Mke wa rapa Kanye West , Kim Kardashian amekanusha kuongeza makalio yake na kusema kwamba anajiamini hahitaji ongezeko  lolote.
Aidha anasema kwa sasa watu wameshaona makalio yake na anaamini wanamjua kwamba hahitaji ongezeko,lolote lile, yeye yuko bomba.
Alisema hayo kupitia tovuti yake.
Kumekuwepo na kelele katika mitandao ya kijamii kwamba mdada huyo anaongeza vitu kuweka shepu yake kuwa na  kalio la nguvu baada ua mpigapicha mmoja kuona kitu kama michirizi inayofanana kabisa na mwisho wa alama za ongezeko la makalio.
Hayo yalionekana wakati mdada huyo alipoenda kuhudhuria mchapalo wa mdogo wake Khloe Kardashian, kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake ambaye alitimiza miaka 32  Jumatatu ya Juni 27 mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika Dave & Buster’s huko L.A. Marekani.
Sketi yake ya kidizaini inayobana aliyovaa ilionesha kitu kama mwisho wa viongeza makalio.
Kardashian, 35, alisema katika webu yake kwamba huo ulikuwa uzushi usiokuwa wa maana na kwamba miaka michache iliyopita kwa bahati mbaya alivaa nguo ambayo ilionesha makalio yake  na akaudhiwa na hilo na tangu wakati huo anahakikisha kwamba  anaweka kitu kingine ili kuzuia kuonekana kwa makalio yake ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi kutokana na nguo anzovaa.
Anasema yeye anachovaa sio butt pads bali shapewear.Anasema anaamini kwamba kila mtu ameshaona makalio yake kutokana na uzembe ule na kwamba wanajua hahitaji kuweka viongeza makalio.

Hata hivyo Aprili mwaka huu mdada huyo alisema kwamba wakati mwingine akiwa katika siku zake anavaa jozi kadha za shapewear ili ajisikie salama katika shughuli zake.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO