 24 tu ndio wenye vyoo bora.
Alisema kutokana na watu kuwa na mazoea ya kutumia vichaka na kwenye maji hatari ya kupata magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji machafu kama kuhara na kipindu ni kubwa.
Alisema nchini asilimia 9 ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 na asilimia 6 ya vifo vya watu wazima vinatokana na magonjwa ya kuhara na kipindupindu hivyo ni muhimu wataalamu wakajadili hilo kw akina na kubadilishana uzoefu.
Mtaalamu wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis, amesema kwamba mradi huo utakaokamilika mwakani kwa kutoa kitabu elekezi unafanyiwa kazi duniani kote kwa lengo la kuwa na mfumo unaowiana wa menejimenti ya maji na majitaka.
Alisema kwa sasa  kuna wataalamu 110 kutoka nchi 41 ambao wanakusanya takwimu ili kupata uwiano wa namna bora ya kuendeleza majisalama na kuwa na viwango vya menejimenti ya majitaka na usafi binafsi.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO