Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa kazi za Filamu nchini (hawapo pichani) waliotembelea kujua Urasimishaji wa kazi hizo katika ofisi ya Bodi hiyo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Afisa Utamaduni Bodi ya Filamu, Bw. Romanus Tairo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa filamu nchini walioitembelea Bodi ya Filamu kujua Urasimishaji wa kazi zao, 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Wahifadhi kazi za Sanaa, Bw. Frank Pangoni (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Kampuni ya Salt Inc, Bw. Edwin Musiba (kulia) akifafanua jambo mbele ya Wasambazaji wa filamu wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Wauzaji DVDs Mikononi, Bw. Jumanne China (kulia) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo.
Mwakilishi wa Wauzaji wa Jumla wa kazi za Sanaa, Bw. Augustino Karia (aliyekaa katikati upande wa kushoto) akimweleza jambo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu (wa pili) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo.

 (Picha zote na Benedict Liwenga)

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO