BATON ROUGE, La.  Marekani— POLISI watatu wameuawa na mtu asiyejulikana na wengine saba kujeruhiwa katika eneo Baton Rouge, La., Mkuu wa polisi wa East Baton Rouge Parish Sheriff’s  amesema
Tukio hilo limefanyika  katika kipindi kisichotimia wiki mbili tangu mwamwerika mweusi alipouawa na polisi na kusabisha maandamano makubwa.
Inaaminika kwamba mtu alioyeua polisi hao naye ameuawa.
Msemaji wa polisi Cpl. L’Jean McKneely anaamini kwamba mtu huyo aliuawa na risasi kutoka bunduki za Polisi.
Hata hivyo polisi hao wamesema kwamba awali walikuwa wanamsaka mtu mwingine lakini baadae waliona kwamba mtu huyo alikuwa peke yake.
Mkuu wa Polisi wa Louisiana, Col. Michael Edmonson, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mtu huyo aliuawa na maofisa waliofika kujibu milipuko ya risasi na kwamba wanaamini alikuwa peke yake.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO