Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi (kulia) akimkaribisha Naibu Waziri – TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (kushoto) kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.


Naibu Waziri – TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo akiongozana na Naibu Katibu Mkuu – TAMISEMI Dr. B.M. Makali wamefika Mkoani Lindi kuembelea Shule ya Sekondari Lindi iliyoteketezwa kwa moto.

Mh. Naibu Waziri alipokelewa na Viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi. Baada ya mapokezi alitembelea shule ya sekondari Lindi naa kujionea majengo ambayo yameungua ambapo pia alielezwa jitihada mbalimbali ambazo zimechukuliwa na Serikali ya Mkoa.
 
Naibu Waziri TAMISEMI akiwa katika moja ya maabara ambayo imeungua kwenye paa peke yake.

Naibu Waziri TAMISEMI akiwa anakagua majengo ya madarasa yaliyoungua na moto.

Naibu Waziri TAMISEMI akiwa anakagua majengo ya madarasa yaliyoungua na moto.

Naibu Waziri TAMISEMI akiwa anaongea na walimu pamoja na wataalam ambao wanafanya kazi ya tathmini ya athari za moto.Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa wanafunzi wote wahakikishe wanariopoti shule kwa wakati kwani serikali ya Mkoa imeshajipanga katika kukabiliana na changamoto iliyopo ya madarasa yaliyoungua. Pia amewataka wazazi na walezi wote kutokuwa na hofu kwani majengo mengine ya shule yapo salama.

Vilevile amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kwa ujumla kuchangia fedha na mali zitakazosaidia katika kukarabati miundombinu ya shule. Aidha, alieleza kuwa serikali imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule za sekondari 33 za zamani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO