Messi na baba yake Juni mwaka huu
MSHAMBULIAJI  wa timu ya taifa ya Argentina na timu ya Barcelona Lionel Messi  amehukumiwa jela miezi 21 kwa kukwepa kulipa kodi.
Baba yake  Jorge Messi,pia amepewa adhabu kwa kukwepa kulipa kodi Hispania ya  ya dola za Marekani  milioni 4.5 kati ya mwaka 2007 na 2009.
Hata hivyo mchezaji huyo na baba yake hawatatupwa jela kwa kuwa kwa mujibu wa sheria za Hispania  kifungo chini ya miaka miwili kinaweza kutekelezwa mtuhumiwa akiwa nje.
Aidha watu hao pia watatozwa faini kwa kukwepa kulipa kodi kwa kupeleka fedha za mapato yao nchini Belize na Uruguay.
Watu hao walipatikana na hatia katika tuhuma tatu  za kukwepa kodi katika mahakama ya Barcelona.
Messi  alipigwa faini ya Euro milioni  2 na baba yake euro milioni 1.5.
Wakati  wa kesi Lionel Messi  alisema kwamba hajui chiochote kuhusiana na masuala yake ya fedha kwani yeye kazi yake ni kucheza mpira.
Baba mtu naye  alisema kwamba hilo ni tatizo la washauri wa fedha.
Lionel Messi amestaafu kucheza mpira wa kimataifa mwezi uliopita na amekuwa mchezaji  bora wa FIFA  amara tano ni miongoni mwa wachezaji tajiri sana duniani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO