Maalim Seif kuburuzwa mahakamani kwa uchochezi

MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amefunguka kuhusu mambo juu ya utendaji wa jeshi hilo na kueleza kuwa wakati wo...


MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amefunguka kuhusu mambo juu ya utendaji wa jeshi hilo na kueleza kuwa wakati wowote litamburuza mahakamani Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuhamasisha uchochezi visiwani Zanzibar.
Amebainisha kuwa jeshi hilo, kamwe halikandamizi wala kuonea chama chochote cha siasa, kwani limekuwa likitekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
Akizungumza katika mahojiano yaliyofanyika kwenye kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Azam jana, IGP Mangu alisema hali ya siasa Zanzibar ilikuwa shwari katika chaguzi zote mbili na kwamba machafuko na vurugu vilianza kutokea baada ya uchaguzi wa pili.
Alisema vurugu hizo zilianza baada ya kubainika kuwa Maalim Seif, alikuwa akifanya mikutano ya ndani na mingine ya chini kwa chini na wafuasi wake katika maeneo ya Kaskazini na Kusini.
“Kwa sababu ilikuwa ni mikutano ya ndani, Polisi hatukuona tatizo na wala hatukumzuia, tuliona ni mwananchi anataka kuzungumza na wafuasi wake, tukasema mwache aongee nao tu,” alisema IGP Mangu.
Alisema baadaye jeshi hilo liligundua kuwa kiongozi huyo wa CUF, alikuwa anawachochea wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani na wapinzani wao ambao ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwafanyia uhalifu.
Alisema baada ya vikao hivyo vya Maalim Seif, visiwani humo kukaanza kuibuka matukio ya vurugu kama vile mashamba kuchomwa moto na mazao kung’olewa.
“Haya mambo hayakutokea kabla ya vikao vya Seif, yalitokea baada ya vikao vyake,” alifafanua mkuu wa polisi.
Alisema wafuasi hao walichochewa, kiasi cha kususa hadi shughuli za kijamii, kama vile misiba na wakati mwingine ilifikia hatua ya kususa kuwauzia bidhaa wafuasi wa CCM.
“Tukasema kama wameona kugeuza biashara zao siasa, basi waendelee tu. Biashara inadumu kwa sababu unatengeneza faida, sasa kama umeamua kuchagua wa kumuuzia ni shauri yako. Hawa tuliwaacha kwa sababu tuliona hawana makosa,” alisema.
Hata hivyo, alisema jeshi hilo kamwe halikuwanyamazia wahalifu waliochoma na kung’oa mazao kwenye mashamba ya wenzao, eti tu kwa kigezo cha ufuasi wa chama au siasa.
“Hawa tuliwakamata na wapo wengine tunaendelea kuwatafuta, watakapoacha ndio hatutawatafuta. Wale wahalifu ndio tunaowatafuta. Pengine kwa sababu ya siasa wanadhani Polisi tunawaonea wananchi tunawakamata bila sababu. Sasa hawa watu tunawaoneaje wakati tunawapeleka mahakamani?” Alihoji.
Maalim Seif kuhojiwa Alisema kutokana na matukio hayo, tayari Maalim Seif amehojiwa na jalada lake halijaamuliwa, lipo kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) Zanzibar. “Lakini pia tunataka tumpeleke mahakamani kumshitaki kwa makosa aliyofanya ya kuchochea fujo,” alieleza.
Alisema kazi kubwa ya Polisi kwa sasa si kujiingiza kwenye siasa au kupatanisha pande mbili zinapokwaruzana, bali kazi yake ni kuhakikisha inadhibiti na kuwakamata wahalifu.
Alisema endapo vyama viwili vinavyolumbana visiwani Zanzibar, vitaamua kuchukua hatua za kisheria kumaliza tofauti zao, polisi haina tatizo, lakini endapo vyama hivyo vitachukua hatua za kijinai au kukomoana, jeshi hilo halitokaa kimya.
“Kazi ya polisi iko wazi, tunakamata tunapeleleza na kupeleka mahakamani umma unatuona tunachofanya hatuna cha kuficha,” alisisitiza.
Maandamano na mikutano
Akizungumzia madai ya jeshi hilo kukandamiza demokrasia na wapinzani kwa kudhibiti shughuli za siasa nchini, IGP Mangu alisema hakuna mwanasiasa au chama chochote, kilichozuiwa kufanya shughuli zake, ikiwemo mikutano.
Alisema kinachotakiwa ni kwa mwanasiasa au chama hicho, kupeleka maombi yake Polisi kwa mujibu wa sheria na baada ya jeshi hilo kufanyia tathmini maombi hayo, endapo yataonekana hayana tatizo yataruhusiwa kuendelea.
Alisema endapo jeshi hilo linazuia shughuli za kisiasa, hutokana na uchunguzi au tathmini lililofanya na kujiridhisha kuwa shughuli husika si salama na inatishia usalama wa raia.
“Unajua unapozungumzia masuala hayo tuwe makini kidogo, kwa sababu hapa kuna watu wa aina mbili kuna wanaofanya siasa na sisi watendaji tunaotekeleza sheria. Ila sisi pia hatuko juu ya sheria, kama kuna mahali tunakiuka upo utaratibu wa kutushughulikia,” alisisitiza.
Alisema hata katika suala la kuzuia shughuli za kisiasa, kama vile mikutano na maandamano endapo, kuna chama au mwanasiasa anahisi kuwa jeshi hilo, halikutenda haki au limeenda nje ya mstari, taratibu zinamruhusu kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais na Mahakama.
Hata hivyo, alisema jeshi hilo halifanyi jambo lolote nje utaratibu wa kisheria, akifafanua, “lakini sisi hatuwezi kujiingiza kwenye siasa kwa sababu sisi sio wanasiasa, pia hatuwezi kuzuia wanasiasa kulumbana kwa sababu ni uwanja wao wa kulumbana. Sasa kama tulitoa maelekezo fulani basi ujue tulikuwa tunatekeleza sheria na utaratibu uliopo.”
“Sidhani kama sisi tunakandamiza upinzani, tunachofanya sisi ni kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na watu wako huru kama wanafikiri tumeenda nje ya mipaka yetu wakatuchukulie hatua,” alisisitiza.
Alitoa mfano wa matukio yaliyozuiwa na Polisi kwa sababu za kiusalama kuwa ni pamoja na mkutano wa mahafali wa Dodoma, ambao ulifanyika siku moja na mkutano wa mahafali uliofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam ambao wenyewe haukuzuiwa. Yote ilikuwa mikutano ya wanafunzi wafuasi wa Chadema.
“Kama sisi tuna sera ya kuzuia, mbona wa Karimjee hatukuuzuia? Dodoma kulikuwa na sababu na imeelezwa na viongozi wa Dodoma. Hii si sera yetu, usichukulie mkutano mmoja kuzuiwa basi ndio yote nchi nzima imezuiliwa. Haiwezekani,” alifafanua.
Alisema sheria inazungumzia wanaohitaji kufanya mkutano au kufanya maandamano, wanatoa taarifa kwa mkuu wa polisi wa hilo eneo, na mkuu huyo ataangalia kama mazingira yanaonesha hakuna tatizo, mkutano utaendelea, kama kuna tatizo atauzuia.
“Sasa ni wapi sisi tumefanya kitu ambacho ni kinyume na tunaonekana tunakandamiza upinzani? Na ikumbukwe kuwa kuna mikutano baadhi iliombwa tukaizuia kwa sababu kipindi hicho kulikuwa na kelele za mauaji Mwanza, Sengerema, Tanga mpaka tunahojiwa Polisi mko wapi,” alisema.
Alisema wakati Polisi ikihojiwa kuhusu dawa ya mauaji, baadhi ya vyama viliwasilisha maombi ya maandamano.
“Hivi kweli? Kwanza mauaji yenyewe mtindo wake ni mpya unajuaje kama wanaoomba wangeenda nao kuvamiwa? Lazima tuchukue tahadhari,” alisema na kuongeza kuwa Polisi imepewa jukumu la kisheria kuhakikisha panakuwepo na amani. “Sasa tunapochukua hatua kuhakikisha kuna amani, naomba tuvumiliane. Msione kuna amani, basi mkajua ipo tu na ni ya kudumu, mjue kuna wengine wameumia kuhakikisha hiyo amani inakuwepo. Lazima iwe hivyo ndio utaratibu wa kuongoza nchi, sisi hatubagui wala kukandamiza chama chochote,” alieleza IGP Mangu.
Matumizi ya nguvu
IGP Mangu alisema si kweli jeshi hilo limekuwa likitumia zaidi nguvu katika kudhibiti vurugu na kubainisha kuwa nguvu hutumika, pale tu inapobainika kuwa upande wa pili unaodhibitiwa nao unatumia nguvu.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa Polisi nchini imekuwa ikitekeleza wajibu wake vyema bila kukandamiza wala kutumia nguvu, kwani hata taasisi ya kimataifa iliyofanya tathmini juu ya utendaji wa jeshi hilo katika uchaguzi mkuu nchini ilibainisha kuwa jeshi hilo lilifanya vyema.
Polisi na rushwa Akizungumzia tuhuma zinazorushiwa Jeshi la Polisi kwamba kuna baadhi ya askari wake, wanatuhumiwa kwa rushwa, alisema askari hawana mamlaka ya kula rushwa na kujilimbikizia mali halafu wasiguswe na mtu.
“Hili haliwezekani. Kwa hiyo nasema bado wananchi wanaweza wakasaidia kama kweli wanazo taarifa za Polisi na zitafanyiwa kazi. Kama hawaamini kama sisi wenyewe hatuwezi kudhibitiana, vipo vyombo vingine vinaweza kufanya hivyo,” alisema.
Hata hivyo, alisema wapo askari Polisi wenye maisha mzuri kwa maana ya nyumba na magari, ambao wamepata mali hizo kupitia taasisi mbalimbali za mikopo ikiwemo Saccos ya Polisi, ambayo ndio kubwa nchini.
“Askari polisi kumiliki gari nzuri si kosa, la msingi amepataje hilo gari, kama kuna polisi ana mali au gari isiyo na maelezo tuleeteni, polisi hazuiliwi kuwa na gari nzuri. Siku hizi kuna taasisi nyingi zinakopesha anaweza kukopa,” alisisitiza.
Kashfa ya Lugumi
Akizungumzia suala la kashfa ya mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, IGP Mangu alisema suala hilo lilichukuliwa na Bunge na kufanyiwa uchunguzi hivyo, matokeo ya uchunguzi hawezi kuyazungumzia.
Alisema anachoweza kukizungumzia ni maelekezo ambayo jeshi hilo limepatiwa na Bunge, ambayo ni kukamilisha yale ambayo hayajakamilishwa.
“Tunaendelea kuchukua hatua za kukamilisha.Kuhusu uchunguzi kazi ilifanywa na Bunge kwa anayetaka anaweza kuwasiliana na Bunge na kupatiwa matokeo kwa kuwa naamini Bunge linawakilisha wananchi, taarifa zao ziko wazi,” alisema.
 Source:Halima Mlacha, Habarileo

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4811,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Maalim Seif kuburuzwa mahakamani kwa uchochezi
Maalim Seif kuburuzwa mahakamani kwa uchochezi
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2016/07/maalim-seif-kuburuzwa-mahakamani-kwa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2016/07/maalim-seif-kuburuzwa-mahakamani-kwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy