Gugu Zulu akiwa na mkewe Letshego
Dereva wa magari ya mashindano nchini Afrika Kusini Gugu Zulu  amekufa wakati akipanda mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.
Zulu, 38, alikuwa mmoja wa washiriki katika upandaji mlima huo kwa hisani kw alengo la kuchangia fedha za ununuzi wa mataulo ya kujisetri wasichana kupitia taasisi ya hisani ya ya Nelson Mandela.
 Zulu na mkewe Letshego walilazimika kukatisha safari yao ya kupanda mlima baada ya  dereva huyo kuanza kujisikia vibaya .
Imeelezwa kuwa wakati akipanda mlima alianza kupata tatizo la kuvuta pumzi na katika chapisho lake la mwisho katika facebook alisema kwamba ana dalili ya mafua makali (flu).
Mshindi mara tatu katika mbio za magari kitaifa nchini Afrika Kusini Zulu pia ni mtangazaji wa kipindi cha  michezo ya mbio za magari


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO