WANANCHI zaidi ya 11,000 kutoka katika vijiji vitatu vya Malinyi, Kipingo na Makere, wilaya mpya ya Malinyi, mkoa wa Morogoro watanufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika ujenzi wa skimu ya maji ya mserereko.
Mradi huo ambao unaendelea kujengwa utakuwa na vituo 47 vya kuchotea maji na baada ya kukamilika utawanufaisha wananchi wa vijiji vya Malinyi, Kipingo na Makere.
Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Majura Kasika,alisema hivi karibuni ( julai 15)  mjini Malinyi, kuwa pamoja na vituo hivyo 47 pia mradi wa uchimbaji wa visima virefu saba utafanyika katika kijiji cha Ngoheranga  na  visima sita katika kijiji cha Tanga .
“ Tayari visima saba vimepatikana kimoja katika kijiji cha Sifi Majiji na sita katika kijiji cha Ngoherenga , ambapo mradi huu utawezesha kutoa huduma ya maji safi nasalama kwa zaidi ya watu 4,000” alisema Kasika.
Mkuu wa wilaya ya Malinyi, alisema wilaya ina visima vifupi vya maji 182 , visima virefu vitano na skimu tatu za maji ya bomba zinazoendeshwa na kumilikiwa na wananchi kupitiaa kamati za maji na Jumuiya za watumia maji.
Licha ya juhudi na mikakati hiyo mkuu huyo wa wilaya alisema,  hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama  katika wilaya hiyo si ya kuridhisha ambapo huduma ya maji inapatikana kwa asilimia 53 pekee.
Source:John Nditi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO