MARAIS wastaafu wa Marekani wamewekewa kima cha mwisho cha fedha  za matumizi huku wakipunguziwa fedha hizo kwa jinsi wanavyoingiza katika kazi zao binafsi .
Bunge la Marekani Ijumaa iliyopita lilipitisha akaunti za matumizi za viongozi hao kuhusu safari, wafanyakazi na gharama za ofisi kuwa dola laki mbili na kwamba kiwango kitapungua kama rais ataingiza katika shughuli zake dola laki nne kwa mwaka.
Waliotengeneza muswada huo wamesema kwamba viongozi wengi wa taifa hilo hawahitaji kodi za wananchi wa Marekani kwani wanatengeneza mamilioni katika shughuli zao binafsi baada ya kustaafu.
"Baada ya kuystaafuy wengi wa marais wanatengeneza mamilioni ya fedha na hawahitaji fedha za walipa kodi," wanasema waliotengeneza muswada huo, wawakilishi Elijah Cummings wa Maryland  na Jason Chaffetz wa Utah katika taarifa yao ya pamoja.
Mwaka  2014 walipa kodi wa Marekani walikamuliwa dola za Marekani  milioni 3.5 kwa ajili ya marais wane ambao wamestaafu nchini humo.
Hizo ni pamoja na dola milioni 1.3 kwa ajili ya  George W. Bush  na dola 950,000 kwa ajili ya Bill Clinton na nyingi ya gharama hizo ni kwa ajili ya kulipia ofisi.
Chini ya mpango mpya posho hiyo itakatwa kwa dola katika kila dola inayoingizwa na viongozi hao  zaidi ya dola  laki nne kwa mwaka.
Gharama hizo hazitahusisha gharama za ulinzi na usalama wao.
Aidha pensheni za marais hao ni dola za Marekani laki mbili kwa mwaka huu huku wake zao kama watakuwa wamekufa na bado wanaishi wataendelea kupokea dola za Marekani laki moja kwa mwaka.
Bunge lilipitisha muswada huo kwa kura za mdomo za ndiyo au hapana sasa inasubiri saini ya Obama

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO