Baadhi ya wakazi wa Mjini Dodoma walijikuta katika tafakari kubwa asubuhi ya leo baada ya kukumbwa na mtikisiko wa ardhi uliosababishwa na tetemeko lililotokea kiasi cha kilomita 76 kaskazini mwa mji huo.
Tetemeko hilo la Richter 5.1. lilitokea saa 06:01:15.2 kitovu chake ni bonde la Haneti - Itiso Wilayani Chemba na lilikuwa na kina cha kilomita 10. Katika ramani ya dunia inaonesdha kwamba limetokea kiasi cha kiliomita 65 Kusini mwa mji wa Kondoa
Akizungumza Ofisi kwake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania Profesa Abdulkarim Mruma alisema tetemeko hilo ni kubwa ukilinganisha na matetemeko ambayo yamezoeleka kutokea ambayo yana ukubwa wa Richter 3.
Alisema mikoa mingine ambayo imeathirika na tetemeko hilo ni Tanga, Dodoma, Singida mashariki  na Manyara.
Kwa upande wake,Mjiolojia Mwandamizi kutoka wakala wa Jiolojia Tanzania mkoani hapa ambaye pia ni mtaalam wa matetemeko Gabriel Mbogoni alisema tetemeko hilo limetokea maeneo ya Haneti kilometa 11 mashariki mwa mji wa Haneti Wilaya ya Chemba ambao upo  kilometa 79 kutoka kaskazini mashariki mwa mji wa Dodoma.
 “Bado hatujapata taarifa zozote za madhara labda kwa sababu bado ni mapema”alisema

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO