IMEELEZWA kuwa mcheza sinema za watu wazima , sinema za ngono, Amber Rayne (31) alibwia unga wa kutosha aliochanganya na pombe kwa kipindi cha saa 13 cha kujidunga, hali iliyompelekea  kufa.
Mcheza sinema huyo alikufa Aprili mbili  mwaka huu.
Imeelezwa kuwa katika kujidunga huko alikuwa na rafiki yake Roy Poole ambaye alimuita nyumbani kwake San Fernando Valley karibu na  Sun Valley mara tu baada ya kuwasili kutoka katika safari yake.
Taarifa ya uchunguzi inasema kwamba Roy na  Rayne walitumia gramu mbili za kokeini na kunywa pombe.
Roy alithibitisha kwamba walianza kunywa pombe wakichanganya na kokeini kuanzia saa saba na nusu usiku na ghafla saa nane na dakika 40 Rayne alisimama na kuanguka akiwa hajitambui.
Poole alipiga simu 911,  lakini pamoja na juhudi zote za kuokoa maisha yake Rayne alitangazwa amekufa saa 9 na dakika 16 jioni yake.
Kwenye taarifa hiyo imesema kwamba hapakuwepo na dalili za kufanyiwa vurugu katika mwili wake.
 Baada ya kifo chake  wanafamilia walisema kwamba  ndugu yao alikuwa na tatizo la kujidunga.
Rayne,ambaye jina lake la ukweli ni Meghan Wren,  alizaliwa Detroit na kukulia kaskazini mwa California.
Mdada huyu aliingia katika sinema za wakubwa mwaka 2005 na kujinyakulia sifa mbalimbali pamoja na tuzo ya AVN kwa filamu yake ya Unsung Starlet of the Year mwaka 2009.Tuzo hiyo katika tasnia ya filamu za wakubwa inafanana na ile ya Oscar.
Rayne, ambaye pia anamiliki shamba la farasi alitangaza kustaafu kuigiza sinema za ngono mwaka 2015 hata hivyo alirejea tena kucheza Wanted . Pamoja na kucheza sinema za wakubwa pia  alikuwa ni dairekta, projuza na mhariri.
Katika maisha yake ya kawaida imeelezwa kuwa Rayne alikuwa katima mfumo wa maisha wa BDSM katika maisha yake nje na ndani ya sinema.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO