JUMLA ya miili 13 kati ya 28 ya waliofariki kwa ajali ya ya mabasi ya
City Boys iliyotokea juzi katika eneo la Maweni wilaya ya Manyoni
mkoani Singida imetambuliwa.

Mamia ya wananchi kutoka mkoani Dodoma na mikoa jirani jana
walikusanyika  nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Dodoma kwenda kutambua ndugu zao waliokufa kwa ajali
hiyo.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi
wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Dk Ibenze Ernest alisema
miongoni mwa  maiti 28,ni 13 tu ndizo zilizotambuliwa.
“Maiti nyingi bado hazijatambuliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo
kuumia vibaya na kuondoa muonekano wao halisi huku wengine wakiwa
wamegawanyika viwiliwili na vichwa” alisema.

Dk Ibenze aliwataja marehemu waliotambuliwa kuwa ni  Ismail Bashe,John
Lukanda,Paul Mfaume,Dickles Kwabugili,Rabia Lema na Levoso Israel .

Wengine ni Paulina Martine, Resta Exavery,Kefun Deus,Charles
Mamunyi,Betty Zumbe,Jesca Lazalo na Leonard Chacha.

 Aidha  aliwataja majeruhi saba ambao bado wanaendelea kupatiwa
matibabu kuwa ni Katra Abubakari (12) ambaye amevunjika miguu yote
miwili na amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi, Athuman George mkazi wa
Geita,Jamila Mathias mkazi wa Shinyanga, Monza Labani Mkazi wa
Nzega,Disko Wabare mkazi wa Kahama ambaye ni Katibu wa Wazazi wa CCM
wilaya ya Kahama na mwingine ambaye hajatambulika ambaye pia amelazwa
wodi ya wagonjwa mahututi na majeruhi moja aliyetambuliwa kwa jina la
Mujaidi,

 Hata hivyo Dk.Ibenze alisema,majeruhi waliofika hospitalini hapo ni
majeruhi 15 ambapo baadhi yao walitibiwa na kuruhusiwa huku wengie
watano wakifanyiwa upasuaji kutokana na mahitaji ya matibabu yao.
Alisema,maiti nyingi bado hazijatambuliwa kwa sababu mbalimbali
ikiwemo kuumia vibaya na kuondoa muonekano wao halisi huku wengine
wakiwa wamegawanyika viwiliwili na vichwa.

“Sababu ya kutotambuliwa kwa idadi kubwa ni kutokana na ndugu wengi
kutofika,kuumia vibaya lakini pia vichwa vingi vipo peke yake na miili
ipo peke yake.”alisema Dk.Ibenze

Dk.Ibenze ambaye ni Daktari bingwa wa mifupa
akizungumzia changamoto alisema ni majeruhi kuchelewa kufikishwa
hospitalini huku akisema,miili ya marehemu ndio iliyotangulia kuingia.

“Changamoto tuliyokutana nayo ni wagonjwa kufikishwa hosptalini
kupatiwa matibabu,wakati miili ya marehemu iliwasili hospitalini hapo
majira ya saa 11 jioni.”

 Mmoja wa watu waliofika kutambua maiti wa ajali hiyo jana alasiri,
Said Musa mkazi wa Dodoma ambaye aliweza kutambua ndugu watatu wa
familia moja.
“Mwanaume aliyekufa na familia yake anafahamika kwa jina la Peter
Sinton a mkewe namfahamu kwa jina moja la Rose ila sijui jina la
motto” alisema

Alisema,Marehemu Peter ni mwalimu katika shule ya Sekondari Mtibwa
mkoani Morogoro na alikuwa akitokea mkoani Tabora kumtambulisha
mwanamke aliyezaa nae (Rose) wa wazazi wake.

Miili yote imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya Rufaa ya Dodoma huku zoezi la utambuzi likiendelea.
Source:  Sifa Lubasi, Dodoma

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO